Imbuki ya kahayile kenako ilolile kikalile ka mhuli. Imhuli yiniyo ili ndimu nhale iyo ili na makanji kunguno ya bhukali bhoyo. Iyoyi igikalaga ing’wenije duhu na amino gayo gali hanze guti giki ili na mholo ya wiza aliyo igasayaga noyi umukikalile kayo. Hunagwene abhanhu bhagihayaga giki, “mang’weng’ula mhuli.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga ang’wenije mino hanze giti munhu mfula alisegasega aliyo ali ndaki noyi umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga wisegeleja bho golecha mino gakwe guti ntengeke noyi aliyo umunholo yakwe alinchilu noyi kunguno ya nhungwa jakwe ija gwita mihayo ya bhubhi yinijo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga widuma na bhanhu bha muchalo jakwe kunguno ya bhudaki bhokwe bhunubho ubho agabhubhisaga bho golecha mino hanze, umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni mhuli iyo igikalaga ing’wenije mino hanze aliyo igasayaga noyi, kunguno nuweyi agikalaga ang’wenije mino hanze guti munhu mfula agusegaga aliyo ali ndaki noyi umunholo yakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “mang’weng’ula mhuli.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guleka gwiyolecha guti bhatengeke aliyo bhali bhadaki umunholo jabho, kugiki bhadule gwikala chiza umukaya jabho.
2 Timotheo 3:3.
Mathayo 7:15.
KISWAHILI: TABASAMU LA TEMBO.
Chanzo cha msemo huo huangalia maisha ya tembo. Tembo huyo ni myama poli ambaye ni mkubwa na mweye hali ya kutisha kwa sababu ya ukali wake. Yeye huonesha meno yake nje kama anatabasamu la moyo mweupe wa furaha wakati ana hasira kali sana. Ndiyo maana watu huongea juu yake kwa kusema, “tabasabu la tembo.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huonesha meno yake kwa nje kama kwamba ni mtu mwema kwa kucheka wakati ni mwenye hasira kali, katika maisha yake. Mtu huyo, hujichekelesha kwa kuonesha meno yake nje ili kujionesha kama ni mwema wakati ana hasira kali ndani yake kwa sababu ya matendo yake kuwa maovu, maishani mwake. Yeye hugombana mara kwa mara na watu wa kwenye kijiji chake kwa sababu ya hasira yake hiyo anayoificha kwa kuonesha meno nje kama mtu mwema, katika maisha yake hayo.
Mtu huyo, hufanana na yule tembo aishiye kwa kuonesha meno yake nje wakati ana hasira kali sana maishani mwake, kwa sababu naye huonesha meno nje kama ni mwema wakati ni mwenye hasira kali, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita jila la “tabasamu la tembo.”
Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuacha tabia ya kujifanya kuwa wema wakati ni wakatili mioyoni mwao, ili waweze kuishi vizuri kwenye familia zao.
2 Timotheo 3:3.
Mathayo 7:15.
ENGLISH: THE ELEPHANT’S SMILE.
The basis of this saying looks at a life of an elephant. The elephant is a large and fearsome creature because of its fierceness. It shows its teeth as if it is smiling with a happy heart while it is a so angry animal. That is why people talk about it by considering it as, “the elephant’s smile.”
This saying is paralleled to a man who shows his teeth as if he is a blameless one by laughing while he is a so angry one in his life. This person laughs by showing his teeth as if he a kind one while he has an angry heart inside because of his wicked actions in his life. He often quarrels with people who stay in his village because of his anger which he hides by showing his teeth as a respectable person in his life.
This person is like an elephant that showed teeth while it is a so angry animal in life because he also shows his teeth as if he is a kind one while he is a so heated one in his life. That is why people call him “the elephant’s smile.”
This saying teaches people about being so cautious enough to stop pretending to be kind while they are cruel in their hearts, so that they can live well in their families.
2 Timothy 3:3.
Matthew 7:15.
