1365. B’UKAGI WANGU MUGULIWA MASUMULE.

Aho kale bhalihoyi bhanhu abho bhatumama nimo umuchalo ja bhusiya. Abhanhu bhenabho bhali bhalemejiwe ugwigasha ulubhaligutumama unimo guniyo kunguno bhalibhadakililwe gugumala wangu unimo gunuyo. Ulu munhu ubhonwa na bhatale bha nimo gunuyo wigashaga ahikanza lyagugutumama unimo gunuyo oliyagwa masumule. Hunagwene abhatumami bhenabho bhikomelejaga gutumama nimo bho guyomba giki, “b’ukagi wangu muguliwa masumule.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo aganyenyekaga ugutumama imilimo ya ng’wigunguli lyakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga unyenyeka ugujiika abhanhu bha ng’wigunguli lyakwe, nulu ugubhambilija abhiye abho bhapandikaga makoye, kunguno ya bhujidadilila bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga makoye gagutulijiwa bhuli makanza aha kaya yakwe kunguno ya bhunyenyeku bhokwe bhunubho ubhoguleka gujutumama milimo ya ng’wigunguli lyakwe, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabho bhigashaga ahikanza lya gutumama milimo yabho, kunguno nuweyi aganyenyekaga ugutumama imilimo iyang’wigunguli lyakwe mpaga otulijiwa ni ligunguli lyakwe linilo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “b’ukagi wangu muguliwa masumule.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka bhunyenyeku bho gutumama milimo ya ng’wigunguli lyabho, kugiki bhadule gwiyambilija gutumama milimo ya gubhenhela matwajo gagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

1 Wakorintho 16:16.

Wakolosai 1:10.

KISWAHILI: AMUKENI HARAKA MTATOZWA FAINI.

Hapo zamani walikuwepo watu waliokuwa wakifanya kazi kwenye kijiji cha Busiya. Watu hao walikuwa wamekatazwa kukaa wakati wa kufanya kazi hiyo, kwa sababu walitakiwa kuimaliza mapema kazi hiyo. Mtu aliyeonekana amekaa kabla ya kuimaliza kazi hiyo, alitozwa faini. Ndiyo maana wafanyakazi hao walikuwa wakihimizana kuendelea kuitekeleza kazi hiyo kwa kusema kwamba, “amukeni haraka mtatozwa faini.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hukwepa kufanya kazi kwenye kijiji chake katika maisha yake. Mtu huyo, huwa anakwepa kwenda kwenye matukio mbalimbali yakiwemo yale ya kuzika wafu au kuwasaidia watu waliokumbwa na matatizo kwenye kijiji chake, kwa sababu ya kutokujali kwake, maishani mwake. Yeye hukumbwa na matatizo ya kutengwa na wanakijiji hao mara kwa mara kwenye familia yake, kwa sababu ya utoro wake huo wa kuacha kujiunga na wenzake katika kutatua matatizo ya kijijini mwake wakiwa pamoja na wanzake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na wale waliokuwa wakitegea kufanya kazi kwa kukaa kabla ya kumaliza kazi yao, kwa sababu naye hukwepa kuhudhulia matukio ya wanakijiji wenzake katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amukeni haraka mtatozwa faini.”

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha ukwepaji wa kwenda kufanya kazi za vijijini mwao, ili waweze kushirikiana vizuri katika kufanya kazi za kuwapatia mafanikio mengi, maishani mwao.

1 Wakorintho 16:16.

Wakolosai 1:10.

ENGLISH: WAKE UP QUICKLY OR YOU WILL BE FINED.

In the past, there were people working in the village of Busiya. These people were forbidden to sit while doing the work, because they were required to finish the work early. Anyone who was seen sitting before finishing the work was fined. That is why the workers used to encourage each other to continue doing the work by saying, “Wake up quickly or you will be fined.”

This proverb is compared to a person who avoids working in his village in his life. That person avoids going to various events including those to bury the dead or help people who have problems in his village, because of his carelessness, in his life. He suffers from the problems of being separated from the villagers from time to time in his family, because of his absence of joining his colleagues in solving the problems of his village while being with his colleagues, in his life.

This person is like those who used to stay up late to work because they avoid attending to the events of their fellow villagers in their lives. That is why people tell them, “wake up quickly, you will be fined.”

This proverb teaches people to stop avoiding going to work in their villages, so that they can cooperate well in doing the work that will bring them much success in their lives.

1Corinthians 16:16.

Colosians 1:10.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.