1479. MHELA YA DALALI.

Olihoyi munhu uyo ali mpeji noyi umuchalo ja ng’wa maswele. Umunhu ng’wunuyo, obhashigaga pye abhiye kunguno ya nguzu yakwe jinijo umuwikaji bhokwe bhunubho.

Aliyo, kihamo nubhupeji bhokwe bhunubho, uweyi adapandikile solobho yoseyose kunguno ya gugayiwa witegeja umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witana giki, “mhela ya dalili.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajitumamilaga sagala isabho ijo agajipandikaga umubhutumami bhokwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambija guchola sabho mpaga ojipandika chiza na oduma ugujilanhana chiza, kunguno ya kujitumamila sagala umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga ukoya na nzala aha kaya yakwe kunguno ya kujikenagula sagala isabho ijo agajipandikaga umutumami bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo opelaga noyi bho nduhu gupandika solobho yoseyose kunguno nuweyi agajitumamilaga sagala isabho ijo agajipandikaga umubhutumami bhokwe mpaga oyukoya na nzala, aha kahaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “mhela ya dalali.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujilanhana chiza isabho ijo bhagajipandikaga umubhutumami bhobho, kugiki jidule gubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Mhubiri 5:10.

Luka 15:11-13.

KISWAHILI: MKIMBIAJI WA BURE.

Alikuwepo mtu aliyekuwa mkimbiaji sana katika kijiji cha mwa mashele. Mtu huyo, alikimbia mpaka akawaacha wenzake wote kwa sababu ya kuwa na nguvu nyingi, maishani mwake.

Lakini, pamoja na ukimbiaji wake huyo, yeye hakupata faida yoyote kwa sababu ya kukosa umakini katika maisha yake hayo. Ndiyo maana watu walimuita jina la “mkimbiaji wa bure.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huzitumia hovyo mali anazozipata matika kazi zake. Mtu huyo, hujibidisha kutafuta mali mpaka anazipata ambazo hushindwa kuzitunza vizuri, kwa sababu ya kuzitumia hovyo, maishani mwake. Yeye husumbuliwa na tatizo la kukosa chakula katika familia yake hiyo, kwa sababu ya kukosa umakini wa kuzitunza vizuri mali anazozipata, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekimbia sana bila ya kupata faida yoyote, kwa sababu naye huzitumia hovyo mali anazozipata mpaka anafikia hatua ya kukosa chakula katika familia yake hiyo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita jina la “mkimbiaji wa bure.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzitunza vizuri, mali wanazozipata katika kazi zao, ili ziweze kuwasaidia katika kuzijenga vizuri familia zao hizo, maishani mwao.

Mhubiri 5:10.

Luka 15:11-13.

 

ENGLISH: FREE RUNNER

There was once a man in the village of Mwamashele who was known as a very fast runner. He would run with great strength and leave all his companions far behind. No one could match his speed.

However, despite all his running, he gained no benefit. He ran without direction and without purpose. In the end, his effort brought him nothing because he lacked attention and wisdom in how he used his strength. For this reason, people called him the “free runner.”

This saying compares such a runner to a person who works hard to earn money but spends it carelessly. That person struggles and labors until he earns income, yet he wastes it without planning or saving. Because of his lack of attention, he later suffers from shortage, even lacking enough food for his family.

Just like the runner who used his energy without gaining anything, the wasteful person uses his earnings without benefit. His hard work produces no lasting results. That is why people call him the “free runner.”

This saying teaches an important lesson: it is not enough to work hard; one must also use what he earns wisely. Careful management of wealth helps build and support a family well.

As it is written in Ecclesiastes 5:10, loving money without wisdom never brings satisfaction. Likewise, in Gospel of Luke 15:11–13, the parable of the prodigal son shows how wasteful living leads to suffering.

Therefore, people should not only run fast in life, but also run with purpose and wisdom.

 

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.