1373. JIDASHIMEJIJE ING’HINGI.

Olihoyi munhu uyo aginhiwa nimo go gusimbila ng’hingi ja gusengela numba. Umunhu ng’wunuyo agajisimbila ing’hingi jinijo ugabhigwilija abho bhang’winha unimo gunuyo igiki omalaga ugugutumama. Aho bhiza ugugulingula unimo gokwe bhubhona giki jidashimejiwe ugusimbilwa ing’hingi jinijo kunguno bhajidimaga jayugwa duhu. Hunagwene abhagayomba giki, “jidashimejije ing’hingi.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alingokolo ugutumama imilimo ya aha kaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo atogilwe gwikala wigashaga duhu nulu lyashigaga ilikanza ilya gutumama milimo yakwe kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi aligikala ukoyiwa ni koye lya bhuhab’i bho gubhiza na nduhu jikolo aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho ubho gwikala wigashije ahikanza lya gutumama milimo yakwe, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo adajishimejije ing’hingi ugujisimbila, kunguno nuwei alingokolo ugutumama imilimo ya kaya yakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “jidashimejije ing’hingi.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gwihanda gutumama milimo yabho chiza bho bhuleka bhugokolo bho gutumama milimo kugiki bhadule gupandika sabho jagubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mithali 10:4.

Mithali 13:7-8.

Mithali 19:4.

KISWAHILI: NGUZO HAZIKUCHIMBIWA KWA KINA KIREFU.

Alikuwepo mtu aliyepewa kazi ya kuchimbia nzuzo za kujengea nyumba. Mtu huyo, alizichimbia nguzo hizo akaenda kuwataarifu wale waliompatia kazi hiyo kuwa ameimaliza. Walipofika kuikagua kazi yake wale waliompatia kazi hiyo waligundua kuwa nguzo hizo hazikuchimbiwa vizuri kwa sababu kila walipozigusa kidogo zilianguka. Ndiyo maana walisema kwamba, “nguzo hazikuchimbiwa kwa kina kirefu.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mvivu wa kufanya kazi kwenye familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo hushinda akiwa amekaa tu hata wakati wa kufanya kazi kwa sababu ya uvivu wake huo, maishani mwake. Yeye husumbulia na tatizo la umakini wa kutokuwa na kitu katika familia yake kwa sababu ya uvivu wake huo wa kushinda amekaa hata wakati wa kufanya kazi, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeshindwa kuitekeleza vizuri kazi ya kuchimbia nguzo aliyopewa, kwa sababu naye ana uvivu wa kutokufanya kazi zake mpaga anasumbuliwa na tatizo la umaskini wa kutokuwa na kitu katika familia yake, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba “nguzo hazikuchimbiwa kwa kina kirefu.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao bila ya kuzembea katika kuyatekeleza majukumu yao, ili waweze kupata mali za kuwasaidia katika kuziendelea vizuri familia zao, maishani mwao.

Mithali 10:4.

Mithali 13:7-8.

Mithali 19:4.

ENGLISH: THE PILLARS WERE NOT DUG DEEP.

There was a man who was given a task of digging foundations for a house. Such man dug pillars and went to inform those who had given him that task that he had finished. When they arrived to inspect his work, those who had given him the task discovered that those pillars were not dug properly because every time they fell after touching them. That is why they said, “The pillars were not dug deep.”

This proverb is equaled to a person who is lazy to work in his family, in his life. Such person wins by just sitting down even when working because of his laziness, in his life. He suffers from the difficult of not having anything in his family because of his laziness of sitting down without working in his life.

This person is like the one who failed to properly carry out the task of digging a pillar given to him, because he is also lazy in doing his work until he is troubled by the problem of poverty of having nothing in his family, in his life. That is why people say to him that “the pillars were not dug deep.”

This proverb teaches people about working hard enough to do their jobs without being lazy in carrying out their responsibilities, so that they can obtain much wealth enough to help them in decent development of their families in their lives.

Proverbs 10:4.

Proverbs 13:7-8.

Proverbs 19:4.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.