1410. WIGUSHA B’O B’ANIGINIGI LUB’UB’U LO MVAA.

Abhaniginigi bhagigushaga bho gutumya lub’ub’u guti mva jilisha. Abhanigini bhenabho bhagatumyaga lub’ub’u kunguno bhagigusijaga masalu nulu moto kunguno ya bhuniginigi bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “wigusha b’o b’aniginigi lub’ub’u lo mvaa.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagatumamaga nyanigini imilimo yabho umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagatumamaga hadoo duhu imilimo yabho bhandya gwigusha mpaga bhaduma uguimala imilimo uguitumama kunguno ya gudilila mahoya ahikanza lya milimo yao umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagagayiyagwa ijiliwa aha kaya jabho kunguno ya bhuniginigi bhobho ubho guduma uguitumama chiza imilimo yabho, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga na bhaniginigi abho bhagadililaga ligusha bho nduhu uguitumama imilimo yabho, kunguno nabhoyi bhagadililaga mahoya mpaga bhaduma uguitumama chiza imilimo yabho, umuwikaji bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “wigusha b’o b’aniginigi lub’ub’u lo mvaa.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gudilila milimo yabho bho gwigulambija guitumama chiza, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila umukaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mithali 20:11.

Mithali 23:13.

Yoeli 1:3.

Marko 9:37-37.

KISWAHILI: MCHEZO WA WATOTO VUMBI LA MBWA.

Watoto hucheza michezo yao kwa kutimua vumbi kama mchezo wa mbwa. Watoto hao hutimua vumbi kwa sababu huwa wanachezea mchanga au kitu kingine ukiwemo moto kwa sababu ya utoto wao huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mchezo wa watoto vumbi la mbwa.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale ambao hufanya kazi zao kitoto katika maisha yao. Watu hao hufanya kazi kidogo tu wanaanza kucheza mpaga wanashindwa kuzimaliza kazi zao, kwa sababu ya kujali maongezi yasiyo na faida wakati wa kufanya kazi, maishani mwao. Wao hukosa chakula katika familia zao kwa sababu ya utoto wao wa kushindwa kufanya kazi zao vizuri, maishani mwao.

Watu hao hufanana na watoto waliojali kucheza bila kufanya kazi, kwa sababu nao hujali maongezi wakati wa kazi mpaka wanashindwa kuzimaliza kazi zao, maishani mwao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “mchezo wa watoto vumbi la mbwa.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kujali kazi zao kwa kuzitekeleza kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mali za kutumia vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Mithali 20:11.

Mithali 23:13.

Yoeli 1:3.

Marko 9:37-37.

ENGLISH: CHILDREN’S GAME DOG DUST.

Children play their games by kicking up dust like a game of dogs. These children kick up dust because they always play with sand or something else including fire because of their childhood. That is why people say that, “children’s game dog dust.”

This proverb is paralleled to people who do their works like a child in their lives. These people only work a little, they start playing around and fail to finish their works, because they care about useless conversations while working, in their lives. They lack food in their families because of their childhood of failing to nicely do their works in their lives.

These people resemble the children who cared about playing without working, because they also care about conversations while working until they fail to finish their works, in their lives. That is why people say to them that, “children’s game dog dust.”

This proverb clarifies in people an idea of taking care of their works by carrying them out with great diligence, so that they can obtain wealth to nicely use in their family lives.

Proverbs 20:11.

Proverbs 23:13.

Joel 1:3.

Mark 9:37-37.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.