sayings

1231. GEHYAGA (LEKAGA) IMHEMBE.

Imbuki ya kahayile kenako, ilolile munhu uyo ofulaga mhembe. Umunhu ng’wunuyo, oifulaga imhembe yiniyo pye amakanza, nose abhiye bhoya ugutogwa kunguno obhayoganijaga noyi. Abhanhu bhenabho bhagayung’wila giki agehye nulu aleke uguifula imhembe yakwe yiniyo. Hunagwene bhagang’wila giki, “gehyaga (lekaga) imhembe.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga uyomba mihayo iyo idinasolobho, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agayombaga bhuli mhayo bho nduhu ugugwikanika chiza isolobho yago, kunguno ya gugayiwa witegeleja, umumahoya gakwe genayo. Uweyi agagaiyagwa abhanhu bha guhoya nanghwe kunguno ya guyomba mihayo iyo idinasolobho yiniyo, umumahoya gakwe genanyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agabhayoganijaga abhiye bho gufula mhembe yakwe, kunguno nuweyi agayomba mihayo iyo idinasolobho, umumahoya gakwe genayo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “gehyaga (lekaga) imhembe.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuleka guyomba mihayo iyo idinasolobho bho guyomba iyo idulile gubhambilia chiza umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule kujilela chiza ikaya jabho.

Mathayo 23:14.

KISWAHILI: PUNGUZA (ACHA) FILIMBI.

Chanzo cha msemo huo, huangalia mtu anayepuliza filimbi. Mtu huyo, huipuliza filimbi hiyo muda wote mwishowe wenzake hukerwa na sauti hiyo kwa sababu ya kuwapigia kelele. Watu hao walianza kumwambia apunguze au aache kuipuliza filimbi hiyo. Ndiyo maana walimwambia kwamba, “punguza (acha) filimbi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huongea maneno yasiyo na faida, katika maisha yake. Mtu huyo, huongea kila neno linalomjia bila ya kulifikiria vizuri kuwa linafaida gani, kwa sababu ya kukosa umakini huo, katika maongezi yake. Yeye hukosa watu wa kuongea naye kwa sababu ya kukosa umakini huo katika maongezi yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewapigia kelele wenzake kwa kupuliza filimbi yake, kwa sababu naye huongea maneno yasiyo na faida, katika maongezi yake hayo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “punguza (acha) filimbi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha kuongea maneno yasiyo na faida maishani mwao, kwa kuyaongea yale yanayoweza kuwasaidia katika kujipatia maendeleo yao, ili waweze kuzilea vizuri familia zao.

Mathayo 23:14.

ENGLISH: REDUCE (LEAVE) THE WHISTLE.

This saying looks at a person who blows a whistle. This person blows such whistle all the time and eventually his colleagues get annoyed by the sound that shouted at them. These people started telling him to slow down or stop blowing the whistle. That is why they told him that, “reduce (leave) the whistle.”

This saying is compared to the person who speaks useless words in his life. Such person speaks every word that comes to him without thinking about what it is good for, because of lacking focus in his speech. He misses people to talk to because of such lack of focus in his speech.

This person resembles the one who yelled at his colleagues by blowing his whistle, because he also speaks useless words in his speech. That is why people tell him that, “reduce (leave) the whistle.”

This saying teaches people to stop speaking useless words in their lives, by speaking those that can help them in their development, so that they can raise their families well.

Matthew 23:14.

music-4408810_1280

maasai-men-6792090__480

gambia-239849__480

1230. TULAGA NGASHI.

Imbuki ya kahayile kenako, ihoyelile nimo go ngashi. Ungashi gunuyo jiliginhu ja gutinila myenda nulu gumogela nzwili. Olihoyi munhu uyo alina nzwili ndihu mpaga jubhipila ukuntwe gokwe gunuyo kunguno ya gujileka shigu ningi bho nduhu ugujitina. Abhanhu bhagayung’wila giki atijine kugiki abhelele ukuntwe gokwe gunuyo. Hunagwene bhagang’wila giki, “tulaga ngashi.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli ntongeji o bhatumami uyo agabhapejaga umumilimo abhatumami abho bhadatumamaga chiza imilimo iyo agabhinhaga. Umunhu ng’wunuyo, agabhagabhilaga milimo abha bhatumami bhokwe na gubhimila chiza kugiki bhadule gutumama chiza, kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho, umukilile kakwe. Uweyi abhagapejaga bhatumami abho bhagadumaga uguitumama chiza imilimo yakwe, kunguno adahaile gukenagujiwa milimo yakwe, umubhutumami bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabho bhagang’wila uo nzwili ndihu giki ajitile, kunguno nuweyi agabhinjaga umumilimo bhatumami abho bhadatumamaga chiza imilimo yakwe. Hunagwene agabhawilaga abhiye giki, “tulaga ngashi.”

Akahayile kenako, kalanga bhatumami bha milimo higulya ya guitumama chiza imilimo yabho, kugiki bhadule gwendelea na bhutumami bhobho bhunubho chiza, umuwikaji bhokwe.

Mwanzo 3:14-24.

Mwanzo 4:1-16.

KISWAHILI: PIGA MKASI.

Chanzo cha msemo huo, huongelea juu ya kazi za mkasi. Mkasi huo, ni kitu cha kukatia nguo, au kunyolea ng’wele. Alikuwepo mtu aliye kuwa na nywele ndefu kichwani mwake mpaka zikamfanya aonekane vibaya kwa wenzake kwa sababu ya kuziacha kwa muda mrefu bila kuzikata nywele hizo. Watu walianza kumwambia kwamba azikate ili kichwa chake kipendeze. Ndiyo maana walimwambia kwamba, “piga mkasi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa kiongozi anayewasimamia watu wake vizuri katika kazi zao. Mtu huyo, huwagawia kazi wafanya kazi hao na kuwasimamia vizuri kwa sababu ya unyofu wake huo, katika utumishi wake. Yeye huwafukuza kazi wafanya kazi wanaoshindwa kuyatekeleza vizuri majukumu yao, kwa sababu ya kutokupenda kazi yake iharibiwe na watendaji hao walio wavivu, katika utumishi wake huo.

Mtu huyo, hufanana na wale waliomwambia mwenye nywele ndefu azikate, kwa sababu naye huwafukuza kazi wale wasioweza kuyatekeleza vizuri majukumu yao, katika mshamba yake. Ndiyo maana huwaambia wenzake kwamba, “piga mkasi.”

Msemo huo, hufundisha wafanya kazi juu ya kuyatekeleza kwa makini majukumu yao ya kila siku kwenye kazi zao, ili waweze kupata nafasi ya kuendelea kubaki katika kazi zao hizo, maishani mwao.

Mwanzo 3:14-24.

Mwanzo 4:1-16.

 ENGLISH: BEAT SCISSORS.

The source of this saying talks about works of scissors. The scissors are tools for cutting clothes, or shaving hairs. There was a man who had long hairs on his head until them made him look badly to his colleagues because he left them for a long time without cutting them. People started telling him to cut them so that his head would look nice. That is why they told him that, “beat scissors.”

This saying is equated to a leader who manages his people well in their works. That person, assigns work to those workers and supervises them well because of his sincerity, in his service. He fires workers who fail to perform their duties well, because he does not like his work to be ruined by those lazy workers, in his service.

This person is similar to those who told the one who had long hears to cut them, because he also fires those who cannot perform their duties well, in his field. That is why he tells his colleagues that, “beat scissors.”

This saying imparts in workers an idea to carefully carry out their daily duties in their works, so that they can have a chance to continue staying in their works, in their lives.

Genesis 3:14-24.

Genesis 4:1-16.

hairdresser-3572051_1280

1228. KOLAGA BHUGILIMILAGA UKO ALIJA.

Olihoyi munhu uyo omanaga usamila muchalo jingi ijo bhaponaga jiliwa abhanhu. Umunhu ng’wunuyo, obhizaga giki, ulu ogakela uko chalo ijo osamilaga jinijo osamilaga kuchalo jingi hangi uko wigwaga giki bhaponile ijiliwa. Uweyi okelaga ijiliwa kunguno ya gukija uguidilila chiza imigunda iyo oilimaga bho guilimila ingese pye iyose. Hunagwene abhanhu bhagaiwila giki, “kolaga bhugilimilaga uko alija.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu ngokolo ugutumama imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunyo, agalimaga migunda yakwe okija ugumala uguilimila ingese kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga ukoya na nzala aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho, ubhoguduma uguilimila pye ngese ya mumigunda yakwe, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo okelaga ijiliwa osamila muchalo jingi, ijo bhaponaga, kunguno nuweyi agalimaga imigunda yakwe oduuma uguilimila ingese pye iyose, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “kolaga bhugilimilaga uko alija.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umukaya jabho.

Methali 27: 11-15.

Mhubiri 10:18.

KISWAHILI: KWANI PALIZI HUJIPALILIA ANAKOENDA!

Alikuwepo mtu ambaye alikuwa akihamia kwenye kijiji walichopata chakula vizuri kwa mwaka huo. Mtu huyo, alikuwa akikosa chakula kwenye kijiji hicho kwa mwaka huo alihamia kwenye kijiji kingine alichosikia kuwa watu wake walipata mazao mengi ya chakula. Yeye alikuwa akikosa chakula katika familia yake kwa sababu ya kutoyatunza vizuri mashamba yake aliyoyalima kwa kuipalilia palizi mpaka kuimaliza. Ndiyo maana watu walisema juu yake kwamba, “kwani palizi hujipalilia anakoenda!

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mvivu kufanya zake, katika maisha yake. Mtu huyo, hulima mashamba ya chakula na kuacha bila kuyapalilia palizi kwa sababu ya uvivu wake huo, maishani mwake. Yeye alikuwa akihangaika na tatizo na njaa katika familia yake hiyo, kwa sababu ya uvivu wake huo, wa kushindwa kupalilia palizi yote ya kwenye mashamba yake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekosa chakula katika kijiji chake na kuhamia kwenye kijiji kingine, ambacho wakazi wake walipata chakula, kwa sababu naye hukosa chakula kwa hulima mashamba na kuyaacha bila kuyapalilia palizi zake, maishani mwake. Ndiyo maana watu huongea juu yake kwamba “kwani palizi hujipalilia anakoenda!

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao, maishani mwao.

Methali 27: 11-15.

Mhubiri 10:18.

ENGLISH: DOES IT MEAN THAT WEEDS ARE WED BY THEMSELVES WHERE HE IS GOING!

There was a person who was moving to a village where they had good food in that year. This man lacked food in his village in that year. Then he moved to another village where he heard that his people got a lot of food crops. He was lacking food in his family because of not taking good care of his cultivated fields. He did not finish weeding them. That is why people said about him that, “does it mean that weeds are wed by themselves where he is going!”

This saying is compared to a person who is lazy in doing his own works, in his life. That person, cultivates food fields and leaves without weeding them because of his laziness. He was struggling with problems and hunger in his family, because of his laziness, of not being able to weed all the weeds in his fields.

This person resembles the one who lacked food in his village and moved to another village where its inhabitants got food, because he also lacks food because he cultivates the fields and leaves them without weeding his weeds, in his life. That is why people talk about him that “does it mean that weeds are wed by themselves where he is going!”

This saying imparts in people an idea about forcing themselves to do their works with great effort, so that they can get a lot of success, in their families.

Proverbs 27: 11-15.

Ecclesiastes 10:18.

hope-3467922__480

1227. PANDULAGA MIHAYO.

Oliyohi munhu uyo uyombaga mihayo yakwe bho lilaka lidoni umumahoya gakwe. Umunhu ng’wunuyo, wikalaga muchalo ja bhanhu bhingi abho bhadumaga uguigwa chiza imihayo yakwe yiniyo kunguno ya guiyomba bho lilaka lidoni, umumahoya gakwe genayo. Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagang’wila giki, “pandulaga mihayo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayombaga mihayo bho guyigondya, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, adaiyigololaga chiza umihayo ya mumahoya gakwe genayo, kunguno ya gubhisa ginhu ijo agikalaga adahayile igiki abhiye bhajimane, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agadumaga ugubhalela chiza abhanhu bha aha kaya yake kunguno ya guduma guigolola chiza imihayo ya mumahoya yakwe genayo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oyombaga mihayo yakwe bho lilaka lidoni, kunguno nuweyi agayomba mihayo yakwe bho nduhu uguigolola chiza, umumahoya gakwe genayo, aha kaya yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “pandulaga mihayo.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higlya ya guyomba bhunhana bho guigolola chiza imihayo ya mumahoya yabho, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mathayo 10:16.

Luka 12:2-3.

KISWAHILI: PASUA MANENO.

Alikuwepo mtu aliyekuwa akiongea maneno yake kwa sauti ndogo katika maongezi yake. Mtu huyo, aliishi kwenye kijiji cha watu wengi, ambao walishindwa kuyasikia vizuri maneno yake kwa sababu ya kuyaongea kwa kutumia sauti ndogo. Ndiyo maana watu hao walimwambia kwamba, “pasua maneno.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huongea maneno yake kwa kuyapindisha, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hayanyoshi vizuri maneno yake hayo, kwa sababu ya kuficha kitu fulani ambacho huwa hataki watu wengine wakielewe, maishani mwake. Yeye hushindwa kuiendeleza vizuri familia yake kwa sababu ya yeye kushindwa kuyanyoosha vizuri maneno yake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyesema maneno yakwe kwa sauti ndogo mpaka wenzake wakashindwa kuyasikia, kwa sababu naye huongea maneno bila kuyanyosha vizuri mpaka watu wanashindwa kuyaelewa vizuri, katika maongezi yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “pasua maneno.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kusema ukweli kwa kuyanyosha vizuri maneno yao, katika maongezi yao, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Mathayo 10:16.

Luka 12:2-3.

ENGLISH: BREAK THE WORDS.

There was a man who was speaking words in a low voice in his speech. Such person lived in a village of many people who failed to hear his words properly because he spoke them in a low voice. That is why those people told him that, “break the words.”

This saying is likened to a person who speaks his words by twisting them, in his life. Such person does not speak correctly his words, because he hides something that he does not want other people to understand, in his life. He fails to develop his family properly because of failing to properly stretch his words, in his life.

This person is similar to the one who said his words in a low voice until his colleagues could not hear them, because he also speaks words without stretching them properly until people are unable to understand them properly, in his speech. That is why people tell him that, “break the words.”

This saying teaches people about telling the truth by stretching their words properly, in their speech, so that they can raise their families well, in their lives.

Matthew 10:16.

Luke 12:2-3.

old-3391298_1280

1225. DAGELALA GUBHONA KALYETO DUHU.

Bhalihoyi bhanhu abho bhalibhaja gujunlola ngeni uyo obhitilaga umuchalo jabho. Abhanhu bhenabho bhagaduma ugumona na gundebha chiza ungeni ng’wunuyo, kunguno agabhita wangu wangu aho bhasangwa bhiyebhaga. Hunagwene bhagayomba giki, “dagelela gubhona kalyeto duhu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagiyebhaga ugutumama imilimo yabho, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagajaga ugujutumama imilimo yabho bhagalendela yingi duhu iyo idina solobho kunguno ya wiyebhu bhobho bhunubho, umubhutumami bho milimo yabho. Abhoyi bhagakelaga bhuli ng’waka umukaya jabho kunguno ya gwiyebha kutumama milimo yabho yiniyo, bho gulendela yingi iyo idina solobho yoseyose, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nabho bhagaja gujunola ngeni bhugiyebha mpaga ubhita bhadamonile chiza, kunguno nabhoyi bhagajaga ugutumama imilimo yabho bhagiyibha bho gulendela iyo idina solobho yoseyose umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagayombaga giki, “dagelega kubhona kalyeto duhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka gwiyebha gutumama milimo yabho bho gwigulambija guitumama na bhukamu bhutale, kugiki bhadule kupandima matwajo mingi, umukaya jabho.

Habakuki 1:11.

Luka 19:1-3.

KISWAHILI: TUMEKOMEA KUONA NUSU TU.

Walikuwepo watu walioenda kumuona mgeni aliyekuwa akipita katika kijiji chao. Watu hao, hawakuweza kumuona na kumfahamu vizuri mgeni huyo kwa sababu yeye alipita haraka wakati wao wakiwa wamejisahamu. Ndiyo maana walisema kwamba, “tumekomea kuona nusu tu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa watu wale ambao hujisahau kufanya kazi zao, katika maisha yao. Watu hao, huenda kufanya kazi zao na kupoteza muda wao kwa kujali vitu visivyo na faida yoyote kwao, kwa sababu ya kujisahamu kwao huko, katika utekelezaji wa majukumu yao. Wao hukosa chakula kila mwaka kwenye mashamba yao, kwa sababu ya kujisahamu kwao huko kufanya kazi zao, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na wale walioenda kumuona mgeni wakajisahau na kukomea kumuona nusu, kwa sababu nao pia huenda kufanya kazi zao na kupoteza muda wao kwa kujali vitu visivyo na faida yoyote, maishani mwao. Ndiyo maana wao husema kwamba, “tumekomea kuona nusu tu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha kujisahau katika kuyatekeleza majukumu yao kwa kujibidisha kuzifanya kazi hizo kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao.

Habakuki 1:11.

Luka 19:1-3.

ENGLISH: WE HAVE ONLY SEEN HALF.

There were people who went to see a stranger who was passing through their village. Those people could not see and get to know the stranger well because he passed quickly while they were busy. That is why they said that, “we have only seen half.”

This saying is compared to people who forget to do their works, in their lives. Those people go to do their works by wasting their time caring about things that are of no benefit to them, because of their self-indulgence in the implementation of their duties. They lack food every year in their fields, because of their indulgence in doing their works, in their lives.

Those people are like those who went to see a stranger and forgot themselves by wasting their time in useless things until they ended up seeing him only half way, because they also go to do their works and waste their time worrying about things that have no benefit in their lives. That is why they say that, “we have only seen half.”

This saying imparts in people an idea of stopping from wasting their time in useless things themselves enough to carry out their responsibilities by forcing themselves to do those tasks with great effort, so that they can get a lot of success, in their families.

Habakkuk 1:11.

Luke 19:1-3.

africa-5274086_1280