legacy

1461. MBUCHA MILIGO

Akahayile kenako kalolile nzobe iyo yabhuchaga miligo. Inzobe yiniyo, ili ndimu iyi abhanhu bhagaitumilaga bho gubhucha milimo yabho kunguno ya wivumilija bhoyo na nguzu jayo jiniyo. Iyoyi igabhambilija abhanhu bhenabho uguyibhucha imiligo yabho bhasiminza mpaga bhashiga uko bhajile umulugendo lobho lunulo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayitanaga giki “mbucha miligo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyumilija gubhambilija bhanhu gubhucha milimo yabho chiza, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, alina nguzu ningi na wiyumilija bhutale ubho gubhabhukija bhanhu miligo yao kunguno ya bhutogwa bhokwe bhunubho ukubhiye, umuwikaji bhokwe. Uweyi agayilalega chiza ikaya yakwe bhogubhalanga abhanhu bhakwe gutumama milimo yabho bho gwiyambilija chiza, kunguno ya wiyumilija na bhutungilija bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nzobe iyo yabhambilijaga bhanhu gubhucha milimo yabho chiza, kunguno nuweyi agabhambilija abhanhu bhakwe ukubhucha chiza imiligo yabho, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanga giki, “mbucha miligo.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gubhambilija bhichabho gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mwanzo 44:13.

Marko 11:1-4.

Mathayo 21:1-7.

Yohana 12:12-16.

KISWAHILI: MBEBA MIZIGO.

Msemo huo humuongelea punda. Punda huyo ni myama ambaye watu humtumia kuwabebea mizigo yao kwa sababu ya nguvu alizonazo na uvumilivu wake huo. Mwenyewe huwasaidia watu hao katika kubeba mizigo yao wanaposafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ndiyo maana watu humuita jina la “mbeba mizigo.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvumilia katika kuwasaidia watu kubeba mizigo yao vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, ana nguvu na uvumilifu wa kutosha kuwasaidia watu kutatua shida zao zikiwemo zile za kuwabebea mizigo yao, kwa sababu ya upendo na uvumilivu wake huo, maishani mwake. Yeye huilea vyema familia yake hiyo kwa kuwafundisha watu wake juu ya kuyatekeleza majukumu yao kwa kusaidiana vizuri, katika maisha yao.

Mtu huyo, hufanana na yule punda aliyewasaidia watu kubeba mizigo yao kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwa sababu naye huwasaidia watu wake kwa kuwabebea mizigo yao, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita jila la “mbeba mizigo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kutosha kusaidiana vizuri katika kuyatekeleza vyema majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 44:13.

Marko 11:1-4.

Mathayo 21:1-7.

Yohana 12:12-16.

1460. JILANGA BADUMA.

Akahayile kenako kanhoyelile munhu ndoo uyo aganhanga munhu uyo bhadalenijije imyaka nulu hado. Aho kale olihoyi namhala uyo ojidimaga ng’ombe jakwe. Umudimi bhokwe bhunubho, igabyala ng’ombe yakwe. Aho yabyala henaho uweyi akagabucha akadilanha, ing’ombe yukagayiwa akana kayo yushoka uko yabyalilaga. Huna wiza ng’wana okwe niyo ndoo ung’wila giki, “b’ab’a ukatuula hasi akana kayo yakabhona, obucha hangi ulu yahaya gunyamuka okatuula hasi hangi.” Oho wita giko unamhala ng’wunuyo ing’ombe yu golola guja kaya.

Unamhala ng’wunuyo agapelana noyi ugulangwa na ng’wana okwe mpaga usola lugoye uginija, kulwa gukolwa gulangwa na ng’wana wakwe chiniko. Hunagwene abhanhu bhagang’witana ung’wana ng’wunuyo giki “jilanga baduma.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina widohya bho gubhalanga bhanhu bhose lilange lya wiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agalitumilaga ilikanza lyakwe bho gubhalemala pye abhanhu bhakwe kajile kagwikala na bhichabho chiza kunguno ya widohya bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga na bhuyegi bhutale aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya widohya bhokwe ubho gubhalanga ilange lya wiza pye abhanhu bhenabho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ng’wana uyo agananga myaji okwe nzila ja uichala kaya ing’ombe yakwe iyo yaliyabyala yiniyo mpaga uishisha, kunguno nuweyi agabhalangaga lilange lyawiza abhanbhu bhakwe mpaga bhikala na buyeji bhutale aha kaya yabho yiniyo, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “jilanga baduma.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na widohya bho gubhalanga lilange lya wiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi bhutale umukaya jabho jinijo.

Luka 2:41-51.

Yohana 2:1-11.

KISWAHILI: MFUNDISHA WAKUBWA.

Msemo huo, humwongelea mtu mdogo aliyemfundisha mtu wasiyelingana naye miaka hata kidogo. Hapo zamani alikuwepo mzee aliyekuwa akichunga mifugo yake. Ng’ombe wake alizaa yeye akambeka yule ndama, yule ng’ombe akamkosa mtoto wake akarudi alikozalia. Ndipo mtoto wa mzee huyo, akamwambia “baba muweke chini ndama ili ng’ombe amuone, hafalafu unambeba tena, ng’ombe akirudi nyuma unamuweka mtoto wake huyo chini tena.” Mzee yule alipofanya hivyo, yule ng’ombe alimfuata mpaka nyumbani.

Mzee huyo alikasirika sana kufundishwa na mtoto wake mpaka akachukua kamba kwenda kujinyonga kwa sababu hasira yake hiyo ya kufundisha na mtoto wake. Ndiyo maana watu walimuita huyo mtoto jina la, “mfundisha wakubewa.”  

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana unyenyekevu wa kuwafundisha maadili mema watu wote, katika maisha yake. Mtu huyo huutumia muda wake kwa kuwafundisha watu wake wote mwenendo wa kuishi vizuri na wenzao kwa sababu ya unyenyekevu wake huo maishani mwake. Yeye huishi kwa furaha kubwa katika familia yake hiyo kwa sababu ya unyenyekevu wake huo wa kuwafundisha maadili mema watu wake wote, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule mtoto aliyemfundisha baba yake namna ya kumpeleka nyumbani ng’ombe aliyezaa, kwa sababu naye huwafundisha watu wake wote, namna ya kuishi vizuri na wenzao, mpaka wanaweza kuishi kwa furaha kubwa katika familia zao. Ndiyo maana watu hao humuita jina la “mfundisha wakubwa.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na unyenyekevu wa kuwafundisha watu wao maadili ya kuishi vizuri na wenzao, ili waweze kuishi kwa kuraha kubwa katika familia zao hizo, maishani mwao.

Luka 2:41-51.

Yohana 2:1-11.

1459. BULI OGALUKA LIFA GUNICHIMA?

Akahayile kenako kahoyelile bhuching’wa bho lifa bho munhu uyo oliadalimanile giki lifa ilinilo. Umunhu ng’wunuyo liganchima ilifa linilo aho obhitila hoyi kunguno oliganikilaga giki lidi lifa. Hunagwene aho lyanchima agabuja giki “buli ogaluka lifa gunichima.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agang’wigalukaga unwani okwe bho gung’witila mihayo ya bhubhi, umukikalile kabho. Umunhu ng’wunuyo aganndyaga gunsiga na gundalahija sagala ung’wiye mpaka nose, bhoya ugwikala kihamo kunguno ya gunminya chiniko ung’wiye, umuwikaji bhobho. Uweyi agabhubhinzaga ubhunwani bhobho bho gung’witila mihayo ya bhubhi chiniyo ung’wiye kunguno ya gung’wigaluka bho gunminya chiniko, umukikalile kabho kenako.

Umunhu ng’winuyo agikolaga ni lifa ilo liganchima uyo oliganikila giki lidi lifa, kunguno nuweyi agaminyaga ung’wiye bho gug’witila mihayo ya bhubhi mpaga obhubhinza ubhunwani bhobho bhunubho umuwikaji bhobho. Hunagwene ung’wiye agamujaga giki, “buli ogaluka lifa gunichima?”

Akahayile kenako kalanga bhanwani higulya ya guleka nhungwa ja gwiigaluka bho gwiitila mihayo ya bhubhi, kugiki bhadule gwikala bho mholele umubhunwani bhobho bhunubho.

Mathayo 26:14-16.

Mathayo 10:21.

Mathayo 24:9.

Marko 14:10-11.

KISWAHILI: KWA NINI UMEGEUKA MWIBA KUNICHOMA?

Msemo huo humuongelea mtu aliyechomwa mwiba ambao aliufikiria kuwa si mwiba. Mtu huyo, ulimchoma mwiba huo alipopitia hapo kwa sababu ya kuufikiria kuwa ni kitu kingine cha kawaida kisichoweza kumuumiza, katika mawazo yake. Ndiyo maana ulipomchoma aliuliza kwamba, “kwa nini umegeuka mwika kunichoma?”

Msemo huo hulinganishwa kwa rafiki anayemgeuka rafiki yake kwa kumtendea maovu, katika maisha yake. Mtu huyo, humsengenya rafiki yake huyo na kumdharau mpaga mwishowe urafiki wao unavunjika kwa sababu ya kumuumiza hivyo mwenzake, maishani mwao. Yeye huuvunja urafiki wao huo kwa sababu ya kumtendea maovu hayo yanayoumiza moyo wa mwenzake huyo, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na ule mwiba uliomchoma yule ambaye alifikiria kuwa siyo mwiba, kwa sababu naye humuumiza rafiki yake kwa kumtendea maovu mpaka urafiki wao unavunjika, maishani mwao. Ndiyo maana yule aliyeumizwa humuuliza mwenzake huyo kwamba, “kwa nini umegeuka mwiba kunichoma?”

Msemo huo, hufundisha marafiki juu ya kuacha tabia ya kugeukana kwa kutendeana maovu katika urafiki wao, ili waweze kuishi kwa amani, maishani mwao.

Mathayo 26:14-16.

Mathayo 10:21.

Mathayo 24:9.

Marko 14:10-11.

1458. KALAGU – KIZE. AB’O B’AB’ILINGAGWA BIZAGA PYE NA NG’HOME – BUSIGA BUHOLILE.

Ikalagu yiniyo ilolile busiga ulu giki buhola ung’wigulya bugab’izaga guti nang’ha gwa ng’home. Ubusiga bhunubho bugabhizaga na ng’home yiniyo ukwigwilya kunguno bhugajilanijaga ulu bhuhola mpaga bholenganila pye chiza. Ubhoyi bhudikilakilaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga bho guyomba giki “ab’ob’ab’ilingagwa bizaga pye na ng’home – busiga buholile.”

Ikalagu yiniyo, ikagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalina masala gagwiyambilija chiza ulu ng’wichabho obhabhilingaga kunimo gokwe, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagib’ilingaga gwiyambilija gutumama milimo yabho bhuli ng’wene obhuka na jitumamilo jakwe bhagatumama milimo yabho bho ng’wigwano gutale, kunguno ya masala gabho agawiza genayo, umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagapandikaga sabho ningi bhuli ng’wene aha kaya yakwe kunguno ya masala gabho genayo aga ng’wigano go gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza chiniko, umuwikaji bhobho bhunubho.

 Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nu busiga ubho bugalenganilaga chiza ulu bohola, kunguno nabhoyi bhalina ng’wigwano go gubhuka na jitumamilo jabho ulu bhab’ilingagwa gujiyambilija gutumama milimo yabho chiza, umuwikaji bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagabhayombaga giki, “ab’ob’ab’ilingagwa bizaga pye na ng’home – busiga buholile.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na masala ga ng’wigwano go gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

1Wakorintho 11:3.

Waefeso 1:22-23.

Waefeso 4:15.

Waefeso 5:23.

Wakolosai 1:18.

Wakolosai 2:10.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

WALIOALIKWA WAMEFIKA WOTE NA RUNGU – MASUKE YA MTAMA.

Kitendawili hicho, huangalia mtama uliotoa masuke yake. Mtama huyo, hutoa masuke ambayo huonekana kama fimbo yenye rundu kwa juu kwa sababu ya kuendana yote vizuri hivyo. Ndiyo maana watu huhadithiana kwa kusema kwamba, “walioalikwa wamefika wote na rungu – masuke ya mtama.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wenye akili za kusaidiana vizuri wanapoalikwa na mwenzao kwenda kumsaidia kufanya kazi yake, katika maisha yao. Watu hao hualikana pamoja kwenda kuyatekeleza majukumu yao kwa kusaidiana ambapo kila mmoja hubeba kitendea kazi kinachofaa kwa kazi hiyo, kwa sababu ya akili zao hizo zenye uelewano wa kusaidia vizuri katika kazi zao, maishani mwao. Wao hupata mali nyingi za kutumia kila mmoja kwenye familia yake kwa sababu ya ushirikiano wao huo mzuri, katika maisha yao.

Watu hao hufanana na ule mtama ambao hutoa masuke yanayoendana vizuri, kwa sababu nao husaidiana vizuri katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao kila wanapoalikwa na mwenzao, maishani mwao. Ndiyo maana watu huwaongelea kwamba, “walioalikwa wamefika wote na rungu – masuke ya mtama.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na akili za kuwawezesha kushirikiana vizuri, katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze kupata maendeleo mengi katika familia zao, maishani mwao.

1Wakorintho 11:3.

Waefeso 1:22-23.

Waefeso 4:15.

Waefeso 5:23.

Wakolosai 1:18.

Wakolosai 2:10.

1457. UISHIGE IMBULA ULUSHIGE NA LUME!

UMEIKIMBIA MVUA WAWEZA KUUKINKIMBIA NA UMANDE PIA!

USULI, MAANA NA MATUMIZI YA KILA SIKU

Methali hii ya Kisukuma inazungumzia ubatili wa kujaribu kuepuka hali zisizoepukika au zisizoepukika za maisha. Katika maisha ya Kisukuma, mvua (imbula) na umande (lume) ni vya kawaida na vya kawaida; vyote huleta unyevu, na vyote viwili haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu. Methali hii hutumia taswira hii kufundisha kwamba mtu hawezi kukimbia kila changamoto baadhi ya mambo maishani lazima yakabiliwe na kukubaliwa tu.

Katika mazungumzo ya kila siku, msemo huu hutumika kumkumbusha mtu anayeepuka majukumu, majukumu, au hali halisi zisizoepukika kwamba kukimbia hakutatui chochote. Inapinga hofu, kuahirisha mambo, na tabia ya kuepuka magumu.

Ujumbe ni rahisi: ukijaribu kuepuka tatizo moja (mvua), hivi karibuni utakutana na jingine (umande). Kwa hivyo, ujasiri na uvumilivu ni majibu bora kuliko kuepuka.

Biblia pia inafundisha kuhusu kukabiliana na changamoto kwa imani na uvumilivu badala ya kukimbia: Yona alijaribu kukimbia wito wa Mungu, kwa mfano, lakini alijifunza kwamba hakuna mtu anayeweza kukimbia kusudi la Mungu kama tunavyosoma katika Yona 1:1-3. Uwepo wa Mungu unafikia kila kona ya maisha, Zaburi 139:7-10, ina maelezo.

Tunapaswa kuuona kuwa ni furaha tupu tunapokabiliwa na majaribu, kwa sababu changamoto huzaa uvumilivu na ukomavu kama tunavyosoma katika Yakobo 1:2-4.

Ulinganifu wa Kibiblia

Yona 1:1-3: “1 Neno la BWANA likamjia Yona, mwana wa Amitai: Ondoka, uende kwa mji mkuu wa Ninawi, ukahubiri dhidi yake; kwa maana uovu wao umekuja mbele yangu. Lakini Yona alijiandaa kukimbilia Tarshishi, mbali na BWANA. Akashuka hadi Yafa, akakuta meli iendayo Tarshishi, akalipa nauli, akashuka ndani yake, aende nao Tarshishi, mbali na BWANA.”

Zaburi 139:7-10: “Niende wapi nijiepushe na roho yako? Nikimbie wapi kutoka mbele zako? Nikipanda mbinguni, uko huko; Nikilala kuzimu, uko huko. Nikichukua mabawa ya alfajiri na kukaa ng’ambo ya bahari, Hata mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika.”

Yakobo 1:2-4: “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mnapopatwa na majaribu mbalimbali; kwa maana mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta uvumilivu. Na uvumilivu uwe kamili, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.”

Mathayo 16:24: “Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote anayetaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.”

Matumizi ya Kisasa na Matumizi ya Kidini

Katika ulimwengu wa leo, methali hii inazungumza kwa nguvu kwa watu binafsi na jamii zinazojaribiwa kukata tamaa au kuepuka magumu. Inaweza kutumika katika kuhimiza uvumilivu wakati wa shida ya ugonjwa, ukosefu wa ajira kwa maisha ya kibinafsi, au mapambano ya kifamilia.

Inaweza pia kutumika katika kuwahimiza Wakristo kuendelea kujitolea kwa maombi, huduma, na uadilifu wa maadili hata wakati njia ni ngumu ya kutosha kutekeleza maisha ya imani katika hali za kila siku.

Pia inakumbusha Jumuiya Ndogo za Kikristo (SCC) na parokia au viongozi kutoacha miradi au majukumu kwa sababu ya vikwazo.

Methali hii kiroho inafundisha kukubali mapenzi ya Mungu kwa kutambua kwamba changamoto, kama mvua na umande, ni sehemu ya maisha au hali za binadamu. Kwa hivyo, kuziepuka huchelewesha ukuaji tu. Imani na ujasiri hubadilisha changamoto kuwa baraka.

Kwa hivyo, huwezi kuepuka kila changamoto jifunze kukabiliana na maisha kwa ujasiri, uvumilivu, na imani kwa Mungu. Hutupa hekima ya kukabiliana na hali halisi za maisha, ikiongozwa na imani inayotuongoza kwenye ukuaji na kusudi la kimungu kwetu.

YOU HAVE FLED FROM THE RAIN, CAN YOU FLEE FROM THE DEW TOO!

Background, Meaning and Everyday Use

This Sukuma proverb speaks about the futility of trying to escape life’s inevitable or unavoidable situations. In Sukuma life, rain (imbula) and dew (lume) are natural and common; both bring moisture, and both are beyond human control. The proverb uses this imagery to teach that one cannot run away from every challenge some things in life must simply be faced and accepted.

In daily conversation, this saying is used to remind someone who is avoiding responsibilities, duties, or inevitable realities that running away solves nothing. It challenges fear, procrastination, and the tendency to escape difficulties.

The message is simple: if you try to avoid one problem (the rain), you will soon meet another (the dew). Therefore, courage and endurance are better responses than avoidance.

 The Bible also teaches about facing challenges with faith and perseverance rather than running away: Jonah tried to flee from God’s call, for instance, but he learned that no one can run away from God’s purpose as what we read in Jonah 1:1-3. The presence of God reaches every corner of life, Psalm 139:7-10, has the detail.

We have to consider it pure joy whenever we face trials, because challenges produce perseverance and maturity as what we read in James 1:2-4.

 Biblical Parallels

Jonah 1:1-3: “1The word of the LORD came to Jonah, son of Amittai: Set out for the great city of Nineveh, and preach against it; for their wickedness has come before me. But Jonah made ready to flee to Tarshish, away from the LORD. He went down to Joppa, found a ship going to Tarshish, paid the fare, and went down in it to go with them to Tarshish, away from the LORD.”

Psalm 139:7-10: “Where can I go from your spirit? From your presence, where can I flee? If I ascend to the heavens, you are there; if I lie down in Sheol, there you are. If I take the wings of dawn and dwell beyond the sea, Even there your hand guides me, your right hand holds me fast.”

James 1:2-4: “Consider it all joy, my brothers, when you encounter various trials, for you know that the testing of your faith produces perseverance. And let perseverance be perfect, so that you may be perfect and complete, lacking in nothing.”

Matthew 16:24: “Then Jesus said to his disciples, “Whoever wishes to come after me must deny himself, take up his cross, and follow me.”

Contemporary Use and Religious Application

In today’s world, this proverb speaks powerfully to both individuals and communities tempted to give up or avoid hardship. It can be applied in encouraging perseverance in times of difficulty illness, unemployment to personal life, or family struggle.

It can also be applied in urging Christians to stay committed to prayer, service, and moral integrity even when the path is hard enough to put into practice the faith life in daily situations.

It also reminds Small Christian Communities (SCCs) and parishes or leaders not to abandon projects or responsibilities because of obstacles.                                                 

This Proverb spiritually teaches acceptance of the will of God by recognizing that challenges, like rain and dew, are part of the human lives or conditions. Hence, avoidance of them only delays growth.  Faith and courage transform challenges into blessings.

Therefore, you cannot escape every challenge learn to face life with courage, patience, and faith in God. It gives to us wisdom of facing life’s realities, guided by faith that leads to growth and divine purpose to us.

By

Sr. Tekla Wande.

+255753443609.