Imbuki ya kahayile kajisuguma kenako, ifumilile kuwikaji bho muchalo umo igiti ja bhujiku mara hingi, jigenhaga bhobha, na wibhakizu ukubhanhu bhenebho. Giko lulu, ulu ligela lisana nulu lya ng’weji nulu lya moto ligenhaga bhuholele na bhupanga. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “lisana lyagwaga mugiti.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinikujo lya gwenha wisagiji, na bhunhana ukubhanhu bhakwe ahikanza lya maluho, umuwikaji bhokwe bhunubho. Umunhu ng’wunuyo, agabhenhelaga nhulu ja wiza abhanhu bhakwe abho bhalina makoye, kunguno ya likujo lyakwe linilo umukikalile kakwe kenako. Uweyi agabhizaga lisana lya kubhatimila chiza abhanhu bha ha kaya yakwe kunguno ya likujo lyakwe ilyagubhatongela chiza umuwikaji bhokwe bhunubho.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nilisana ilo ligabhatimila abhanhu abho bhalimugiti mpaka bhuyega, kunguno nuweyi agabhatongelaga bho likujo abhanhu abho bhalina makoye mpaga bhayega umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu abhenabho bhagang’witanaga lisana bho guyomba giki, “lisana lyagwaga mugiti.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na nikujo lya gubhinha nhulu jawiza ijagubhatongela chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwenha lisana ukubhichabho abho bhalimugiti umukaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.
Yohana 8:12.
Yohana 3:19-21.
Luka 8:16.
Mathayo 4:15-16.
KISWAHILI: MWANGA UMEANGUKA GIZANI
Msemo huu wa Kisukuma unatokana na maisha ya kitamaduni ya kijijini, ambapo giza usiku mara nyingi huleta hofu, kutokuwa na uhakika, na hatari. Katika nyakati kama hizo, kuonekana ghafla kwa mwanga iwe kutoka mwezini, motoni, au taa kulileta utulivu, usalama, na uwazi. Kifungu “mwanga umeanguka” kinaelezea wazo kwamba mwanga umeingia bila kutarajia mahali ambapo hapo awali palikuwa na giza, na kubadilisha hali hiyo kabisa. Ndiyo maana watu walisema kwamba “mwanga umeanguka gizani.”
Msemo huu hulinganishwa kwa mtu anayeleta matumaini, ukweli, au suluhisho katika wakati wa mkanganyiko, mateso, au ujinga katika maisha yake. Mtu kama huyo huonekana wakati mambo yanaonekana kuwa hayaeleweki au magumu na huwasaidia wengine kuona njia sahihi kwa kuwaletea wema wanajamii wake kwa sababu ya hekima yake kwa watu wake. Yeye huwa mwanga kwa wanafamilia wake kwa sababu ya hekima yake ya kuwaongoza vizuri inayomfanya aishi kwa busara katika maisha yake.
Mtu huyu hufanana ule mwanga ulioleta usalama gizani kwa sababu pia naye huleta habari njema kwa wanafamilia wake kwa kuwaongoza kwa busara katika maisha yake. Ndiyo maana wanafamilia wake hao husema juu yake kwamba, “mwanga umeanguka gizani.”
Msemo huu huwafundisha watu kuhusu umuhimu wa kuleta ukweli ambapo kuna mkanganyiko ili waweze kufikia malengo yao katika maisha yao. Hiyo ndiyo kusema kwamba, maarifa, hekima, na wema vinaweza kushinda giza katika familia.
Yohana 8:12.
Yohana 3:19-21.
Luka 8:16.
Mathayo 4:15-16.
Yohana 1:5 “Nuru hung’aa gizani, wala giza halikuishinda.”
Isaya 9:2 “Watu wanaotembea gizani wameona nuru kuu.”
Mathayo 5:14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.”
Waefeso 5:8 “Kwa maana hapo awali mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana.”
Mistari hii inaonyesha ujumbe ule ule: nuru inayoashiria ukweli, uwepo wa Mungu, na haki ambayo hushinda giza na kuleta uzima, mwelekeo, na tumaini.
ENGLISH: LIGHT HAS FALLEN IN THE DARKNESS
This Sukuma saying comes from traditional village life, where darkness at night often brought fear, uncertainty, and danger. In such moments, the sudden appearance of light whether from the moon, fire, or a lamp brought relief, safety, and clarity. The phrase “light has fallen” expresses the idea that illumination has unexpectedly entered a place that was once covered in darkness, transforming the situation completely. That is why people say “light has fallen in the darkness.”
This saying is compared to a person who brings hope, truth, or solutions in a time of confusion, suffering, or ignorance in his life. Such a person appears when things seem unclear or difficult and helps others to see the right path by bringing goodness to his societal members because of his wisdom to his people. He becomes the light to his family members because of his wisdom which make him live wisely in his life.
This person resembles the light which brought safety in the darkness because he also brings good news to his family members by guiding them wiselly in his life. That is why his family members say about him, “light has fallen in the darkness.”
This saying teaches people about an importance of bringing truth where is confusion so that, they can actualize their goals in their lives. That is to say, knowledge, wisdom, and goodness can overcome darkness in families.
John 8:12.
John 3:19-21.
Luke 8:16.
Matthew 4:15-16.
John 1:5 “The light shines in the darkness, and the darkness has not overcome it.”
Isaiah 9:2 “The people walking in darkness have seen a great light.”
Matthew 5:14 “You are the light of the world.”
Ephesians 5:8 “For you were once darkness, but now you are light in the Lord.”
These verses reflect the same message: that light symbolizing truth, God’s presence, and righteousness which overcomes darkness and brings life, direction, and hope.