Imbuki ya kahayile kenako ilolile kalile ka jiliwa ka bhanhu. Abhanhu abho bhalilya jiliwa bhagalangula tamu na bhamila ijiliwa ijo bhalijilya jinijo kunguno bhadadulile ugumila ijiliwa ukunu bhagundamile. Hunagwene abhanhu ulubhalilya bhagikomelejaga bho guyomba giki, “dubhulangulile.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajitumilaga chiza ijikolo jakwe giti numo jidakililwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajitilaga bhukengeji bho gujidebha chiza pye ikolo jakwe na wandya ugujitumamila kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga matwajo mingi aha kaya yakwe kunguno ya kujitumamila chiza ijikolo jakwe jinijo, umumilimo yakwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nabho bhalangulaga na bhajimila ijiliwa ijo bhajilyaga jinijo, kunguno nuweyi agajitumamilaga ijikolo jakwe chiza kitumo jidakililwe ugutumamilwa, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agabhawilaga abhiye giki, “dubhulangulile.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujitila bhukengeji bho gujidebha chiza ijikolo jabho na bhandye ugujitumamila, kugiki jidule gubhambilija chiza ugujilanhana ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Marko 14:22-26.
Wakolosai 3:1.
Mwanzo 26:30.
Mwanzo 19:3.
Luka 5:29.
KISWAHILI: TUUINULIE VICHWA.
Chanzo cha msemo huo, huangalia ulaji wa chakula wa watu. Watu wanapokula chakula huinua vichwa vyao ndipo wanameza kwa sababu haiwezekani kumeza chakula hicho wakiwa wameinama. Ndiyo maana watu wanapokula huhimizana kwa kusema kwamba, “tuuinulie vichwa.”
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvitumia vizuri vitu vyake kama vinavyotakiwa kutumiwa, katika maisha yake. Mtu huyo, huvifanyia utafiti wa kutosha kuvielewa vizuri vitu vyake hivyo ndipo anaanza kuvitumia kwa sababu ya umakini wake huo, maishani mwake. Yeye hupata mafanikio mengi katika familia yake kwa sababu ya kuvitumia vizuri vitu vyake hivyo, katika maisha yake.
Mtu huyo, hufanana na wale waliokuwa wakiviinue vichwa vyao ndipo wanavimeza vyakula walivyokuwa wanakula, kwa sababu naye huvitumia vitu vyake vizuri kama vinavyotakiwa kutumiwa, maishani mwake. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “tuuinulie vichwa.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuvifanyia vitu vyao utafiti wa kutosha kuvielewa vizuri, ndipo waanze kuvitumia ili viweze kuwasaidia vizuri katika kuzitunza familia zao, maishani mwao.
Marko 14:22-26.
Wakolosai 3:1.
Mwanzo 26:30.
Mwanzo 19:3.
Luka 5:29.

ENGLISH: LET US LIFT UP OUR HEADS FOR IT.
The source of this saying stares at people’s food intake. When people eat food raise their head for swallowing because it is impossible to swallow such food while bending down. That is why when they eat, encourage each other by saying, “Let us lift up our heads for it.”
This saying is paralleled to a man who uses his belongings well as they are supposed to be used, in his life. Such person does good research enough to understand his possessions well and then he starts using them nicely because of his thoughtfulness, in his life. He gets a lot of success in his family because of using his properties well, in his life.
This person is similar to those who used to raise their heads while swallowing the food which they ate, because he also courteously uses his possessions as they should be used, in his life. That is why he tells people that, “Let us lift up our heads for it.”
This saying instills in people an idea of being careful to enough do research on their possessions for understanding them well, then they start using them so that these possessions can help them well in taking care of their families in their lives.
Mark 14:22-26.
Colossians 3:1.
Genesis 26:30.
Genesis 19:3.
Luke 5:29.