Olihoyi munhu uyo wikalaga muchalo jilebhe. Umunhu ng’wunuyo, oipandaga isii bho nguvu noyi kunguno ya gulya jiliwa mpaga wiguta noyi. Uweyi wiganikaga giki adalacha na gujikwa umugati ya sii iyo ayipandaga yiniyo, kunguno ya lwiguto lokwe lunulo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “mpandage aliyo agugulya.”
Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu nsabhi uyo agiganikaga giki adalacha, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajisanyaga isabho jakwe bho gwita mihayo iyo atogilwe weyi umusii ng’wenumu, kunguno ya bhudoshi bho gwiganika giki isabho jigung’wingija pye amakoye mpaka nu lufu, umuwikaji bhokwe, bhunubho. Uweyi agadumaga uguilela chiza ikaya yakwe kunguno ya gwisanya sabho jakwe bho gwita mihayo iyo atogilwe weyi, umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agiguta jiliwa uipanda isii bho nguzu, kunguno nuweyi agajisanyaga isabho jakwe bho gwita mihayo iyo atogilwe weyi umusii guti giki adalacha, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “mpandage aliyo agugulya.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwita mihayo ya wiza umusi hayo ingelelo yabho idinashiga, kunguno bhuli ng’wene alina ngelelo yakwe, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umubhulamu bhobho bhunubho.
Hesabu 16:29-30.
Ayubu 7:21.
Ayubu 20:11.
KISWAHILI: MKANYAGE LAKINI ATAKULA.
Alikuwepo mtu aliyekuwa akiishi kwenye kijiji fulani. Mtu huyo, alikuwa akiikanyaga ardhi kwa nguvu sana kwa sababu ya kula chakula mpaka akashiba sana. Yeye alikuwa akifikiri kwamba hatakufa na kuzikwa ndani ya ardhi hiyo aliyokuwa akiikanyaga kwa sababu ya kushiba kwake chakula alichokula. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “mkanyage lakini atakula.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu tajiri ambaye hufikiria kwamba, hatakufa, katika maisha yake. Mtu huyo, huutegemea utajiri wa wali zake katika kutatua matatizo yake yote kwa kufanya atakalo yeye kwa sababu ya majivuno ya kuufikiria utajiri wake kwamba utamwondolea matatizo yote hata kumzuia kufa, maishani mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake kwa sababu ya kutegemea mali zake hizo kwa kuzifikiria kama mtatuzi wa matatizo yake yote, katika maisha yake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyeshiba chakula mpaka akaanza kuikanyaga ardhi kwa mguvu, kwa sababu naye huutegemea utajiri wa mali zake mpaka anafanya anachotaka hapa duniani kama kwamba, hatakufa, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mkanyage lakini atakula.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kutenda matendo mema hapa duniani kabla ya kufika mwisho wao, kwa sababu kila mmoja ana mwisho wake, ili waweze kuzilea vyema familia zao, wakati wa uhai wao wote.
Hesabu 16:29-30.
Ayubu 7:21.
Ayubu 20:11.
ENGLISH: TREAD IT BUT IT WILL EAT YOU.
There was a man who lived in a certain village. Such man was treading the ground very hard because of eating food until he was very full. He was thinking that he will not die and be buried in the ground which he was treading. That is why people told him that, “Tread it but it will eat you.”
This saying is equaled to a rich man who thinks that he will not die in his life. Such person depends on the wealth of his parents in solving all his problems by doing what he wants because of thinking that his wealth will remove all problems and even prevent him from dying in his life. He fails to raise his family well because of relying on his possessions by thinking of them as the solution to all his problems, in his life.
This person resembles the one who ate food until he began to tread the ground with strength, because he also depends on the wealth of his possessions until he does what he wants in this world as if he will not die. That is why people tell him that, “Tread it but it will eat you.”
This saying imparts in people an idea about doing good deeds on this world before reaching their end, because everyone has his/her end, so that they can raise their families well, during their whole lives.
Numbers 16:29-30.
Job 7:21.
Job 20:11.
