Sukuma Proverbs

1357. JALIWA NA BHANDELEBEYA.

Ulusumo lunulo luhoyelile bhandelebeya abho bhali bhanhu abho bhadina wikalo. Abhanhu bhenabho bhagasola mhiya ja ng’wa munhu uyo agabhalekela bho nduhu ugubhitila bhukengeji wiza kunguno ya gukija gwitegeleja gokwe chiza umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo aho bhajisola abhanhu bhelabho imhiya jakwe agandya guyubhachola bho guja agubhujaga kubhanhu ulu bhabhabhonaga. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’wila giki imhiya jakwe “jaliwa na bandelebeya.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhinhaga bhanhu sagala ijikolo jakwe bho nduhu ugubhitila bhukengeji ubho gung’wambilija gubhadebha chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agabhinhaga bhanhu sagala isabho jakwe abho bhajimilaga najo kunguno ya gugayiwa witegeleja bho gubhitila bhukengeji bho gubhadebha chiza haho atali ugubhalekela ijikolo jakwe jinijo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agajimijaga sabho ninyi noyi aha kaya yakwe kunguno ya kubhalekela bhanhu abho bhadina wikaji bho gumanyika chiza, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agasojiwa mhiya jakwe na bhanhu abhadina wikalo abho agabhalekela, kunguno nuweyi agabhinhaga bhanhu sagala isabho jakwe mpaga bhajimila najo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki isabho jakwe jinijo “jaliwa na bhandelebeya.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guleka kubhalekela bhanhu sagala isabho jabho, kugiki bhadule gujilanhana chiza isabho jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Walawi 19:13.

Zaburi 119:78.

Mithali 22:22.

Yeremia 22:17.

KISWAHILI: ZIMELIWA NA WATU WASIO NA MAKAO.

Methali hiyo huongelea watu wasio na makao ambao ni wale wanaoishi katika sehemu isiyojulikana vizuri. Watu hao walichukua pesa za mtu aliyewaachia bila ya kuwafanyia utafiti mzuri kwa sababu ya kukosa umakini wa kumsaidia kuwafahamu vizuri, maishani mwake.

Mtu huyo, alianza kuwatafuta watu wale waliozichukua pesa zake kwa kuwauliza watu kama wamewaona. Ndiyo maana wale watu walimwambia kwamba, pesa zake hizo “zimeliwa na watu wasio na makao.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwapatia watu hovyo mali zake bila ya kuwafanyia utafiti wa kumsaidia kuwafahamu vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, huwaachia watu hovyo mali zake hizo ambao hupotea nazo kwa sababu ya kukosa umakini wa kuwafanyia utafiti wa kuwafahamu vizuri, maishani mwake. Yeye huzipoteza hovyo mali za kwenye familia yake hiyo kwa sababu ya kuwaachia watu hao asiyowafahamu vizuri, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewaachia pesa zake watu wasio na makao ambao walipotea nazo, kwa sababu naye huwapatia watu hovyo mali zake mpaka wanapotea nazo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba mali zake hizo “zimeliwa na watu wasio na makao.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuacha kuwaachia mali zao watu wasio wafahamu vizuri, ili waweze kuzitunza vizuri mali zao hizo, maishani mwao.

Walawi 19:13.

Zaburi 119:78.

Mithali 22:22.

Yeremia 22:17.

 

ENGLISH: THEY HAVE BEEN EATEN BY HOMELESS PEOPLE.

This proverb refers to homeless individuals who live in an unknown place. These persons took money of a person who left it carelessly. He left such money without doing proper research because of a lack of responsiveness enough to aid him get to know what kind of people who were there at that time.

This person began to look for people who took his money by asking people if they had seen them. That is why the people told him about his money that “they have been eaten by homeless people.”

This proverb is related to a person who gives his wealth to individuals without doing any research that can support him enough to recognize them well in his life. This person gives his wealth to people without doing any research which can support him enough to know them well in his life. He loses his family’s wealth because of leaving it to people whom he does not know well in his life.

This person is like the one who left his money to the homeless ones who lost it, because he also gives his wealth to people carelessly until they lose it in his life. That is why people say to him about his wealth that, “they have been eaten by homeless people.”

This proverb imparts in people an idea of being so cautious enough to not leave their wealth to people whom they do not know well, so that they can take upright carefulness of their wealth in their lives.

Leviticus 19:13.

Psalm 119:78.

Proverbs 22:22.

Jeremiah 22:17.

 

money-1477064_1280

1347. B’ULUGU B’O KULA NAJE MUMAGOGEJA.

Aho kale alihoyi munhu uyo olinsab’i o mitugo. Imitugo jinijo jalikihamo na ngoko, mbuli, nholo na ng’ombe. Unsab’i ng’wunuyo, ojinjaga nkoko nulu mbuli ulu opandikaga ikoye idoo aha kaya yakwe kugiki adule kupandika hela ja gulimalila wantgu, kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho umukikalile kakwe.

Aliyo lulu, lushigu lumo agapandika likoye litale ilo lyalilya gumala bho gujinja ntugo ntale guti ng’ombe. Uweyi agiyangula gujinja ng’ombe kunguno ohayaga ab’ukinde wangu ub’ulugu bhunubho. Hunagwene agayomba giki, “b’ulugu b’o kula naje mumagogeja.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli nsab’i uyo agajitumamilaga chiza isabho jakwe umukikalile kakwe kenako. Unsab’i ng’wunuyo, agajilanhanaga chiza isabho jakwe kugiki jidule gung’wambilija ugugamala wangu amakoye ayo galampandike aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agajitumamilaga chiza isabho jakwe jinijo ulu opandikaga makoye aha kaya yakwe mpaga ogamala wangu kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako.

 Unsab’i ng’wunuyo, agikolaga nuyo agajinja ng’ombe aho opandika likole litale mpaga ulimala wangu ilikoye linilo, kunguno nuweyi agajitumamilaga isabho jakwe ulu upandikaga likoye mpaga olimala wangu umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “b’ulugu b’o kula naje mumagogeja.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujilanhana chiza isabho jabho kugiki ulu bhupandika makoye jidule gubhambilija ugugamala wangu amakoye genayo, umukaya jabho jinijo.

 Mathayo 6:19-34.

KISWAHILI: VITA IMEKUA KUBWA NIUZE NG’OMBE.

Hapo zamani alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa tajiri wa mifugo. Mifugo hao waliokuwa pamoja na kuku, mbuzi, kondoo, na ng’ombe. Tajiri huyo alikuwa akiuza kuku au mbuzi akipata shida ndogo katika familia yake ili apate hela ya kuyatatulia kwa sababu ya umakini wake huo, katika maisha yake.

Lakini basi, siku moja tajiri huyo alipata tatizo kubwa lililohitaji kuuza mfugo mkubwa kama ng’ombe ili kupata pesa za kulitatulia. Yeye aliamua kuunza ng’ombe kwa sababu ya kutaka aishinde haraka vita hiyo. Ndiyo maana alisema kwamba, “vita imekua kubwa niuze ng’ombe.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa tajiri yule ambaye huzitumia vizuri mali zake katika maisha yake. Tajiri huyo, huzitunza vizuri mali zake hizo ili ziweze kumsaidia kuyamaliza haraka matatizo yatakayojitokeza kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya umakini wake huo, maishani mwake. Yeye huzitumia vizuri mali zake hizo mpaka anayamaliza haraka matatizo yanayojitokeza kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya umakini wake huo, katika maisha yake hayo.

Tajiri huyo, hufanana na yule aliyeuza ng’ombe alipopata tatizo kubwa mpaka akapata hela zilizomuwezesha kulitatua haraka, kwa sababu naye huzitumia mali zake kwa kuyatatua matatizo yanayoikumba familia yake hiyo mpaka anayamaliza haraka kwa sababu ya umakini wake huo, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “vita imekua kubwa niuze ng’ombe.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzitunza vizuri mali zao ili ziweze kuwasaidia katika kuyatatua haraka matatizo yatakayozikumba familia zao, maishani mwao.

 Mathayo 6:19-34.

masai-7235675_1280

cow-7200409_1280

dances-341961_1280

ENGLISH: THE WAR HAS BECOME BIG, LET ME SELL THE COW.

Once upon a time, there was a man who was rich in domesticated animals. These animals included chickens, goats, sheep, and cows. He used to sell chickens or goats when he had minor hitches in his family for getting money which can solve them because of his thoughtfulness in his life.

But then, one day such rich man had an enormous difficult that required selling a large animal like a cow for getting enough money to solve it. He decided to bring a cow because he wanted to win the war quickly. That is why he said, “the war has become big, let me sell the cow.”

This proverb is related to a rich man who uses his wealth well in his life. This rich man takes upright care of his wealth so that it can support him quickly in solving hitches that will arise in his family, because of his responsiveness in his life. He uses his wealth well until he quickly solves the glitches which arise in his family, because of his thoughtfulness in his life.

This rich man resembles the one who sold his cow when he encountered a big delinquent until he got the money that enabled him to solve it quickly, because he also uses his wealth to solve the hitches which befall his family until he quickly solves them.That is why he says that, “the war has become big, let me sell the cow.”

This proverb imparts in individuals an idea of being so attentive enough to take decent care of their wealth so that they can support them in quickly solving glitches which will befall their families in their lives.

Matthew 6:19-34.

1339. AMANDEGE GASHILA LYASAGA LIGONGOTE DUHU.

Aho kale bhalihoyi bhanhu abho bhayugulaga mandege bhagaponya amagongote gago. Munhu umo agalibhona iligongote ulipelela alihaya giki lilina mandege kunguno oliotubha noyi. Aho olidima umana igiki gashinaga lyasaga ligongote duhu uliponya. Hunagwene agayomba giki, “amandege gashila lyasaga ligongote duhu.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo olileka ililange lya nhungwa jakwe ijawiza ijo olinajo ikale, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo olileka ililange lya gubhambilija chiza abhanhu abho bhalina makoye, ubhiza ng’wimi nholo, na ndalahija obhiye kunguno ya gwilunga mu magele ga bhang’wi bha walwa na bhabehi bha njemu, umuwikaji bhokwe. Uweyi agidumaga na bhanwani bhakwe aha kaya yakwe, kunguno ya gulileka ililange lyakwe ilyawiza linilo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga niligongote ilo gamala guyugulwa amandege galyo, kunguno nuweyi alileka iliange lyakwe ilya gwita mihayo ya wiza wandya gwita mihayo ya bhubhi, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “amandege gashila lyasaga ligongote duhu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleta gwilunga mumagele ga bhanhu abho bhagitaja mihayo ya bhubhi, bho gulidimila chiza ililange lyabho ilyawiza, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mithali 3:14.

Mithali 14:4.

Mithali 14:23.

KISWAHILI: MAHINDI YALISHAISHA LIKABAKIA GUNZI TU.

Hapo zamani walikuwepo watu waliokuwa wanapukuchua mahindi na kuyatupa magunzi yake. Mtu mmoja aliliona gunzi mojawapo akalikimbilia akifikiri kwamba lina mahindi kwa sababu alikuwa ameshikwa na njaa sana. Alipolishika aligundua kwamba kumbe lilikuwa limebakia gunzi tu akalitupa. Ndiyo maana alisema kwamba, “mahindi yalishaisha likabakia gunzi tu.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule aliyeyaacha malezi mema aliyokuwa nayo hapo zamani, katika maisha yake. Mtu huyo, aliyaacha malezi yake mema ya kuwasaidia watu vizuri, akawa mchoyo na mwenye dharau kwa wenzake kwa sababu ya kujiunga na makundi ya walevi na wavuta bhangi, maishani mwake. Yeye hukosana na marafiki zake katika familia yake kwa sababu ya kuiacha tabia yake njema aliyokuwa nayo mwanzoni, akaiga tabia ya kutenda maovu, katika maisha yake.

Mtu huyo hufanana na lile gunzi liliishiwa mahindi kwa kupukuchuliwa, kwa sababu naye ameiacha tabia yake njema ya kutenda mema kwa kuiga matendo maovu, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mahindi yalishaisha likabakia gunzi tu.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha kuiga matendo maovu kwa kuyaishi vizuri malezi mema, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Mithali 3:14.

Mithali 14:4.

Mithali 14:23.

corn-4640522_1280

ENGLISH: THE MAIZE RAN OUT ONLY HUSK REMAINED.

In the past, there were people who were shelling maize and throwing away their husks. One man saw one of the husks and ran to it thinking that it contained maize because he was so hungry. When he caught it, he discovered that it was actually just a husk and threw it away. That is why he said, “the maize ran out only husk remained.”

This proverb is matched to an individual who left respectable upbringing which he had in his past life. Such person left his decent nurture of assisting people well, became greedy and contemptuous of his nobles because of joining groups of drunkards and drug addicts in his life. He is at odds with his friends in his family because of leaving his upright personality that he had at first, and imitated patterns of doing evil deeds in his life.

This individual resembles the husk that ran out of maize by being hulled, because he also has abandoned his decent custom of doing decent deeds by imitating evil deeds in his life. That is why people say to him that, “the maize ran out only husk remained.”

This proverb teaches people about stopping imitating evil deeds by living a respectable nurture, so that they can nicely rear their family members in their lives.

Proverbs 3:14.

Proverbs 14:4.

Proverbs 14:23.

1335. JITAB’O JA NG’WA MULUNGU JIDACHOLELAGWA NG’WA MFUMU.

Ulusumo lunulo luhoyelile munhu uyo ocholaga jitab’o ja Ng’wa Mulungu ng’wa mfumu. Umunhu ng’wunuyo, agashiga aha ng’wa mfumu henaho alibhabhuja ulu bhalinajo ijitab’o jinijo, gukiki bhang’winhe, kunguno oli adinajo weyi umubhuzunya bhokwe.

Abhanhu bhenabho bhagankumya noyi unzunya ng’wunuyo, kunguno abhoyi bhadebhile igiki ijitab’o jinijo, jidikalaga aha ng’wa mfumu, ijoyi jigikalaga kubhazunya nulu kwikelesia. Hunagwene bhagang’wila giki, “ijitab’o ja ng’wa Mulungu jidacholelagwa ng’wa mfumu.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli nzunya uyo agasangijaga mihayo ya ng’wa Mulungu ni ya ng’wa shetani, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajaga ukwisalila ulu oshoga koyi wandya gulamya ya ng’wa shetani, kunguno ya gugayiwa witegelega bho gubhudimila chiza ubhuzunya bhokwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga wita mihayo ya bhubhi aha kaya yakwe kunguno ya gugayiwa witegeleja bhunubho ubho gugudimila chiza umhayo go ng’w Mulungu, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo ocholaga jitab’o ja ng’wa Mulungu ng’wa mfumu, kunguno nuweyi agajaga ukwisalila ukunhu aliita mihayo ya ng’wa Shetani iyabhubhi yiniyo, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ijitab’o ja ng’wa Mulungu jidacholelagwa ng’wa mfumu.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gugudimila umhayo go ng’wa Mulungu bho nduhu ugugusangilija na ya ng’wa shetani, kugiki bhadule kupandika mbango ja kupandika mafumilo mingi na kushiga Ng’widulu, umuwikaji bhobho.

Zaburi 119:33.

Ufunuo 3:15b.

Kutoka 4:15.

KISWAHILI: KITABU CHA MUNGU HAKITAFUTIWI KWA MGANGA WA KIENYEJI.

Methali hiyo, huongelea mtu aliyeenda kutafuta kitabu cha Mungu kwa mganga wa kienyeji. Mtu huyo alifika kwa mganga huyo akawauliza aliowakuta kama kipo kitabu hicho ili wampe, kwa sababu hakuwa nacho katika ukristo wake.

Watu hao walimshangaa sana mkristo huo kwa sababu wao wanaelewa wazi kuwa, kitabu hicho hupatikana kwa wakristo, au Kanisani. Ndiyo maana watu hao walimwambia kwamba, “kitabu cha Mungu hakitafutiwi kwa mganga wa kienyeji.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huchanganya mambo ya Mungu na ya shetani, katika maisha yake. Mtu huyo, huenda kusali kanisani lakini anaporudi huanza kuabudu miungu wengine, kwa kutenda maovu, kwa sababu ya kukosa umakini wa kuuishi vizuri ukristo wake, maishani mwake. Yeye hutenda maovu mengi katika familia yake hiyo kwa sababu ya kukosa umakini huo wa kufuata njia ya kuliishi neno la Mungu vizuri, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeenda kutafuta kitabu cha Mungu kwa mganga wa kienyeji, kwa sababu naye huenda kanisani lakini anaporudi hufuata mambo ya shetani, kwa kutenda maovu, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kitabu cha Mungu hakitafutiwi kwa mganga wa kienyeji.”

Methali hiyo, hufundisha wakristo juu ya kuwa na umakini wa kulishikilia neno la Mungu bila kutenda maovu, ili waweze kupata Baraka nyingi maishani mwao na kuweza kufika Mbinguni.

Zaburi 119:33.

Ufunuo 3:15b.

Kutoka 4:15.

 

ENGLISH: THE BOOK OF GOD IS NOT SOUGHT FROM A TRADITIONAL HEALER.

This proverb speaks of a person who went to seek the book of God to a local medicine man. A certain person went to such medicine man and asked him if he saw the book of God so that he could give it to him, because he did not have it in his Christian life.

These people were very surprised at such Christian because they clearly understand that such book is found among Christians, or in the Church. That is why these people told him that, “the book of God is not sought from a traditional healer.”

This proverb is paralleled to a person who mixes things of God and those of a devil in his life. Such person can pray in church but when he returns he begins to worship other gods, by committing evil deeds, because of a lack of responsiveness of living his Christianity well, in his life. He commits various evil deeds in his family because of a lack of thoughtfulness of following the path of putting into practice the word of God well in his life.

This person resembles the one who went to seek the book of God to a local traditional healer, because he also goes to church but when he returns he follows the possessions of devil by doing evil in his life. That is why people tell him that, “the book of God is not sought from a traditional healer.”

This proverb teaches Christians about being cautious enough to hold on to the word of God without doing evil, so that they can receive several blessings in their lives to the point of reaching Heavenly Kingdom.

Psalm 119:33.

Revelation 3:15b.

Exodus 4:15.

 

bible-2110439_1280

south-africa-742507_1280

praying-5406270_1280

1332. IGULILU LYA NGOKO GUGULA NA GUSINZA NI JIYU JILIB’ONA.

Iligulilu lya ngoko liligulilu ilo bhanhu bhagajingaga na gugula ngoko. Ahi igulilu linilo abhaguji bhagajigulaga ingoko jinijo na gwandwa gujisinza ni jiyu nulu susu jilib’ona kunguno ya kuhaya gupandika hela bho guzuka nyama ya ngoko na guijinja aha nada gunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “igulilu lya ngoko gugula na gusinza ni jiyu jilib’ona.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho b’agitaga mito ga b’ub’i na gasoni na bhana bhalib’ona, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagitaga mihayo ya b’ub’i na ya soni yiniyo habhutongi bho bhana bhabho bho nduhu nulu gucha soni, kunguno bhali na nhungwa ja bhubhi umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagabhalangaga abhana bha ha kaya jabho gwita mihayo ya b’ub’i kunguno ya nhungwa jabho ijabhubhi jinijo, umukikalile kakwe.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga nabho bhasinzaga ngoko ni jiyu jilib’ona, kunguno na bhoyi bhagitaka mihayo ya soni na bhana bhalibhona, umuwikaji bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “igulilu lya ngoko gugula na gusinza ji jiyu jilib’ona.”

Ulusumo lunulo lolanga bhabyaji higulya ya guleka nhungwa ja gwita mihayo ya soni na bhana bhalib’ona, bho gwikala na nhungwa jawiza kugiki bhadule gubhinha lilange lyawiza abhana bhabho bhenabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 5:27-30.

Zaburi 106:39.

Mathayo 22:23-33.

Waefeso 5:3.

1Wathesalonike 4:3-6.

Wakolosai 3:5.

Wagalatia 5:19.

KISWAHILI: GULIO LA KUKU, KUNUNUA NA KUCHINJA NA VIFARANGA WANAONA.

Gulio la kuku ni soko lile ambalo watu huuza na kununua kuku. Kwenye soko hilo wanunuaji wa kuku huwanunua na kuwachinja na vifaranga wakiwa na wanaona, kwa sababu ya kutaka kupata pesa kwa kupika nyama ya kuku na kuiza hapo gulioni. Ndiyo maana watu husema kwamba, “gulio la kuku kununua na kuchinja na vifaranga wanaona.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao hutenda maovu na mambo ya aibu na watoto wakiwa wanaona, katika maisha yao. Watu hao, hutenda maovu hayo na mambo hayo ya aibu mbele ya watoto wao bila hata ya kuona aibu kwa sababu wanatabia mbaya, maishani mwao. Wao huwafundisha watoto wao tabia ya kutenda maovu kwa sababu ya tabia yao hiyo mbaya ya kutenda mambo ya aibu, mbele ya watoto wao hao, katika maisha yao.

Watu hao hufanana na wale waliochinja kuku na vifaranga wakiwa wanaona, kwa sababu nao hutenda maovu na mambo ya aibu mbele ya watoto wao hao, maishani mwao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “gulio la kuku kununua na kuchinja na vifaranga wanaona.”

Methali hiyo, hufundisha wazazi juu ya kuacha tabia ya kutenda mambo ya aibu mbele ya watoto wao, kwa kuishi katika tabia njema, ili waweze kuwapatia malezi mema watoto wao hao, maishani mwao.

Mathayo 5:27-30.

Zaburi 106:39.

Mathayo 22:23-33.

Waefeso 5:3.

1Wathesalonike 4:3-6.

Wakolosai 3:5.

Wagalatia 5:19.

 

ENGLISH: CHICKEN MARKET, TO BUY AND SLAUGHTER WHILE CHICKS ARE WATCHING.

Chicken market is an arcade where people sell and buy chickens. In that arcade, chicken buyers buy and kill them while chicks are watching, because they want to make money by cooking chicken meat and selling it there in the market. That is why people say, “Chicken market, to buy and slaughter while chicks are watching.”

This proverb is related to individuals who do evil deeds by doing shameful acts in front of their children in their lives. These people do those evil deeds shamefully in front of their children without even feeling ashamed because they have wicked manners in their lives. They teach their children practices of doing evil deeds because of their evil conducts of doing shameful deeds in front of their children in their lives.

These people are like those who slaughtered chickens in front of their chicks, because they also commit evil deeds by doing shameful acts in front of their children in their lives. That is why people say to them that, “Chicken market, to buy and slaughter while chicks are watching.”

This proverb teaches parents to stop doing shameful acts in front of their children, by living in virtuous character, so that they can provide their children with worthy upbringings in their lives.

Matthew 5:27-30.

Psalm 106:39.

Matthew 22:23-33.

Ephesians 5:3.

1Thessalonians 4:3-6.

Colossians 3:5.

Galatians 5:19.

 

turkey-218742__480