Imbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo witanagwa Limbe. Ulimbe ng’wunuyo oli na nzob’e yakwe iyo witumamilaga mlugendo bho gwidamhila. Giko lulu lushigu lumo bhagiza bhanhu aha ng’wa Limbe abho bhajinjaga myenda bhililagwa b’ujiku, bulomba gulalija hoyi.
Aho lyashiga likanza lya gwingila mu kaya gulala, bhagawilwa gwingila mukaya bhulema bhaligongeja gulala hanze. Bhuwilwa giki jiliho shimba aliyo bhadazunije ugwingila umu kaya.
Aha bhujiku bhokula umo ob’o ub’ona giiti ubhawila ab’iye giki yiyo shimba. Umo wabho uhaya nduhu yeniyo nzob’e ya ng’wa Limbe. Umunhu ng’wenuyo yiza yunsola ishimba yugamulaga. Hii mbuki ya guhaya giki “nzob’e ya ng’wa Limbe.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adazunyaga mihayo ya kukandwa na bhiye iyo idulile gung’wambilija, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agakandagwa na bhiye giki wite ginhu jilebhe, nulu aleke gwita ginhu jilebhe olema kunguyo ya bhuhalali bhokwe bhunubho umukikalile kakwe. Uweyi agapandikaga makoye mingi aha kaya yake kunguno ya bhuhalali bhokwe bhunubho ubho gulema gukandwa na bhiye umuwikaji bhokwe bhunubho.
Umunhu ng’wunuyo alikola nuyo agawilwa aje mukaya kugiki apile guliwa na Shimba ulema mpaka iza yunsola ishimba yiniyo, yugamulaga, kunguno nuweyi agakandagwa na bhiye bho guwilwa mihayo ya gumpija ohalalika, mpaga nowe opandika makoye umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “punda ya Limbe.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guzunya mihayo ya kukandwa na bhichabho kugiki bhadule gubhulanhana chiza ubhupanga bhobho, umuwikaji bhobho bhunubho.
Kumbukumbu la Torati 30: 15-16.
Wafilipi 1:11.
2 Wathesalonike 2:10.
KISWAHILI: PUNDA YA LIMBE.
Chanzo cha msemo huo huangalia mtu aliyeitwa Limbe. Limbe huyo alikuwa na pumba aliyemtumia katika safari zake kama usafiri wake. Hivyo basi siku moja walifika watu waliokuwa wakiuza nguo wakati wa usiku wakaomba kulala hapo kwake.
Ulipofika wakati wa kuingia kulala watu hao waliambiwa waingie ndani ya nyumba, wakakataa wakitaka kulala nje. Waliambiwa kwamba, kuna simba hapo, lakini hawakukubali kuingia ndani.
Usiku ulipoenda sana mmoja wao aliona giza akawaambia wenzake huyo Simba. Mmoja wao alisema, “hapana huyo ni punda ya Limbe.” Simba alifika akamchukua na kumuua mtu huyo. Hicho ndicho kikawa chanzo cha watu kusema “punda ya Limbe.”
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huukataa ushauri wa wenzake unaoweza kumsaidia, katika maisha yake. Mtu huyo, hushauriwa na wenzake juu ya kuacha au kutenda jambo fulani, akakataa kwa sababu ya ubishi wake huo maishani mwake. Yeye hukumbwa na matatizo mengi kwenye familia yake kwa sababu ya ubishi wake huo wa kuukataa ushauri wa wenzake unaoweza kumsaidia, katika maisha yake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyeukataa ushauri wa kuingia ndani ya nyumba ili apone kuliwa na Simba, mpaka mwishowe simba akamuua, kwa sababu naye huukataa ushauri wa wenzake mpaga anakumbwa na matatizo katika familia yake hiyo. Ndiyo maana yeye huuita ushauri huo kuwa ni “Punda ya Limbe.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuupokea ushauri wa wenzao unaoweza kuyaokoa maisha yao, ili waweze kuutunza vizuri uhai wao, maishani mwao.
Kumbukumbu la Torati 30: 15-16.
Wafilipi 1:11.
2 Wathesalonike 2:10.
ENGLISH: THE DONKEY OF LIMBE.
The origin of this saying is about a man named Limbe. Limbe had a donkey that he used as his transportation on his travels. So one day, people who were selling clothes came at night and asked to sleep at his place.
When it was time to go to sleep, the people were told to go inside the house, but they refused, wanting to sleep outside. They were told that there was a lion there, but they refused to go inside.
When the night was very late, one of them saw the darkness and told his companions that the lion was there. One of them said, “No, that is Limbe’s donkey.” The lion came there that killed him. That is why people started to say that “The Donkey of Limbe.”
This saying is compared to a man who rejects advice of his companions that can help him in his life. Such person is advised by his companions to stop misbehaving or doing something, but he refuses because of his disagreement in his life. He faces sundry hitches in his family because of his stubbornness of rejecting the advice of his nobles that can help him, in his life.
This person is similar to the one who rejected the advice of entering the house to save himself from being eaten by a Lion, until finally the lion killed him, because he also rejects the advice of his fellows to the point of facing problems in his life. That is why he calls that advice “The Donkey of Limbe.”
This saying imparts in people an idea of receiving decent advice of their nobles that can save their lives, so that they can take respectable care of their lives.
Deuteronomy 30: 15-16.
Philippians 1:11.
2 Thessalonians 2:10.


