Ikalagu yiniyo, ililolile lukubha. Ulukubha lunulo jili ginhu ja makanji ijo jigikalaga ng’wigulya. Uloyi ulagatemaga ginhu ja mbika ningi, ijo lugajilolelaga bho kule na guja lwisongile hoyi. Hunagwene abhanhu bhagalyutanaga giki, “ntemi o liso – lukubha.”
Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayipangaga chiza imilimo yakwe haho atali uguitumama. Umunhu ng’wunuyo, agitaga bhukengeji bho gugudebha chiza bhuli nimo kunguno ya gwiinha ikanza lya gujidebha isolobho ja nimo gunuyo. Uweyi agapandikaga solobho ningi umubhutumami bhokwe bhunubho kunguno ya gwuitila bhukengeji bhutale imilimo yakwe yiniyo, haho atali uguitumama, umuwikaji bhokwe.
Ikalagu yiniyo, igikolaga nu lukubha ulo lugalolelaga bho gufumila kule uko luligatema, kunguno nuweyi agayilolaga bho guyitila bhukengeji bhutale imilimo yakwe, haho atali uguyandya uguitumama. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “ntemi o liso – lukubha.”
Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya guyitila bhukengeji bhutale imilimo yabho, haho bhatali uguitumama, kugiki bhadule guitumama imilimo iyo ilina solobo nhale, umuwikaji bhobho.
Yona 3:4.
Mathayo 16:1-3.
Yohana 14:27-31.
Mathayo 17:22-23.
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.
MFALME WA JICHO – RADI.
Kitendawili hicho, huangalia Radi. Radi hiyo, ni kitu cha kutisha kiishicho juu. Yenyewe hupiga vitu vya aina mbali mbali, ambacho hukiona kutokea mbali na kwenda kukipiga kule kiliko. Ndiyo maana watu hukiita, “mfalme wa jicho – Radi.”
Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyapanga vizuri majukumu yake kabla ya kuyatekeleza. Mtu huyo, hufanya utafiti wa kumuwezesha kuifahamu vizuri kila kazi kwa sababu ya kujipatia muda wa kuzifahamu faida za kazi hiyo. Yeye hupata faida ya kuwa na mali nyingi, katika utekelezaji wa majukumu yake hayo, kwa sababu ya kuzifanyia utafiti mkubwa kazi zake kabla ya kuanza kuzitekeleza, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na ile Radi ionayo kutokea mbali sehemu ile itakayoipiga, kwa sababu naye huziangalia kazi zake kwa kuzifanyia utafiti, kabla ya kuanza kuzitekeleza. Ndiyo maana watu humuita kwamba ni “Mfalme wa jicho – Radi.”
Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuzifanyia utafiti wa kina kazi zao, kabla ya kuanza kuzitekeleza, ili waweze kupata faida kubwa, maishani mwao.
Yona 3:4.
Mathayo 16:1-3.
Yohana 14:27-31.
Mathayo 17:22-23.
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE- LET IT COME.
THE KING OF THE EYE – THE LIGHTING.
The above riddle speaks about the lighting. This lightning a horrible thing that occurs during the rain time. It strikes a variety of objects, which one can see when it is coming from afar while to strike it. That is why people call it “the king of the eye –the Lightning.”
This riddle is equated to the person who carefully arranges his duties before performing them. This person conducts good research enough to enable him or her become better acquainted with each job because he or she has time to understand the benefits of such job. He gets benefits of having a lot of wealth fulfilling his/her responsibilities, because of doing a lot of research on each work before doing it, in his life.
This person is like the Lighting that sees in a distance the part that is going to hit, because he also looks at his work by doing research, before starting to implement them. That is why people call him “the King of the eye – the Lightning.”
This riddle teaches people on how to do a thorough study of their works, before they start implementing them, so that they can get many benefits from their lives.
Jonah 3: 4.
Matthew 16: 1-3.
John 14: 27-31.
Matthew 17: 22-23.