1008. MUSI NIMO

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya milimo. Alihoyi munhu umo uyo otumamaga milimo yakwe bho makanza malihu bhuli lushigu. Abhanhu abho bhangenihaga aha kaya yakwe bhangayiyagwa mpaga bhanondeja guko milimo yakwe kunguno oliatogilwe gutumama milimo yakwe yiniyo. Hunagwene oyombaga giki, “musi milimo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga gutumama milimo yakwe mpaga opandika sabho ja guilisha chiza ikaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agamishaga diyu ogatumama milimo mitale bhuli lushigu kunguno ahayile guibheja chiza ikaya yakwe, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi ja gudula guyilanhanila chiza ikaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo otumamaga milimo yakwe bho makanza malihu bhuli lushiku mpaga nose upandika sabho ningi, kunguno nuweyi agipunaga diyu agigulambija kutumama milimo bhuli lushigu, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “musi nimo.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gwiyumiliga gutumama milimo yabho mpaga bhapandike sabho ja gubhambilija chiza umuwikaji bhobho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho.

Mwanzo 2:15.

Mithali 18:20.

Mithali 21:5.

KISWAHILI: DUNIANI KAZI.

Msemo huo waongelea juu ya kazi. Alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa akifanya kazi zake kwa muda mlefu kila siku. Watu waliomtembelea walilazimika kumfuata kwenye kazi zake hizo kwa sababu alipenda kufanya kazi zake hizo. Ndiyo maana aliwaambia watu kwamba, “duniani kazi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kufanya kazi zake mpaga anapata mali za kuilisha vizuri familia yake. Mtu huyo, hujilawa asubuhi na mapema kwenda kufanya kazi kubwa kila siku kwa sababu anapenda kuiedeleza vizuri familia yake, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi za kuweza kuitunza familia yake hiyo, kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kufanya kazi, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwa akifanya kazi kwa muda mlefu kila siku mpaga mwishowe alipata mali nyingi, kwa sababu naye hujilawa asubuhi kwenda kujibidisha kufanya kazi kubwa kila siku, katika maisha yake. Ndiyo maana watu waliomuona walifahamu kwamba, “duniani kazi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuvumilia kufanya kazi zao mpaka wapate mali za kuwasaidia vizuri maishani mwao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Mwanzo 2:15.

Mithali 18:20.

Mithali 21:5.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.