1053. KALAGU –  KIZE. ILALE LWANE LITALE LILINA JIGOGO JIMO – NDA NA NKUNDI.

Ikalagu yiniyo, ihoyelile higulya ya Nda na Nkundi ja ng’wa munhu. Inda ya ng’wa munhu isolile ibala litale ilo ligikolanijiyagwa ni ilale, alu nkundi guli gumo duhu, uyo gugikolanijiyagwa na jigogo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ilale lyane litale llilina jigogo jimo – Nda na Nkundi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa ku abhanhu abho bhagikalaga bhiyigwile chiza, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagapangaga kihamo imilimo ya gutumama iyo bhagatumamaga bho gwiyambilija chiza chiniko kunguno ya ng’wigwana gobho na witogwi bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagikalaga na bhuyeji bhutale aha kaya yabho kunguno ya gwikala na ng’wigwano gobho gunuyo, umukikalile kabho.

Abhanbu bhenabho bhagikolaga na nda na nkundi ijo jigikolaga kihamo umumili go ng’wa munhu, kunguno nabhoyi bhagatumamaga milimo yabho kihamo na bho ng’wigwano gutale aha kaya yabho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “ilale lwane litale lilina jigogo jimo – Nda na Nkundi.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’wigwano go gutumama milimo yabho bho gwiyambilija kihamo umuwikaji bhobho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Waefeso 5:21- 26.

Utatu Mtakatifu.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

SHAMBA LANGU KUBWA LINA KISIKI KIMOJA – TUMBO NA KITOVU.

Kitendawili hicho chaongelea juu ya tumbo na kitovu zilizopo pamoja kwenye mwili wa mtu. Tumbo la mtu huchukua sehemu kubwa ambayo hufananishwa na shamba, lakini kitovu ni kimoja tu, ambacho hufananishwa na kisiki. Ndiyo maana watu husema kwamba, “shamba langu kubwa lina kisiki kimoja – tumbo na kitovu.” 

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale ambao huishi kwa uelewano mzuri, katika maisha yao. Watu hao, hupanga mipango yao ya kazi kwa pamoja kiasi cha kutosha kuzitekeleza vizuri kazi hizo kwa kusaidiana kwa sababu ya uelewano na upendo wao huo. Wao huishi maisha ya furaha kubwa kwenye familia yao, kwa sababu ya ushirikiano na uelewano wao huo, katika maisha yao.

Watu hao hufanana na tumbo na kitovu viishivyo pamoja mwilini mwa mtu, kwa sababu nao hushirikiana kufanya kazi kwa pamoja na kwa uelewano mkubwa kwenye familia yao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “shamba langu kubwa lina kisiki kimoja – tumbo na kitovu.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na uelewano wa kufanya kazi zao kwa kusaidiana pamoja, katika maisha yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Waefeso 5:21- 26.

Utatu Mtakatifu.

man-7440399__480

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.