1291. LYATUMUKILA SI KI?

Imbuki ya kahayile kenako ilolile bhasimbi bha ng’ana. Abhanhu bhenabho bhagikalaga bhubhugilija uko jiligele ing’ana jinijo kunguno ya witegeleja bhobho ubho guhaya gumana chiza uko jiligelela kugiki bhaje koyi bhagajisimbe. Hunagwene bhagabhujaga giki, “lyatumikila si ki?”

Akahayile kenako kakagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagwitilaga bhuengeji bhutale bhuli nimo uyo alihaya gugutumama haho atali ugugwandya umubhutumami bhokwe bhunubho. Umunhu ng’wunuyo agawitaka ubhukengeji bhunubho bho gubhugilija chiza ukubhanhu abho bhagudebhile chiza unimo gunuyo, kugiki nanghwe agudebhe chiza kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga matwajo mingi aha kaya yakwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho gugwitila bhukengeji bhuli nimo gwene uyo alihaya gugutumama aho atali ugugwandya, umubhutumami bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nabho bhabhugilijaga chiza uko jigelelaga ing’ana kugiki bhaje bhagajisimbi koyi, kunguno nuweyi agagwitilaga bhukengeji bhuli nimo gwene uyo alihaya gugutumama hayo atali ugugwandya kugiki adebhe chiza isolobho jago na agwandye lulu, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agabhujaga giki, “lyatumukila si ki?”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gugwitila bhukengeji bhuli nimo gwene uyo bhali haya gugutumama haho bhatali ugugwandya, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umubhutumami bho milimo yabho yiniyo.

Mambo ya walawi 5:4.

Waamuzi 19:30.

KISWAHILI: LIMELIPUKIA ARDHI GANI?

Chanzo cha msemo huo huangalia wachimbaji wa Alimasi. Watu hao huwa wanaulizia mahali ambapo Almasi hizo zimeonekana kwa sababu ya umakini wao wa kutaka kufahamu vizuri kule zilipoonekana ili waende kuzichimba huko. Ndio maana watu hao huwa wanauliza kwamba, “limelipukia Ardhi gani?”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya utafiti mkubwa wa kila kazi anayotaka kuifanya kabla hajaianza kuitekeleza katika kazi zake. Mtu huyo huufanya utafiti huo kwa kuulizia kwa watu wanaoifahamu vizuri kazi hiyo kwa sababu ya umakini wake huo wa kutaka kuifahamu vizuri kazi hiyo kabla ya kuianza, maishani mwake. Yeye hupata mafanikio mengi katika familia yake kwa sababu ya umakini wake huo wa kuifanyia utafiti kila kazi anayotaka kuifanya kabla hajaianza kuitekeleza, katika kazi zake.

Mtu huyo hufanana na wale walioulizia vizuri kule zilipopatikana zile Almasi ili waende kuzichimba huko, kwa sababu naye huifanyia utafiti kila kazi anayotaka kuifanya kabla hajaianza ili afahamu faida zake ndipo aianze kuitekeleza, maishani mwake. Ndiyo maana mtu huyo huuliza kwamba, “limelipukia Ardhi gani?”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuifanyia utafiti kila kazi ile wanayotaka kuifanya kabla hawajaianza kuitekeleza, ili waweze kupata mafanikio mengi katika kazi zao.

Mambo ya walawi 5:4.

Waamuzi 19:30.

ENGLISH: WHICH LAND HAS IT EXPLODED?

The cradle of the above saying looks at the diamond miners. These people always ask where the Diamonds have been seen because of their interest in knowing exactly where they were seen so they can go there and mine them. That is why people always ask, “Which land has it exploded?”

This saying is related to a man who does a lot of researches on every job which he wants to do before implementing it in his work. Such person does research by asking people who know the job well because of his good attention enough to clearly know the job before starting it in his life. He gets a lot of success in his family because of his focus on researching every job which he wants to do before implementing it in his jobs.

This person is similar to those who asked well where the Diamonds were found so they could go there to mine them, because he also researches every job which he wants to do before starting it so as to know its benefits enough to implement it, in his life. That is why he asks that, “Which Land has it exploded?”

This saying teaches people about being careful enough to research every job which they want to sort out before doing it, so that they can get a lot of success in their jobs.

Leviticus 5:4.

Judges 19:30.

 

hand-5443280_1280

caterpillar-4374222_1280

ice-4444860_1280

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.