1476. UNG’WENE OKILAGA BUNASI.

Olihoyi munhu uyo wikalaga muchalo ja Gabale. Umunhu ng’wunuyo agageniha kubhutemi bhungi kunguno ohayaga gujugisha kubhutemi bhungi. Uweyi agabhawila abhanhu bhakwe aho okila bhutemi bhungi kunguno oli ajidebhile imbimbi ja bhutemi bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki, “ung’wene okilaga bunasi.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina witegeleja bho gujidebha chiza imbimbi jakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, ojilanhanaga imbimbi jakwe inija bhiye bho guhoya chiza na bhiye bhenabho kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga chiza na bhanhu bha muchalo jakwe jinijo kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho gujidebha chiza imbimbi jakwe, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oliajidebhile chiza imbimbi jakwe mpaka ubhawila abhiye aho okila bhutemi bhungi umubhugeni bhokwe bhunubho, kunguno nuweyi alina witegeleja bho gujidebha chiza imbimbi jakwe mpaga ojilanhana chiza, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ung’wene okilaga bunasi.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhitegeleja bho gujibebha chiza isabho jabho nija bhichabho, kugiki bhadule gujilanhana chiza, umuwikaji bhobho bhunubho.

Ezekieli 12:3.

Mwanzo 47:21.

Luka 10:2.

 KISWAHILI: HUYO AMEVUKA UTAWALA.

Alikuwepo mtu aliyeishi kwenye kijiji cha Gabale. Mtu huyo, alisafiri kwenda nje ya utawala wake kwa sababu alitaka kwenda kusalimia huko. Yeye aliwataarifu watu wake alipovuka utawala wake huo na kuingia kwenye utawala ng’wingine kwa sababu alikuwa anaielewa vizuri mipaka yake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “huyo amevuka utawala.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana umakini wa kuielewa vyema mipaka yake, katika maisha yake. Mtu huyo, huilinda vyema mikapa yake na ya wenzake kwa kuongea vyema nao kwa sababu ya umakini wake huo maishani mwake. Yeye huishi vizuri na watu wa kijiji chake hicho kwa sababu ya umakini wake huo wa kuielewa vyema mikapa yake, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeielewa vyema mikapa yake mpaka akawataarifu wenzake alipoingia kwenye utawala mwingine katika safari yake hiyo, kwa sababu naye ana umakini wa kuielewa vyema mipaka yake na ya wenzake mpaka akailinda vizuri, maishani mwake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “huyo amevuka utawala.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzielewa vyema mali zao na wenzao, ili waweze kuzilinda vyema, maishani mwao.

Ezekieli 12:3.

Mwanzo 47:21.

Luka 10:2.

 

ENGLISH: HE HAS CROSSED THE RULE

There was a man who lived in the village of Gabale. One day, he traveled beyond his boundary because he wanted to go and greet people in another place. Since he clearly understood the limits of his own rule, he informed his people when he crossed into another rule. He respected the boundaries and did not enter secretly. Because of this, people said of him, “He has crossed the rule.”

This saying is compared to a person who carefully understands his own boundaries in life. Such a person protects his responsibilities and respects the boundaries of others. He speaks well with his colleagues and neighbors because he values peace and order. By recognizing limits and acting with care, he lives peacefully with the people of his village.

He is like the man who understood his boundaries so well that he informed others when he entered another rule during his journey. In the same way, a wise person protects both his own responsibilities and those of others. That is why people say of him, “He has crossed the rule.”

This saying teaches people to respect boundaries, whether they are possessions, responsibilities, or relationships, so that they may protect them well in their lives.

The teaching of respecting boundaries can also be seen in the Bible, such as in Book of Ezekiel 12:3, Book of Genesis 47:21, and Gospel of Luke 10:2, where responsibility, movement, and duty are shown within proper order and understanding.

 

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.