1316. ISATA NGESE YA MU MILI.

Ingese gali maswa mingi ayo gali mungunda go ng’wa munhu. Amaswa genayo gagajilemeja ijiliwa ugupya kunguno ya kujimaja aminzi. Ung’winikili ngunda gunuyo agagudilila ungunda gokwe bho guilimila ingese yiniyo kunguno igajizonjaga ijiliwa gitumo gugasongelaga umili go ng’wa munhu uyo alisata. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “isata ngese ya mu muli.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagudililaga chiza umu mili gokwe ulu alisata, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, aganguhaga kuja kusitali ulu alisata ogaping’wa na gwinhiwa bhugota bho gudula guipija isata yakwe yiniyo, kunguno ya witegeleja bho gugudilila chiza umili gokwe gunuyo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapilaga wangu ulu osata kunguno ya gugudilila chiza chiniko umili gokwe, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agagudilila chiza ungunda gokwe bho guilimila ingese mpaga upandika jiliwa aha kaya yakwe, kunguno nuweyi agagudilila chiza umili gokwe ulu alisata bho guja kusitali ogapandika bhugota bho gudula gumpija wangu, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “isata ngese ya mu muli.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guidilila chiza imimili yabho ulu bhalisata, kugiki bhadule gupila wangu na gwikala bho bhuyegi umukaya jabho.

Marko 10: 46-49

KISWAHILI: UGONJWA PALIZI YA MWILI.

Palizi ni uwepo wa majani mengi ndani ya shamba la mtu. Majani hayo huyazuia mazao kuzaa kwa sababu ya kuyamalizia maji. Mwenye shamba hilo hujitahidi huyapalilia mazao yake kwa kuyakata majani hayo kwa sababu yenyewe huyasonga mazao yake kama vile ugonjwa unavyoukosesha raha mwili mwa mtu anayeumwa. Ndiyo maana watu husema kwamba, “ugojwa palizi ya mwili.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huujali vizuri mwili wake anapougua, katika maisha yake. Mtu huyo, huwahi kwenda hospitalini kwenda kupata vipimo na dawa za kuweza kumponyesha haraka, kwa sababu ya umakini wake huo wa kuujali vizuri mwili wake, maishani mwake. Yeye hupona haraka anapougua kwa sababu ya kuujali vizuri hivyo mwili wake huo kwa kuuwahisha hospitalini kila anapougua, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyelijali vizuri shamba lake kwa kulipalilia palizi mpaka akapata mazao kwenye familia yake, kwa sababu naye huujali vizuri mwili wake kwa kuuwahisha hospalini anapougua kwenda kupata vipimo na dawa za kumsaidia kupona haraka, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “ugojwa palizi ya mwili.”

Msemo huo, hufundisna watu juu ya kuwa na umakini wa kuijali miili yao kwa kuiwahisha hopitalini kila wanapougua, ili waweze kupona haraka na kuishi kwa furaha maishani mwao.

Marko 10: 46-49.

 

ENGLISH: SICKNESS A WEED OF THE BODY.

Weed is an unwanted leave in a person’s field. This leave prevents crops from producing yields because they drain water. The owner of the field strives to weed his crops by cutting these leaves because they themselves suffocate his crops just as a disease makes the body of a sick person uncomfortable. That is why people say, “Sickness a weed of the body.”

This saying is matched to a person who takes good care of his body when he is sick in life. This person sometimes goes to the hospital for getting medicines which can heal him quickly, because of his courtesy for taking good care of his body in his life. He recovers quickly when he is sick because he takes good care of his body by going to the hospital every time when he is sick in his life.

This person is like the one who took good care of his field by weeding it until it yielded crops for his family, because he also takes good care of his body by going to the hospital when he is sick for geting medicines which can help him to recover quickly in his life. That is why he says that, “Sickness a weed of the body.”

This saying teaches people to be careful enough to take care of their bodies by going to the hospital whenever they are sick, so that they can recover quickly and live happily in their lives.

Mark 10: 46-49.

 

working-4465967_1280

gardening-2518377_1280

sadness-1783794_1280

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.