1388. OISHIDAKAGA ISATA.

Olihoyi munhu uyo osadaga umuchalo ja Masanga. Umunhu ng’wunuyo agaja kubhugota ugayibhulila isata yiniyo bho gung’wila udakitali pye umoosatilaga kunguno ya gugudilila chiza umili gokwe gunuyo. Uweyi agalagulwa mpaga upila wangu kunguno ya guibhulila chiza isata yiniyo ukuli dakitali okwe. Hunagwene abhanhu bhang’wila giki, “oishidakaga isata.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagudililaga chiza umili gokwe bho guguchala kubhugota ulu osadaga umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agasataga wanguha guja kusitali oganomela udakitali umo agusatilaga bho nduhu uguibhisa isata kunguno ya witegeleja bhokwe ubho gugudilila chiza umili gokwe gunuyo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapilaga wangu ulu osataga kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho gwanguha guja kusitali ulu osataga umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agajuibhulila kuli dakitali isata yakwe mpaga upila wangu, kunguno nuweyi aganguhaga guja kusitali ulu osataga ogalagulwa mpaga opila wangu, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “oishidakaga isata.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gwanguha guja kusitali ulu bhasataga, kugiki bhadule gulagulwa na gupila wangu, umuwikaji bhokwe.

Mathayo 8:1-4.

Mathayo 8:28-34.

Mathayo 9:1-2.

Mathayo 9:18-22.

KISWAHILI: AMEUSHITAKI UGONJWA.

Alikuwepo mtu aliyekuwa anaumwa kwenye kijiji cha Masanga. Mtu huyo, alienda hosipitalini kuushitaki ugonjwa huo kwa kumweleza dakitali alivyokuwa anaumwa kwa sababu ya kuujali vizuri mwili wake huo. Yeye alitibiwa mpaka akapona haraka kwa sababu ya kuushitaki vizuri ugonjwa huo kwa dakitali wake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “ameushitaki ugonjwa.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huujali vizuri mwili wake kwa kuupeleka hosipitalini anapoumwa, katika maisha yake. Mtu huyo, huwahi kwenda hosipitalini anapoumwa kwenda kumweleza dakitali anavyoumwa bila ya kuuficha ujonjwa wake kwa sababu ya umakini wake huo wa kuujali vizuri mwili wake. Yeye hupona haraka anapougua kwa sababu ya kuwahi kwenda kutibiwa hosipitalini, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeushitaki ugonjwa kwa dakitali wake mpaka akatibiwa na kupona haraka, kwa sababu naye huwahi kwenda hopitalini kutibiwa na kupona haraka anapoumwa, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “ameushitaki ugonjwa.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuwahi kwenda kutibiwa hositalini wanapoumwa ili waweze kupona haraka, katika maisha yao.

Mathayo 8:1-4.

Mathayo 8:28-34.

Mathayo 9:1-2.

Mathayo 9:18-22.

ENGLISH: HE HAS ACCUSED ILLNESS.

There was a man who was sick in the village of Masanga. He went to the hospital to complain about such disease by telling the doctor how he was sick because he took respectable care of his body. He was treated until he recovered quickly because he had complained about it well to his doctor. That is why people told him that, “he has accused illness.”

This saying is equaled to a person who takes decent care of his body by taking it to the hospital when he is sick, in his life. Such man, when he is sick, goes to the hospital to tell the doctor how he is sick without hiding his illness because of his decent attention enough to take respectable care of his body. He recovers quickly when he gets sick because of attending to the hospital to get treatments in his life.

This man resembles the one who complained about his sickness to his doctor until he was treated and recovered quickly, because he also goes to the hospital to be treated enough to recover quickly when he is sick, in his life. That is why people say to him that, “he has accused illness.”

This saying imparts in people an idea of being careful enough to go to the hospital for treatment when they are sick so that they can recover quickly in their lives.

Matthew 8:1-4.

Matthew 8:28-34.

Matthew 9:1-2.

Matthew 9:18-22.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.