Aho kale bhalihoyi bhanhu abho bhayugulaga mandege bhagaponya amagongote gago. Munhu umo agalibhona iligongote ulipelela alihaya giki lilina mandege kunguno oliotubha noyi. Aho olidima umana igiki gashinaga lyasaga ligongote duhu uliponya. Hunagwene agayomba giki, “amandege gashila lyasaga ligongote duhu.”
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo olileka ililange lya nhungwa jakwe ijawiza ijo olinajo ikale, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo olileka ililange lya gubhambilija chiza abhanhu abho bhalina makoye, ubhiza ng’wimi nholo, na ndalahija obhiye kunguno ya gwilunga mu magele ga bhang’wi bha walwa na bhabehi bha njemu, umuwikaji bhokwe. Uweyi agidumaga na bhanwani bhakwe aha kaya yakwe, kunguno ya gulileka ililange lyakwe ilyawiza linilo, umukikalile kakwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga niligongote ilo gamala guyugulwa amandege galyo, kunguno nuweyi alileka iliange lyakwe ilya gwita mihayo ya wiza wandya gwita mihayo ya bhubhi, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “amandege gashila lyasaga ligongote duhu.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleta gwilunga mumagele ga bhanhu abho bhagitaja mihayo ya bhubhi, bho gulidimila chiza ililange lyabho ilyawiza, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Mithali 3:14.
Mithali 14:4.
Mithali 14:23.
KISWAHILI: MAHINDI YALISHAISHA LIKABAKIA GUNZI TU.
Hapo zamani walikuwepo watu waliokuwa wanapukuchua mahindi na kuyatupa magunzi yake. Mtu mmoja aliliona gunzi mojawapo akalikimbilia akifikiri kwamba lina mahindi kwa sababu alikuwa ameshikwa na njaa sana. Alipolishika aligundua kwamba kumbe lilikuwa limebakia gunzi tu akalitupa. Ndiyo maana alisema kwamba, “mahindi yalishaisha likabakia gunzi tu.”
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule aliyeyaacha malezi mema aliyokuwa nayo hapo zamani, katika maisha yake. Mtu huyo, aliyaacha malezi yake mema ya kuwasaidia watu vizuri, akawa mchoyo na mwenye dharau kwa wenzake kwa sababu ya kujiunga na makundi ya walevi na wavuta bhangi, maishani mwake. Yeye hukosana na marafiki zake katika familia yake kwa sababu ya kuiacha tabia yake njema aliyokuwa nayo mwanzoni, akaiga tabia ya kutenda maovu, katika maisha yake.
Mtu huyo hufanana na lile gunzi liliishiwa mahindi kwa kupukuchuliwa, kwa sababu naye ameiacha tabia yake njema ya kutenda mema kwa kuiga matendo maovu, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mahindi yalishaisha likabakia gunzi tu.”
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha kuiga matendo maovu kwa kuyaishi vizuri malezi mema, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.
Mithali 3:14.
Mithali 14:4.
Mithali 14:23.

ENGLISH: THE MAIZE RAN OUT ONLY HUSK REMAINED.
In the past, there were people who were shelling maize and throwing away their husks. One man saw one of the husks and ran to it thinking that it contained maize because he was so hungry. When he caught it, he discovered that it was actually just a husk and threw it away. That is why he said, “the maize ran out only husk remained.”
This proverb is matched to an individual who left respectable upbringing which he had in his past life. Such person left his decent nurture of assisting people well, became greedy and contemptuous of his nobles because of joining groups of drunkards and drug addicts in his life. He is at odds with his friends in his family because of leaving his upright personality that he had at first, and imitated patterns of doing evil deeds in his life.
This individual resembles the husk that ran out of maize by being hulled, because he also has abandoned his decent custom of doing decent deeds by imitating evil deeds in his life. That is why people say to him that, “the maize ran out only husk remained.”
This proverb teaches people about stopping imitating evil deeds by living a respectable nurture, so that they can nicely rear their family members in their lives.
Proverbs 3:14.
Proverbs 14:4.
Proverbs 14:23.