1462. OBALAGASHA UKUNGUBHALA ILIMI LYASEB’AGA.

Imbuki ya kahayile kenako kahoyelile jisunva ijo jigitanagwa kungub’ala. Ikungub’ala yiniyo jilijisunva ijo jikolile na bhushishi. Akajisunva kenako kali kabhuluguti gete ako kagigelaga ilimu ulu lyaseb’a. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki “obalagasha ukungub’ala ilimi lyaseb’aga.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyumilijaga gutumama milimo yakwe chiza nulu lyaseb’aga ilimi umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo bhugelaga ubhujiku ogatumama milimo yakwe chiza mpaga lyagalib’ila ilimi kunguno ya wiyumilija bhokwe ubho gutumama milimo yakwe nulu lyasebaga ilimi, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi noyi aha kaya yakwe yiniyo kunguno ya wiyumilija bhokwe ubho gutumama milimo yakwe chiza chiniko, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nakakungub’ala ako kagigelaga ulu lyaseb’aga ilimi, kunguno nuweyi agiyumilijaga gutumama milimo yakwe chiza nulu lyasebhaga ilimi, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “obalagasha ukungub’ala ilimi lyaseb’aga.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na wiyumilija bho gutumama milimo yabho chiza, nulu lyaseb’aga ilimi, kugiki bhadule gupandika sabho ningi umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Luka 12:36-40.

Luka 13:24-26.

Yakobo 5:7-8.

2Thimotheo 4:5.

KISWAHILI: KACHANGAMUKA KIUMBE JAMII YA SISIMIZI JUA LIMEKUWA KALI.

Chanzo cha msemo huo humwongelea kiumbe jamii ya sisimizi. Jamii hiyo ya sisimizi ni kiumbe kinachofanana na sisimizi. Kiumbe hicho ni kichangamfu sana ambacho huonenaka wakati jua linapokuwa kali sana. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kachangamuka kiumbe jamii ya sisimizi jua limekuwa kali.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvumilia kufanya kazi zake hata wakati wa jua kali, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya kazi zake kuanzia asubuhi hadi jioni kwa sababu ya uvumilivu wake huo wa kufanya kazi  vizuri hata wakati wa jua kali, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi sana katika familia yake kwa sababu ya uvumilivu wake huo wa kuyatekeleza vizuri majukumu yake wakati wote, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na kile kiumbe jamii ya sisimizi ambacho huonekana wakati wa jua kali, kwa sababu naye huyatekeleza vizuri majukumu yake hata wakati wa jua kali, maishani mwake. Ndiyo maana watu husema juu yake kwamba, “kachangamuka jamii ya sisimizi jua limekuwa kali.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuyatekeleza vizuri majukumu yao hata wakati wa jua kali, ili waweze kupata mali nyingi katika familia zao, maishani mwao.

Luka 12:36-40.

Luka 13:24-26.

Yakobo 5:7-8.

2Thimotheo 4:5.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.