Akahayile kenako kalolile shili. Ishili jinijo jili jiliwa ijo jigasanjiyagwa mumasangu kugili ganone chiza. Ijoyi jigalimagwa jazwa na gulandala chiza mpaga amadutu gajo gabhiza makubhi manonu gagulila abhanhu. Abhanhu bhagajilanhanaga mpaga jakula na kupya chiza kunguno ya wiza bhojo bhunubho. Hunagwene bhagiwilaga giki, “mayu nilang’hanijage shili.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli ng’wana ng’waniki uyo agalelagwa chiza na bhabyaji bhakwe umukikalile kakwe. Ung’waniki ng’wunuyo, agakulaga adebhile ugutumama imilimo nu gwikala chiza na bhanhu kunguno ya gulangwa chiza na bhabyaji bhakwe bhenabho. Uweyi agayilelaga chiza ikaya yakwe bho gubhalang’hanila ilange lya wiza abhanhu bhakwe kunguno ya lilange lya wiza ilo winhiwa na bhabyaji bhakwe bhenabho, umuwikaji bhokwe.
Ung’waniki ng’wunuyo agikolaga ni shili ijo jigalang’hanwa chiza mpaga jibhiza jiliwa jinonu, kunguno nuweyi olelwa chiza mpaga udebha ugubhalang’hana abhanhu bhakwe bho gubhalela chiza, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “mayu nilang’hanijage shili.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhalanga chiza abhana bhabho kugiki bhadule gukula ni lange lya kujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Waefeso 6:4.
Esta 2:7.
Mithali 22:6.
1Thimotheo 5:10.
KISWAHILI: MAMA NITUNZIE KUNDE.
Msemo huo, huangalia kunde. Kunde hizo ni chakula ambacho huchanganywa kwenye makande ili kuyanogesha. Zenyewe zinapopandwa huota na kutambaa mpaga majani yake huwa mboga tamu ya watu kulia chakula. Watu huzitunza vizuri kunde hizo mpaga zinakomaa na kuiva kwa sababu ya utamu wake huo. Ndiyo maana watu hao huambiana kwamba, “mama nitunzie kunde.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa msichana yule aliyelelewa vizuri na wazazi wake, katika maisha yake. Msichana huyo, hukua akiwa anayaelewa vizuri majukumu ya kufanya kazi na kuishi vizuri na watu kwa sababu ya malezi hayo mema aliyolelewa na wazazi wake. Yeye hufanikiwa kuilea vizuri familia yake kwa kuwatunza na kuwakuza watu wake katika malezi mema kwa sababu ya kulelewa vizuri na wazazi wake hao, maishani mwake.
Msichana huyo hufanana na zile kunde zilizotunzwa vizuri mpaga zikafikia hatua ya kuwa chakula kizuri, kwa sababu naye amelelewa vizuri mpaka akafahamu kuwatunza watu wake kwa kuwalea vizuri, maishani mwake. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “mama nitunzie kunde.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwalea watoto wao kwa kuwapatia malezi mema ya kuwawezesha kuishi vizuri na watu ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.
Waefeso 6:4.
Esta 2:7.
Mithali 22:6.
1Thimotheo 5:10.
ENGLISH: MOTHER, TAKE CARE OF THE BEANS FOR ME.
This saying looks at the beans. These beans are foods which are mixed in dough to make it nice. When they are planted, they sprout and crawl, and their leaves become delicious vegetable for people to eat. People take good care of them when they mature and ripen because of their sweetness. That is why people tell each other that, “mother, take care of the beans for me.”
This saying is equated to a girl who was raised well by her parents, in her life. Such girl grows up with a good understanding of responsibilities of working and living well with people because of good upbringing in which she was brought up by her parents. She manages to raise her family well by taking care of and nurturing her people in a good upbringing because of being well raised by her parents in life.
This girl resembles those were well-cared-for beans until they reach the point of being good food, because she has also been well-raised until she learned to take care of her people by raising them well in her life. That is why they tell people that, “mother, take care of the beans for me.”
This saying teaches people about nurturing their children by providing them with good education enough to enable them live well with people so that they can raise their families well, in their lives.
Ephesians 6:4.
Esther 2:7.
Proverbs 22:6.
1 Timothy 5:10.
