1440. NAJA.

Aho kale olihoyi munhu uyo agasumba lugendo lo guja bhugeni. Umunhu ng’wunuyo agabhitana abhanwani bhakwe bhuja aha kaya yakwe kunguno ya gubhalaga. Aho bhaja abhanwani bhakwe bhenabho abhagabhawila giki bhikale mhola uweyi aligeniha. Hunagwene agayomba giki, “naja.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga chiza na bhanhu bha ha kaya yake. Umunhu ng’wunuyo, agabhalangaga lilange lya gwikala bhitogilwe chiza bho gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi apandikaga mbango ja gwikala na bhuyegi aha kaya yakwe yiniyo kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho ubho guyilela chiza ikaya yakwe, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agabhitana gubhalaga abhanwani bhakwe aho ohaya gugeniha, kunguno nuweyi agajaga gujubhalanga lilange lya gwikala chiza na bhanhu umuwikaji bhokwe. Hunagwene ulu alibhalaga agayombaga giki, “naja.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho gubhalela chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi umukaya jabho jinijo.

Kutoka 18:27.

1Wafalme 8:66.

Marko 6:46.

2 Wakorintho 2:13.

KISWAHILI: NAENDA.

Hapo zamani alikuwepo mtu aliyetaka kusafiri kwenda ugenini. Mtu huyo aliwaita rafiki zake kwenda nyumbani kwake kwa sababu alitaka kuwaaga. Walipofika kwake wale rafiki zake aliwaambia wakae salama kwa sababu yeye alikuwa anaenda ugenini. Ndiyo maana aliwaambia kwamba, “naenda.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule anayeishi vizuri na watu wa nyumbani mwake katika maisha yake. Mtu huyo, huwafundisha watu wake malezi ya kuishi kwa upendo wakisaidiana vizuri katika kufanya kazi zao, kwa sababu ya uaminifu wake huo maishani mwake. Yeye hupata baraka za kuishi kwa furaha katika familia yake hiyo kwa kwa sababu ya uaminifu wake huo wa kuwafundisha malezi mema watu wake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewaita rafiki zake ili awaage alipotaka kusafiri, kwa sababu naye kuenda kuwafundisha malezi mema watu wake katika maisha yake. Ndiyo maana anapotaka kuwaacha huwaambia kwamba, “naenda.”

Msemo huyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kuwalea vyema watu wao, ili waweze kuishi kwa furaha katika familia zao, maishani mwao.

Kutoka 18:27.

1Wafalme 8:66.

Marko 6:46.

2 Wakorintho 2:13.

ENGLISH: I AM GOING.

Once upon a time, there was a man who wanted to travel abroad. Before leaving, he invited his friends to his house so that he could say goodbye to them. When they arrived, he spoke to them kindly and encouraged them to live safely and peacefully together, because he was about to depart. That is why he said to them, I am going.”

This saying is equated to a person who lives well with the people in his household. Such a person teaches his family good upbringing: to live with love, to help one another, and to work together honestly. Because of his integrity and good example, he receives blessings and lives happily with his family.

This person is like the man who called his friends together before his journey. Before leaving, he made sure to leave behind good teachings and wise guidance. In the same way, a responsible person prepares his people well before he departs, whether through words, actions, or example. That is why he can confidently say, “I am going.

This saying teaches the importance of honesty, responsibility, and good upbringing, so that people may live in peace and happiness within their families and communities.

Exodus 18:27

1 Kings 8:66

Mark 6:46

2 Corinthians 2:13.

 

 

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.