1392.  LWINZI LONE LOKAMA

Alihoyi munhu uyo olina lwinzi umuchalo ja Jishapu. Umunhu ng’wunuyo, olialutogilwe noyi ulwinzi lokwe lunulo kunguno lo ng’wambilijaga noyi. Aliyo lulu, ulwinzi lunulo lugakama kunguno gagashila aminzi genayo. Hunagwene agayomba giki, “lwinzi lone lokama.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo olimsab’i omajikolo mingi uyo oliadakoyaga, ijo jigashila mpaga wandya guyukoya, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, olinsab’i o majikolo mingi ayo ogatumamilaga bho gugisanya nyadoshi mpaga nose gushila, kunguno ya gugisanya goyi bhuli nimo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agahabhika mpaka wandya guyukoya aha kaya yakwe kunguno ya bhudoshi bhokwe ubho gujisanya isabho jinijo na kujitumilaga sagala, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo lugakama ulwinzi ulo olialutogilwe, kunguno nuweyi jigashila isabho jakwe ijo oliajisanije noyi mpaga uyukoyakoya, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayomba giki, “lwinzi lone lokama.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka gudosela jikolo ulu bhajipandikaga, kugiki bhadule gujilanija jisoga na bhichabho abhahab’i, umuwikaji bhobho.

Kutoka 22:25.

Kutoka 23:6.

Mathayo 5:40.

Mithali 19:17.

Mithali 22:2.

Mithali 22:9.

KISWAHILI: KISIMA CHANGU KIMEKAUKA.

Alikuwepo mtu aliyekuwa na kisima kwenye kijiji cha Kishapu. Mtu huyo, alikuwa anakipenda sana kisima chake hicho kwa sababu kilikuwa kinamsaidia sana maishani mwake. Lakini basi, kisima hicho kilikauka akaanza kuhangaika. Ndiyo maana alisema kwamba, “kisima changu kimekauka.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule aliyekuwa tajiri ambaye alifirisika mpaka akaanza kuhangaika, katika maisha yake. Mtu huyo, alipokuwa tajiri wa mali nyingi, alikuwa akizitumia mali zake hizo kwa majivuno mpaka mwishowe zikaisha, kwa sababu ya kuzitegemea sana mali hizo kwenye kutatua kila tatizo, maishani mwake. Yeye alifirisika mpaka akanza kuhangaika kwenye familia yake, kwa sababu ya majivuno yake ya kutegemea mali zake na kuzitumia vizuri, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule ambaye kisima alichokuwa anakipenda kilikauka, kwa sababu naye aliishiwa mali zake alizokuwa anazitegemea sana mpaka akaanza kuhangaika, maishani mwake. Ndiyo maana alisema kwamba, “kisima changu kimekauka.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha majivuno wanapotajirika, ili waweze kuendana vizuri na wenzao ambao ni maskini, maishani mwao.

Kutoka 22:25.

Kutoka 23:6.

Mathayo 5:40.

Mithali 19:17.

Mithali 22:2.

Mithali 22:9.

 

ENGLISH: MY WELL HAS DRIED UP.

There was a man who had a well in the village of Kishapu. Such man liked his well so much because it supported him a lot in his life. But then, the well dried up until he began to worry. That is why he said that, “my well has dried up.”

This saying is matched to a rich man who lost his wealth until he started to worry, in his life. When this man was rich with a lot of wealth, he used his wealth arrogantly until it finally ran out, because he relied too much on it in solving every difficult in his life. He was broke until he started to worry about his family, because of his pride of relying too much on his wealth in using it.

This man is similar to the one whose well which he liked dried up, because he also ran out of the wealth which he had relied on so much until he started to worry, in his life. That is why he said that, “my well has dried up.”

This saying imparts in people an idea of abandoning pride when they become rich, so that they can fit in well with their poor nobles in their lives.

Exodus 22:25.

Exodus 23:6.

Matthew 5:40.

Proverbs 19:17.

Proverbs 22:2.

Proverbs 22:9.

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.