1318. NZALA YA MHIYA NDALO.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile bhanhu abho bhali na numba ja gulala bhageni. Abhanhu bhenabho bhajizenga inumba jinijo mumaboma kunguno umunumo bhagajaga bhageni bhingi abho bhagacholaga numba ya gulala. Abhageni bhenabho bhagafunyaga hela na bhalala umunumba jinijo, kunguno jilija gulipila bhuli chumba.

Kuyiniyo lulu, abhanikili numba jinijo bhagayimalaga inzala ya gugayiwa mhiya ulu bhabokela ihela jinijo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “nzala ya mhiya ndalo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina bhugagaja bho gutumama milimo mingi iyo igang’wenhelaga hela, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agajitumilaga ihela ijo agajipandikaga bho kulima migunda mitale, guzengo manumba ga gung’wenhela hela, na kulima mabonde ga jiliwa ja mbika ningi ijo jiganpandikilaga hela ng’wingi kunguno ya bhugagaja bhokwe bhunubho umumiganiko gakwe. Uweyi apandikaga hela ningi noyi ijo jigambilijaga uguibheja chiza ikaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nabho bhali na numba ja gulala bhageni ijo jabhenhelaga mahela mingi, kunguno nuweyi alina bhugagaja bho gutumama milimo mingi iyo iganpandikalaga mahela mingi, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “nzala ya mhiya ndalo.”

Akahahile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhugagaja bho gwigulambija gutumama milimo mingi iyo idulile gubhenhela hela ya gutumamila umukaya jabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhokwe.

Mithali 10:15.

Ufunuo 3:17.

KISWAHILI: NJAA YA PESA MALAZI.

Chanzo cha msemo huo huongelea watu wale ambao wana nyumba za kulala wageni. Watu hao, walizijenga nyumba zao hizo mijini kwa sababu humo kuna wageni wengi ambao hutafuta nyumba za kulala wageni.

Wageni hao hutoa pesa ndipo wanapewa chumba, kwa sababu kila chumba hulipiwa na yule anayetaka kulala. Kwa hiyo basi, wenye nyumba hizo huimaliza nja ya kukosa pesa wanapozipokea pesa hizo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “njaa ya pesa malazi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana vitega uchumi vingi vya kumpatia pesa, katika maisha yake. Mtu huyo, ana ubunifu wa kuzitumia pesa katika kujiwekea vitega uchumi kama vile kulima mashamba makubwa, kujenga majumba ya kulala wageni, kulima bustani zenye vyakula vya aina mbalimbali, kwa sababu ya ubunifu wake huo katika mawazo yake. Yeye hupata pesa nyingi sana ambazo humsaidia katika kuiendeleza vizuri familia yake, maishani mwake.

Mtu huyo hufanana na wale waliokuwa na numba mijini ambazo ziliwaletea pesa nyingi, kwa sababu naye huutumia ubunifu wake huo katika kutengeneza vitega uchumi vingi ambavyo humletea pesa nyingi, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “njaa ya pesa malazi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na ubunifu wa kujibidisha kuweka vitega uchumi vingi ambavyo zitawapatia pesa za kutumia katika familia zao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao hizo, maishani mwao.

Mithali 10:15.

Ufunuo 3:17.

ENGLISH: HUNGER FOR MONEY ACCOMMODATION.

The origin of this saying refers to people who have guest houses. These people built their houses in cities because there are various visitors who search for lodging.

These visitors give a lot of money to them because each room is paid for by the person who wants to sleep in it. Therefore, the owners of these houses satisfy their hunger for money when they receive those money. That is why people say, “Hunger for money accommodation.”

This saying is equaled to a person who has various investments which provide him with money in his life. This person is creative enough to make use of money for starting new investments such as cultivating large fields, building guest houses, growing gardens with various types of food crops, because of his creativity in his thoughts. He earns a lot of money that helps him in developing his family well in life.

This person is like those who had houses in the cities which brought them a lot of money, because he also uses his creativity for making several investments which bring him a lot of money in his life. That is why people say to him that, “Hunger for money accommodation.”

This saying imparts in people an idea of being creative enough to put in a lot of investments that will give them money for spending on their families, so that they can progress their families well in their lives.

Proverbs 10:15.

Revelation 3:17.

 

bedroom-374982_1280

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.