sayings

1416. IGEMBE NAGEMA NG’WELELE.

Aho kale olihoyi nhimi uyo olimilaga ligembe lya makono. Unhimi ng’wunuyo olialisanije iligembe lyakwe linilo kunguno olilimilaga chiza mpaga lyang’wenhela jiliwa aha kaya yakwe. Uweyi olidimilaga china iligembe linilo guti numo agabhukikaja ng’wana ng’welele, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayomba giki, “igembe nagema ng’welele.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina bhutungilija bho gwihanda gutumama chiza nimo uyo gugang’wenhelaga jiliwa, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agihandaga gugudumama unimo gokwe bho gubhalanga abhanhu bhakwe higulya ya gwigulambija kugugutumama chiza mpaga gobhapandikila jiliwa, kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga jiliwa ja gulya chiza bhuli ng’waka aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho ubho gwigulambija gugutumama chiza unimo gokwe gunuyo, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu nhimi uyo olilimilaga chiza iligembe lyakwe mpaga lya ng’wenhela jiliwa aha kaya yakwe, kunguno nuweyi agagudimilaga chiza unimo gokwe gunuyo bho gwigulambija gugutumama chiza mpaga opandika jiliwa ja gulya chiza aha kaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “igembe nagema ng’welele.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho gwigulambija guyitumama chiza imilimo yabho iyo igabhenhelaga jiliwa, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila chiza umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mwanzo 3:19.

Mithali 24:27.

KISWAHILI: JEMBE NIMEJARIBU MTOTO MCHANGA

Hapo zamani alikuwepo mkulima aliyelimia jembe la mkono. Mkuliwa huyo alilitegemea jembe lake hilo kwa sababu ya kulilimia vizuri mpaka linamletea chakula kwenye familia yake. Yeye alilishikilia vizuri jembe hilo kama anavyobeba mtoto mchanga, maishani mwake. Ndiyo maana alisema kwamba, “jembe nimejaribu mtoto mchanga.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujikaza kuifanya vizuri kazi ile ambayo humletea chakula, katika maisha yake. Mtu huyo, huishikilia kazi yake hiyo kwa kuwafundisha watu juu ya kujibidisha kuitekeleza vizuri mpaka inawapatia chakula, kwa sababu ya uaminifu wake huo, maishani mwake. Yeye hupata chakula cha kula vizuri kila mwaka kwenye familia yake kwa sababu ya uaminifu wake huo wa kujibidisha kuitekeleza vizuri kazi yake hiyo, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo hufanana na yule mkulima aliyelilimia vizuri jembe lake mpaka likamletea chakula kwenye familia yake, kwa sababu naye hujibidisha kuitekeleza vizuri kazi yake hiyo mpaka inamletea chakula cha kula kila mwaka kwenye familia yake, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “jembe nimejaribu mtoto mchanga.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kujibidisha kuzitekeleza vizuri kazi zao zinazowaletea chakula, ili waweze kupata mali za kutumia vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 3:19.

Mithali 24:27.

ENGLISH: A HOE HAS TESTED A BABY.

Once upon a time, there was a farmer who cultivated farms by using a hand hoe. This farmer relied on his hoe because it worked well until it brought food to his family. He held the hoe tightly like he was carrying a baby, in his life. That is why he said that, “a hoe has tested a baby.”

This saying is equaled to a person who strives to do well the work that brings him food, in his life. Such person holds on to his work by teaching people about working hard enough to do it well until it provides them with food, because of his loyalty, in his life. He gets good food to eat every year for his family because of his loyalty to work hard enough to finish well his work in his life.

This person resembles the farmer who cultivated his farm until it brought food to his family, because he also strives to carry out his work well until it brings food to his family every year, in his life. That is why he says that, “a hoe has tested a baby.”

This proverb teaches people about being honest enough to carry out their work well that brings them food, so that they can obtain wealth for using well in their families, in their lives.

Genesis 3:19.

Proverbs 24:27.

1414. UGENIHA B’UGENI UGULONJIWA NDUHU.

Akahayile kenako kahoyelile jisumva ijo jigingilaga mukaya bho nduhu ugulongiwa na bhinikili kaya yiniyo.  Ijisumva jinijo jili guti jilungu mifa, danga, nole, nulu jigona ijijigingilaga umukaya ijo jidalongiyagwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ugeniha b’ugeni ugulonjiwa nduhu.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adabhadililaga abhageni ulu bhizaga aha kaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adabhadililaga abhageni abho bhagangenihaga bho nduhu agubhazugila ijiliwa aha kaya yakwe, kunguno ya wiminholo bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agagayiyagwa imbango ja gwikala na bhuyegi aha kaya yakwe, kunguno ya gukija ugubhalonja abhageni abho bhangenihaga, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo adajilonjaga ijisumva ijo jingilaga umukaya yakwe, kunguno nuweyi adabhalonjaga abhageni abho bhagangenihaga aha kaya yakwe, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhageni bhenabho bhagayombaga giki, “ugeniha b’ugeni ugulonjiwa nduhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizanholo bho gubhalonja abhageni abho abha bhagabhagenihaga, kugiki bhadule gupandika mbango ja gwikala na bhuyegi umukaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 25:35-41.

Matendo 10:28.

Warumi 12:13.

1Thimotheo 5:10.

KISWAHILI: UMEENDA UGENINI LAKINI HAWAKUJALI.

Msemo huo huongelea viumbe wanaoingia nyumbani bila mwenye nyumba kuwajali. Viumbe hayo ni kama vile kilungu yeye, chura, mijusi, na wengine ambayo ni jamii ya hao ambao huingia kwenye nyumba ya mtu bila ya yeye kuwajali. Ndiyo maana watu husema kwamba, “umeenda ugenini lakini hawakujali.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hawajali wageni wanaomtembelea kwenye familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hawajali bhageni ambao humtembelea kuwaacha bila kuwapikia chakula kwenye familia yake, kwa sababu ya uchoyo wake huo maishani mwake. Yeye hukosa baraka za kuishi kwa furaha kwenye familia yake hiyo kwa sababu ya uchoyo wake huo wa kutowajali wageni wanaomtembelea, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo hufanana na yule ambaye hakuwajali viumbe walioingia nyumbani kwake, kwa sababu naye hawajali wageni wanaomtembelea kwenye familia yake, maishani mwake. Ndiyo maana wageni hao husema kwamba, “umeenda ugenini lakini hawakujali.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwajali wageni wanaowatembelea nyumbani mwao, ili waweze kupata baraka za kuishi kwa furaha katika familia zao, maishani mwao.

Mathayo 25:35-41.

Matendo 10:28.

Warumi 12:13.

1Thimotheo 5:10.

 

ENGLISH: YOU HAVE BEEN A STRANGER BUT THEY DO NOT CARE YOU.

This saying refers to creatures which enter a house without the owner paying attention to them. These creatures are like deer, frogs, lizards, and others which are a type of those that enter a person’s house without him paying attention to them. That is why people say that, “you have been a stranger but they do not care you.”

This saying is equated to a person who does not care about guests who visit his family, in his life. Such person does not take care about visitors who visit him by leaving them without cooking food for them, because of his greed in his life. He misses blessings of living happily in his family because of his greed of not taking care about visitants who visit him in his life.

This person is like the one who did not care about the creatures that entered his house, because he also does not take care about guests who visit his family, in his life. That is why those guests say that, “you have been a stranger but they do not care you.”

This saying imparts in people an idea of being hospitable and considerate of strangers who visit their homes, so that they can experience blessings of living happily in their family lives.

Matthew 25:35-41.

Acts 10:28.

Romans 12:13.

1 Timothy 5:10.

 

 

1413. AGALYAGA JAGUKANDIWA.

Olihoyi munhu uyo olyaga jiliwa bho nduhu ugutumama imilimo. Umunhu ng’wunuyo oliadajaga gujutumama umilimo kunguno ya gwikalila ha kaya ahikanza ilya milimo yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “agalyaga jagukandiwa.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alingokolo o milimo umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga wigashije ahikanza lya gutumama imilimo mpaga lyashila ilikanza linilo kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agagayiyagwa ijiliwa aha kaya yakwe bhuli ng’waka kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho ubho gwikala wigashije ahikanza lya guitumama imilimo yiniyo, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo olyaga jiliwa bho nduhu ugutumama imilimo, kunguno nuweyi agikalaga wigashije bho nduhu gutumama imilimo mpaga lyashila ilikanza lya milimo yiniyo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “agalyaga jagukandiwa.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza bhakamu bha gutumama milimo yabho bho gwigulambija guitumama chiza, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila umukaya jabho.

Mwanzo 50:21.

Zaburi 81:16.

Mithali 11:21.

Ezekieli 34:23.

KISWAHILI: ANAKULA CHA MASIMANGO.

Alikuwepo mtu ambaye alikuwa akila chakula bila kufanya kazi. Mtu huyo, alikuwa haendi kufanya kazi kwa sababu alikuwa akikaa nyumbani wakati wa kufanya kazi. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “anakula cha masimango.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mvivu wa kazi katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia muda wake kwa kukaa nyumbani wakati wa kufanya kazi mpaka muda huo unapita, kwa sababu ya uvivu wake huo maishani mwake.  Yeye hukosa chakula kwenye familia yake kila mwaka kwa sababu ya uvivu wake huo wa kukaa nyumbani bila kufanya kazi, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekula chakula bila kufanya kazi, kwa sababu naye hushinda akiwa amekaa nyumbani bila kufanya kazi mpaka wakati huo wa kazi unapita, maishani mwake.  Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “anakula cha masimango.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kufanya kazi, kwa kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao vizuri, ili waweze kupata mali za kutumia katika familia zao.

Mwanzo 50:21.

Zaburi 81:16.

Mithali 11:21.

Ezekieli 34:23.

ENGLISH: HE EATS THE FOOD OF INSULTS.

There was a man who ate food without working. Such man did not go to work because he was staying at home during working hours. That is why people said to him that, “he eats the food of insults.”

This saying is equaled to a person who is lazy in his life. Such man spends his time by staying at home during working hours until that time passes, because of his laziness in his life. He lacks food for his family every year because of his laziness in staying at home without working in his life.

This man resembles the one who ate food without working, because he also wins while staying at home without working until such time of work passes, in his life. That is why people said to him that “he eats the food of insults.”

This saying imparts in people an idea being diligent in working, by working hard enough to fulfill their duties well, so that they can earn wealth for their families.

Genesis 50:21.

Psalm 81:16.

Proverbs 11:21.

Ezekiel 34:23.

1412. NG’WICHAGE UNG’WANA AGUGUB’UNA.

1412. NG’WICHAGE UNG’WANA AGUGUB’UNA.

Olihoyi munhu uyo wikalaga muchalo jilebhe. Umunhu ng’wunuyo oliobyalwa na jika ijo jaligungule ukungongo gokwe kunguno ya gubhumbwa chene. Uweyi obhizaga guti giki abhuchije ng’wana ukungongo gokwe gunuyo. Hunagwene abhanhu bhamelaga bho gung’wilaga giki, “ng’wichage ung’wana agugub’una.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina bhudoshi bho gubhaseka abhanhu abho bhalina jika, umukikalile kakwe. Munhu ng’wunuyo, agabhaluhyaga abhanhu abho bhalina jika jilebhe bho gubhaseka kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agagayiyagwa imbango ja gwikala na bhuyegi aha kaya yakwe, kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho ubho gubhaseka abhanhu abho bhalina jika, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’winuyo, agikolaga nabho bhansegaka uyo oliobyalwa na jika ukungongo, kunguno nuweyi agabhasekaga abhanhu abho bhali na jika, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agabhawilaga giki, “ng’wichage ung’wana agugub’una.”

Akahayile kenako kalanga bhahu higulya ya gubhiza na bhutengeke bho gwikala chiza na bhanhu abho bhalina jika, kugiki bhadule kupandika mbango ja gwikala na bhuyegi umukaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mathayo 9:27-30.

Luka 14:13-14.

2 Samweli 4:4.

KISWAHILI: MSHUSHE MTOTO ATAKUCHOSHA.

Alikuwepo mtu aliyeishi katika kijiji fulani. Mtu huyo, alizaliwa akiwa na kilema kilichoinuka mgongoni mwake kwa sababu ya kuumbwa hivyo. Yeye alionekana kama amebeba mtoto mgongoni mwake. Ndiyo maana watu walimtania kwa kumwambia kwamba, “mshushe mtoto atakuchosha.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu aliye na majivuno ya kuwacheka watu wenye vilema, katika maisha yake. Mtu huyo, huwatesa vilema kwa kuwacheka kwa sababu ya majivuno yakwe hayo, maishani mwake. Yeye hukosa baraka za kuishi kwa furaha katika familia yake hiyo, kwa sababu ya majivuno yake hayo ya kuwacheka vilema, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na wale waliomcheka yule aliyekuwa na kilema mgongoni mwake, kwa sababu naye huwacheka watu wenye vilema, maishani mwake. Ndiyo maana huwaambia kwamba, “mshushe mtoto atakuchosha.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuishi vizuri na watu walio na vilema, ili waweze kupata baraka za kuishi kwa furaha, katika familia zao, maishani mwao.

Mathayo 9:27-30.

Luka 14:13-14.

2 Samweli 4:4.

ENGLISH: PUT THE CHILD DOWN, YOU WILL BE BORED.

There was a man who lived in a certain village. Such man was born with a crippled back because of his birthmark. He looked like he was carrying a child on his back. That is why people joked about him by saying that, “Put the child down, you will be bored.”

This saying is compared to a person who is proud enough to laugh at people who have disabilities in his life. Such man tortures disabled ones by laughing at them because of his pride in his life. He misses blessings of living happily in his family because of his pride of laughing at the disabled ones in his life.

This man is like those who laughed at the man who had a crippled back because he also laughs at the disabled people in his life. That is why he says that, “Put the child down, you will be bored.”

This saying imparts in people an idea of having decent habits of nicely living with people who have disabilities, so that they can receive blessings of living happily, in their family lives.

Matthew 9:27-30.

Luke 14:13-14.

2 Samuel 4:4.

1410. WIGUSHA B’O B’ANIGINIGI LUB’UB’U LO MVAA.

Abhaniginigi bhagigushaga bho gutumya lub’ub’u guti mva jilisha. Abhanigini bhenabho bhagatumyaga lub’ub’u kunguno bhagigusijaga masalu nulu moto kunguno ya bhuniginigi bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “wigusha b’o b’aniginigi lub’ub’u lo mvaa.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagatumamaga nyanigini imilimo yabho umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagatumamaga hadoo duhu imilimo yabho bhandya gwigusha mpaga bhaduma uguimala imilimo uguitumama kunguno ya gudilila mahoya ahikanza lya milimo yao umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagagayiyagwa ijiliwa aha kaya jabho kunguno ya bhuniginigi bhobho ubho guduma uguitumama chiza imilimo yabho, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga na bhaniginigi abho bhagadililaga ligusha bho nduhu uguitumama imilimo yabho, kunguno nabhoyi bhagadililaga mahoya mpaga bhaduma uguitumama chiza imilimo yabho, umuwikaji bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “wigusha b’o b’aniginigi lub’ub’u lo mvaa.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gudilila milimo yabho bho gwigulambija guitumama chiza, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila umukaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mithali 20:11.

Mithali 23:13.

Yoeli 1:3.

Marko 9:37-37.

KISWAHILI: MCHEZO WA WATOTO VUMBI LA MBWA.

Watoto hucheza michezo yao kwa kutimua vumbi kama mchezo wa mbwa. Watoto hao hutimua vumbi kwa sababu huwa wanachezea mchanga au kitu kingine ukiwemo moto kwa sababu ya utoto wao huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mchezo wa watoto vumbi la mbwa.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale ambao hufanya kazi zao kitoto katika maisha yao. Watu hao hufanya kazi kidogo tu wanaanza kucheza mpaga wanashindwa kuzimaliza kazi zao, kwa sababu ya kujali maongezi yasiyo na faida wakati wa kufanya kazi, maishani mwao. Wao hukosa chakula katika familia zao kwa sababu ya utoto wao wa kushindwa kufanya kazi zao vizuri, maishani mwao.

Watu hao hufanana na watoto waliojali kucheza bila kufanya kazi, kwa sababu nao hujali maongezi wakati wa kazi mpaka wanashindwa kuzimaliza kazi zao, maishani mwao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “mchezo wa watoto vumbi la mbwa.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kujali kazi zao kwa kuzitekeleza kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mali za kutumia vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Mithali 20:11.

Mithali 23:13.

Yoeli 1:3.

Marko 9:37-37.

ENGLISH: CHILDREN’S GAME DOG DUST.

Children play their games by kicking up dust like a game of dogs. These children kick up dust because they always play with sand or something else including fire because of their childhood. That is why people say that, “children’s game dog dust.”

This proverb is paralleled to people who do their works like a child in their lives. These people only work a little, they start playing around and fail to finish their works, because they care about useless conversations while working, in their lives. They lack food in their families because of their childhood of failing to nicely do their works in their lives.

These people resemble the children who cared about playing without working, because they also care about conversations while working until they fail to finish their works, in their lives. That is why people say to them that, “children’s game dog dust.”

This proverb clarifies in people an idea of taking care of their works by carrying them out with great diligence, so that they can obtain wealth to nicely use in their family lives.

Proverbs 20:11.

Proverbs 23:13.

Joel 1:3.

Mark 9:37-37.