sayings

1331. OB’UKAGA HASI.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile b’ub’uki bho ng’wa munhu uyo winga kuwelelo. Umunhu ng’wunuyo agabhukila muli munhu uyo aginikwa lina lyakwe aho obyalwa kunguno ya gufunya likujo ukuliweyi na gulanhana ludugu. Hunagwene ulu munhu winikwa lina lya njimiji, abhanhu bhagayombaga giki, unjimiji ng’wunuyo, “ob’ukaga hasi.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo akikalaga na nhungwa jawiza kugiki adule gubhupandika ubhupanga ubho bhudashilaga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhalangaga nhungwa jawiza abhiye bho gutumama milimo chiza na gubhambilija abhanhu abho bhali na makoye, kunguno ya bhutogwa bhokwe ukubhiye bhenabho. Uweyi agadulaga ugubhalela bho gubhalanga nzila ja kubhupandika ubhupanga ubho bhudashilaga abhanhu bha ha kaya yakwe kunguno ya nhungwa jakwe ijawiza jinijo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agabhitila ya wiza abhiye mpaga ilina lyakwe winikwa ung’wana uyo agabyalwa, kunguno nuweyi agabhalangaga abhiye nhungwa ja gubhambilija ugubhupandika ubhupanga ubho bhudashilaga, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanbu bhagang’wizukaga ulu bhabhubhona uwiza bho lilande lyakwe bho guyomba giki, “ob’ukaga hasi.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na nhungwa jawiza bho gwikala na bhichabho chiza, kugiki bhadule gubhupandika ubhupanga ubho bhudashilaga, ulu bhinga ukuwelelo.

1Wakorintho 15:53-58.

1 Wathesalonike 4:13-17.

KISWAHILI: AMEINUKA CHINI.

Chanzo cha msemo huo, huongelea uinukaji wa mtu yule aliyefariki dunia. Mtu huyo aliinuka kupitia mtu aliyepewa jina lakwe baada ya kuzaliwa kwa sababu ya kuonesha heshima kwake na kutunza undugu. Ndiyo maana mtu anapopewa jila na marehemu watu husema kwamba, yule marehemu, “ameinuka chini.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyaishi malezi mema yawezayo kumpatia uzima wa milele, baada ya kuaga dunia. Mtu huyo, huwafundisha wenzake tabia njema ya kuishi malezi mema kwa kujibidisha kufanya kazi na kuwasaidia watu walioko kwenye matatizo mbalimbali, kwa sababu ya upendo alionao kwa watu wake hao. Yeye hufanikiwa kuwapatia malezi hayo mema watu wa kwenye familia yake, kwa kuwafundisha njia za kuupata uzima huo wa milele, kwa sababu ya tabia yake hiyo njema, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewatendea mema wenzake mpaga jila lake akapewa mtoto aliyezaliwa, kwa sababu naye huwafundisha wenzake malezi mema ya kuwasaidia kuupata uzima wa milele, maishani mwake. Ndiyo maana watu hao humkumkuka wanapoyaona mema yake hayo, kwa kusema kwamba, “ameinuka chini.”

Msemo huo huwafundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuwafundisha wenzao namna ya kuyaishi malezi mema, ili waweze kuupata uzima wa milele baada ya kuaga dunia.

1Wakorintho 15:53-58.

1 Wathesalonike 4:13-17.

ENGLISH: THE ONE HAS RISEN DOWN.

The origin of this saying refers to the rise of a person who has passed away. Such person rose through the person who was given his name after birth because of showing respect for him in taking care of the family. That is why when a person is given a name of a deceased one, people say that, “the one has risen down.”

This saying is matched to a person who lives a worthy upbringing that can give him eternal life after passing away. This person teaches his people decent conducts of living a upright upbringing by working hard and helping others who are in various hitches, because of having a true love for his populaces. He succeeds in giving decent nurture to the people in his family by teaching them about ways which can help them enough to gain such eternal life because of his upright character in his life.

This person resembles the one who did good deeds to his societal members who gave his name to a newborn child, because he also teaches his family members about virtuous upbringings which can assist them in gaining eternal life. That is why those people praise him when they see his decent deeds by saying that “the one has risen down.”

This saying instills in individuals a clue of having a decent attitude for teaching their family members on how to live a blameless upbringing, so that they can gain eternal life after passing away.

1 Corinthians 15:53-58.

1 Thessalonians 4:13-17.

 

1330. JISUJI JA NJINGO.

Ijisuji ja njingo jilisuji ja ng’wa munhu uyo agajaga ogalilila kunjingo. Umunhu ng’wunuyo, agajaga ukunjingo ogalila mpaga omala na oshoka ukubhiye kunguno ya gubhabhisa abhiye bhakije ugumana igiki agalilaga.

Aliyo lulu, abhanhu bhenabho nose bhagamana igiki agajaga ogalilila kunjingo kunguno amiso gakwe galalukaga ulu omala ugulila ukunjingo gunuko. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’witana giki, “jisuji ja njingo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina sada ya kupanza iyo agayibhisaga ukubhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agakoyiyaga ni sada yiniyo mpaga okonda kunguno ya guyibhisa ukubhiye na kukija guichala kusitali kujulagulwa wangu, umuwikaji bhokwe. Uweyi agakoyiyagwa ni sada yiniyo mpaga gobhipa umili gokwe kunguno ya gugaiwa witegeleja bho gwanguha gujulagulwa kusitali, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agabhisa jisuji bho gulilila kunjingo kunguno nuweyi agayibhisaga isada yakwe mpaga okonda, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “jisuji ja njingo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho kuleka kubhisa makoye gabho kugiki bhadule gwambilijiwa wangu, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mathayo 11:28-30.

Luka 4:40.

Yakobo 5:15-16.

KISWAHILI: MACHOZI YA UWIGONI.

Machozi ya uwigoni ni machozi ya mtu ambaye huenda hulilia kwenye uwigo wa nyumba. Mtu huyo, huenda kwenye uwigo huo ambako hulia mpaka anamaliza ndipo anaenda kwa wenzake kwa sababu ya kujificha kwa wenzake hao ili wasifahamu kuwa huwa analia.

Lakini basi, watu hao walifahamu mwishowe kuwa yeye huwa anaenda kulia uwigoni kwa sababu ya macho yake kuwa mekundu anapomaliza kulia kule uwigoni. Ndiyo maana watu hao walimuita jila la “machozi ya uwigoni.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana ugonjwa wa kuharisha ambao huufika kwa wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huharisha mpaga anakonda kwa sababu ya kuufisha ugonjwa wake huo kwa wenzake ambao wangeweza kumpeleka hospitalini kutibiwa mapema, maishani mwake. Yeye husumbuliwa na ugonjwa huo mpaga anaishiwa nguvu mwilini mwake, kwa sababu ya kukosa umakini wa kuwahi kwenda kutibiwa hospitalini, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeficha machozi yake kwa kwenda kulilia uwigoni, kwa sababu naye huuficha ugonjwa wake mpaga anaishiwa nguvu, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita jina la “machozi ya uwigoni.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuacha kuficha matatizo yao, ili waweze kusaidiwa kuyatatua mapema, maishani mwao.

Mathayo 11:28-30.

Luka 4:40.

Yakobo 5:15-16.

 

ENGLISH: TEARS OF THE KITCHEN GARDEN.

Tears of kitchen garden are tears of a person who cries in the garden of the house. This person goes to the garden where he cries until he finishes doing so and then goes to his friends because of hiding from his friends so that they do not know that he is crying.

But then, those people finally realized that he always goes to the garden to cry because his eyes become red when he finishes crying in the garden. That is why those people called him “tears of the kitchen garden.”

This saying is paralleled to a man who has diarrhea disease which he hides from his friends in his life. This person suffers diarrhea sickness until he becomes thin because of hiding his illness to his friends who could have taken him to the hospital for treatment earlier, in his life. He is troubled by the disease to the point of losing strength in his body, because of lack of responsiveness of going to the hospital for treatment in his life.

This person is like the one who hid his tears by going to the kitchen garden because he also hides his illness until he is exhausted in his life. That is why people call him “tears of the kitchen garden.”

This saying teaches people to be cautious enough to stop hiding their problems, so that they can be helped by others enough to solve them early in their lives.

Matthew 11:28-30.

Luke 4:40.

James 5:15-16.

 

man-1465525_1280

1326. IZUGA LYA MANYANYA NULU HALIMI DUHU JUPYA.

Imbuki ya kahayile kenako ilolile bhuzugi bho manyanya. A manyanya genayo gadi nizuga lidamu kunguno unzugi ogo adulile nulu gugachembagula duhu ugaleka mulimi gupya. Umunhu ng’wunuyo, agagutumamaga unimo gunuyo bho nduhu nulu gunoga. Hunagwene agayombaga giki “izuga lya manyanya nulu halimi duhu jupya.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile gutumama milimo yakwe chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga na milimo mingi iyo aidebhile uguitumama mpaga oyimala chiza kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi noyi aha kaya yakwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho gudebha guitumama mingi chiza chiniko, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo oliadebhile guzuga nyanya chiza, kunguno nuweyi adebhile gutumama milimo yakwe chiza chiniko, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “izuga lya manyanya nulu halimi duhu jupya.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gudebha kutumama milimo yabho chiza chiniko, kugiki bhadule gupandika matwajo  mingi, umuwikaji bhobho.

Ezra 5:8.

KISWAHILI: UPISHI WA NYANYA HATA JUANI TU ZINAIVA.

Chanzo cha msemo huo huangalia upishi wa nyanya. Nyanya hizo hazina mapishi magumu kwa sababu mpikaji wake aweza hata kuzikatakata tu akaziacha juani zikaiva. Mtu huyo huifanya kazi hiyo bila hata ya kumchosha. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “upishi wa nyanya hata juani tu zinaiva.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anaelewa kufanya kazi zake vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo hufanya kazi nyingi anazizoelewa kuzitekeleza mpaga anazimaliza vizuri, kwa sababu ya  umakini wake huo, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi sana kwenye familia yake kwa sababu ya umakini wake huo wa kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi zake hizo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeelewa kupika nyanya vizuri, kwa sababu naye anaelewa kuzitekeleza kazi zake vizuri, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “upishi wa nyanya hata juani tu zinaiva.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi zao zote, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Ezra 5:8.

 

ENGLISH: COOKING TOMATOES EVEN IN THE SUN WILL RIPEN.

The origin of this saying looks at cooking tomatoes. These tomatoes do not have difficult recipes because their cook can even just chop them and leave them in the sun to ripen. This person does this work without even being tired. That is why he says, “Cooking tomatoes even in the sun will ripen.”

This saying is matched to a man who understands how to do his work well, in his life. Such person does several tasks that he understands how to do, and he finishes them well, because of his responsiveness, in his life. He earns a lot of wealth in his family because of his thoughtfulness of understanding and carrying out his tasks well, in his life.

This person resembles the one who understood how to cook tomatoes well, because he also understands how to carry out his tasks well, in his life. That is why he says, “Cooking tomatoes even in the sun will ripen.”

This saying teaches people to be careful enough to understand and carry out all their tasks well, so that they can achieve great success in their lives.

Ezra 5:8.

 

 

woman-5935805__480

1325. UMUNHU UYO ADIMANILE ING’HANA UDIZUNG’WILA ING’HANA.

Akahayile kenako kandija kuli munhu uyo oyombaga mihayo ya bhulomolomo umukikalile kakwe. Abhanhu abho wikalaga nabho umunhu ng’wunuyo, bhang’wilaga giki  aileke imihayo yiniyo iyabhulongo bho guyomba bhunhana, olema kunguno ya bhuhalali bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “umunhu uyo adimanile ing’hana udizung’wila ing’hana.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitaga mihayo ya bhubhi umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alinsembo uyo adigwaga  mihayo ya guwilwa na bhiye kunguno ya nhungwa jakwe ija bhuhalali jinijo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguilela chiza ikaya yakwe kunguno ya bhusembo bhokwe ubho gwita mihayo ya bhubhi bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo owilagwa giki aleke guyomba mihayo ya bhulomolomo olema, kunguno nuweyi agawilagwa na bhiye giki, aleke gwita mihayo ya bhubhi, olema, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu abho agabhahalalikaga bhagiwilaga giki, “umunhu uyo adimanile ing’hana udizung’wila ing’hana.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka nhungwa ja gwita mihayo ya bhubhi bho gwita mihayo ya wiza kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

2Wakonritho 7:14.

Yohane 14:17.

KISWAHILI: MTU ASIYEUJUA UKWELI USIMWAMBIE UKWELI.

Msemo huo, ulianzia kwa mtu yule aliyekuwa alisema maneno ya uongo katika maisha yake. Watu waliokuwa wakiishi naye, walimwambia kwamba aache kusema uongo kwa kusema ukweli, akakataa kwa sababu ya ubishi wake huo. Ndiyo maana watu hao, walisema kwamba, “mtu asiyeujua ukweli usimwambie ukweli.”                                 

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutenda maovu katika maisha yake. Mtu huyo hutenda maovu kwa wenzake na kukataa kuyaacha pale wenzake hao wanapomshauri kuayaacha, kwa sababu ya tabia yake hiyo mbaya ya ubishi, maishani mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake hiyo kwa sagabu ya kutenda maovu hayo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekataa kuacha kusema uongo aliposhauriwa na wenzake, kwa sababu naye hukataa kuacha kutenda maovu anaposhauriwa na wenzake, maishani mwake. Ndiyo maana wenzake hao, huambiana kwamba, “mtu asiyeujua ukweli usimwambie ukweli.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kutenda maovu kwa kufuata ushauri wa kutenda mema kwa wenzao, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

2Wakonritho 7:14.

Yohane 14:17.

ENGLISH: DO NOT TELL THE TRUTH TO A PERSON WHO DOES NOT KNOW IT.

This saying is originated from a person who had told lies in his life. The people who lived with him told him to stop lying by telling the truth, but he refused because of his argumentativeness. That is why those people said, “Do not tell the truth to a person who does not know it.”

This saying is equated to a person who commits evil deeds in his life. Such person commits evil deeds against his nobles and refuses to stop when those nobles advise him to stop, because of his wicked argumentative behavior in his life. He fails to nurture his family well because of committing those evil deeds in his life.

This person is similar to the one who refused to stop lying when advised by his fellows, because he also refuses to stop committing evil deeds when advised by his fellows in his life. That is why those fellows say to each other, “Do not tell the truth to a person who does not know it.”

This saying imparts in people an idea of stopping habits of doing evil deeds by following advice of doing good deeds to their fellows, so that they can nurture their families well, in their lives.

2 Corinthians 7:14.

John 14:17.

1323. HUJU YA B’UKI.

Ihuju ya b’uki jili nzuki ijo jili na b’uki wingi gete. Abhanhu bhagawapaga ub’uki bhunubho bhuli makanza bho nduhu ugubhumala kunguno ya wingi bhobho bhunubho. Hunagwene abhabhu bhenabho bhagawikolanijaga na huju ilo lililitabha lya minzi mingi bho guwitana giki, “huju ya b’uki.”

Akahayile kenako kagalengajiyagwa kuli munhu uyo alinsabhi o majikolo mingi aha kaya yakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga na sabho ningi noyi ijo agatumamilaga bho gubhagunana abhiye abho bhali na makoye kunguno ya wizanholo bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga na bhanhu bhingi noyi aha kaya yakwe abho agabhambilija kunguno ya wizang’oholo ubho ugubhutumamila chiza ubhusabhi bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nzuki iyo yali na b’uki wingi noyi, kunguno nuweyi alinsabhi o masabho mingi ayo agagatumamilaga bho gubhagunana abhiye abhali na makoye, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “huju ya b’uki.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizanholo bho gubhagunana abhichabho abho bhali na makoye, kugiki bhadule kupandika mbango ya gwikala bho bhuyegi umukaya jabho.

Mathayo 7:7-8.

Mathayo 8:21-30.

Mwanzo 13:2.

Yakobo 2:5.

KISWAHILI: BWAWA LA ASALI.

Bwawa la asali ni nyuki wenye asali nyingi sana. Watu huilina asali hiyo kila wakati bila ya kuimaliza kwa sababu ya wingi wake huo. Ndiyo maana wao huufananisha na bwawa la hilo ambalo ni dimbwi lenye kina kirefu cha maji kwa kuiita, “bwawa la asali.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni tajiri wa mali nyingi kwenye familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, ana utajiri wa mali nyingi sana ambazo huzitumia kwa kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali, kwa sababu ya ukarimu wake huo, maishani mwake. Yeye huishi na watu wengi kwenye familia yake anaowasaidia kwa sababu ya ukarimu wake huo wa kuutumia utajiri wake kwa kuwasaidia watu wenye matatizo maishani mwao.

Mtu huyo, hufanana na wale nzuki waliokuwa na asali nyingi, kwa sababu naye na utajiri wa mali nyingi ambazo huzitumia kwa kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita jila la “bwana la asali.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na moyo wa ukarimu uwawezeshao kuwasaidia wenzao wanaokumbwa na matatizo mbalimbali, ili waweze kupata Baraka za kuishi kwa furaha, katika familia zao.

Mathayo 7:7-8.

Mathayo 8:21-30.

Mwanzo 13:2.

Yakobo 2:5.

 

ENGLISH: HONEY POND.

A honey pond is a bee with a lot of honey. People eat the honey all the time without finishing it because of its abundance. That is why they compare it to a pond, which is a deep pool of water by calling it, “honey pond.”

This saying is paralleled to a person who is rich in countless belongings in his family. This person, has a lot of wealth which he uses for assisting people who face various glitches, because of his generosity in life. He lives with numerous people in his family whom he helps because of his generosity in using his wealth to help people who face problems in their lives.

This person is similar to the bees which had a lot of honey, because he also has a lot of wealth that he uses for helping people who face various problems in life. That is why people call him “honey pond.”

This saying teaches people about having a generous heart that enables them to help their people who are experiencing various problems, so that they can receive God blessings of living happily in their families.

Matthew 7:7-8.

 

honey-4770245_1280

honey-1958464_1280

honey-1970626_1280