Akahayile kenako kahoyelile munhu uyo agamilinga ng’wiye kunimo gokwe uyo agalema. Umunhu ng’wunuyo agamilinga ung’wiye ng’wunuyo, gung’wambilija gulima ngunda gokwe kunguno goligutale noyi. Uweyi agalima weyi duhu ukungunda gokwe gunuyo kunguno uyo agamilinga gwiza gung’wambilija agalema. Hunagwene aho bhamuja abhiye ung’winikili ngunda agayomba giki, “namilinga osalang’hana.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adina bhumo bho gulungana na bhiye umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga bhung’wene bho nduhu ugwiyambilija na bhiye ugutumama imilimo yakwe yiniyo, kunguno ya gugayiwa bhumo bhokwe bhunubho ubho gwiyambilija gutumama milimo nabhiye bhenabho, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agadumaga uguyilela chiza ikaya yakwe yiniyo, kunguno ya nhungwa jakwe jinijo ija gugayiwa bhumo nabhiye bhunubho, umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agabhilingwa gujung’wambilija ng’wiye gujulima ngunda ulema, kunguno nuweyi adina bhumo ubho gwiyambilija nabhiye ugutumama imilimo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “namilinga osalang’hana.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhumo bho gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho umuwikaji bhobho bhunubho.
Mathayo 22:1-3.
2Petro 1:3.
Waefeso 5:9.
Mathayo 21:28-31.
KISWAHILI: NIMEMWALIKA AKAKATAA.
Msemo huo huongelea mtu aliyemwalika mwenzake kumsaidia kwenye kazi yake akakataa. Mtu huyo, alimwalika mwenzake huyo kwenda kumsaidia kulima shamba lake kwa sababu lilikuwa kubwa sana. Yeye alilima yeye tu kwenye shamba lake hilo kwa sababu yule aliyemwalika kuja kumsaidia alikataa. Ndiyo maana watu walimuuliza juu ya yule aliyekataa alisema kwamba, “nimemwalika akakataa.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hana ushirikiano wa kusaidiana na wenzake katika kuyatekeleza majukumu yake, maishani mwake. Mtu huyo huishi peke yake bila ya kusaidiana na wenzake wanaomwalika kuwasaidia kufanya kazi zao, kwa sababu ya kukosa ushirikiano wake na wenzake, katika maisha yake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake hiyo, kwa sababu ya kukosa ushirikiano wake na wenzake katika utekelezaji wa majukumu yao hayo, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyekataa mwaliko wa kumsaidia mwenzake kulima shamba lake, kwa sababu naye hana ushirikiano wa kusaidiana kufanya kazi na wenzake, maishani mwake. Ndiyo maana watu husema juu yake kwamba, “nimemwalika akakataa.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na ushirikiano wa kusaidiana kufanya kazi na wenzao vizuri, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.
Mathayo 22:1-3.
2Petro 1:3.
Waefeso 5:9.
Mathayo 21:28-31.
ENGLISH: I INVITED HIM, BUT HE REFUSED.
This saying refers to a person who invited his colleague to help him with his work, but the colleague refused. He invited him to help cultivate his field because it was too large for one person. As a result, he cultivated the field alone since the one he invited refused to help. When people asked him about his colleague, he replied, “I invited him, but he refused.”
This saying is compared to a person who does not cooperate with his colleagues in carrying out his responsibilities in life. Such a person lives and works alone, refusing to join others when they invite him to help with their work. Because of his lack of cooperation, he struggles to fulfill his responsibilities and may even fail to raise his family well.
This person is like the one who refused to help cultivate his colleague’s field. He does not work together with others in his daily life. That is why people say about him, “I invited him, but he refused.”
This saying teaches an importance of partnership and cooperation. People should help one another in their work so that they can fulfill their responsibilities and build strong families in their lives.
Matthew 22:1–3.
2 Peter 1:3.
Ephesians 5:9.
Matthew 21:28–31.














