924. LUCHIBHA MAPANDA.

Amapanda jili njila ja gubhitila bhanhu nulu mitugo. Olihoyi munhu uyo alina nguzu za gudula gubhalemeja ugubhita abhanishi bhakwe. Umunhu ng’wunuyo, ajijichib’aga inzila ijo bhabhitilaga abhanishi bhakwe bhose bhab’ize bhana ndimu bhagudima mitugo jakwe, nulu b’ibhi bha jikolo ja aha kaya yakwe. Hunagwene abhanbu bhagang’witana giki, “luchib’a mapanda.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alintongeji ng’wiza o bhanhu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alina nguzu ja gung’wambilija ugubhatongela chiza abhanhu bhakwe bho gubhahangija abhanishi bhabho ugujisola isabho jabho, nulu ugujikenagula. Uweyi agabhalang’hanaga abhanhu bhakwe bho gubhatongela chiza, kunguno ya nguzu jakwe na masala miza ayo alinago, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo olina nguzu ja gujijicha injia ijo bhajibhitilaga abhanishi bhakwe, kunguno nuweyi alina nguzu ja gubhatongela na gubhalang’hana chiza abhanhu bhakwe. Uweyi agabhalemeja abhanishi bhakwe ugushiga ukubhanhu bhakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wiganaga giki, “luchibha mapanda.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na masala miza ga gubhatongela chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwikala mhola abhanhu bhenabho kihamo ni sabho jabho, umuwikaji bhobho.

Kutoka 4:1-8.

1Wakorintho 15:56-58.

Kutoka 14:10-31.

Mathayo 8:23-27.

Wafilipi 2:5-11.

 

KISWAHILI: MZIBA NJIA.

Njia ni sehemu za kupitia watu au mifugo. Alikuwepo mtu aliyekuwa na nguvu za kuwazuia kupita maadui zake. Mtu huyo, alikuwa na uwezo wa kuziziba njia zile walizopitia maadui hao wote, wawe watu, au wanyama wakali waliovamia mifugo ya kwenye familia yake. Ndiyo maana watu walimuita yeye kuwa ni “mziba njia.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni kiongozi mzuri wa watu. Mtu huyo, ana nguvu na akili za kuwaongoza vyema watu wake kwa kuwazuia maadui wanaotaka kuharibu mali za watu wake. Yeye huwalinda vizuri watu wake hao kwa kuwaongoza vyema, kwa sababu ya nguvu na akili alizo nazo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeziziba njia zile walizozitumia maadui zake kuwavamia, kwa sababu naye ana nguvu za kuwaongoza na kuwalinda vizuri watu wake. Yeye huwazuia maadui kufika kwa watu wake. Ndiyo maana watu humuita kwamba ni “mziba njia.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na akili njema za kuwawezesha kuwaongoza watu wao vizuri, ili watu hao waweze kuishi kwa usalama, na mali zao ziwe salama, maishani mwao.

Kutoka 4:1-8.

1Wakorintho 15:56-58.

Kutoka 14:10-31.

Mathayo 8:23-27.

Wafilipi 2:5-11.

car-

ENGLISH: ROADS’ BLOCKER.

Paths are places where people or livestock pass. There was a man who had the power to stop enemies from passing in his Area. He was able to block the paths that all those enemies had passed, be they humans, or wild beasts that had invaded his family’s livestock. That is why people called him that he is a “roads’ blocker.”

This saying is likened to a man who is a good leader of the people. He has the power and intelligence to lead his people in the right direction by stopping enemies who want to destroy properties of his people. He well protects his people by leading them in the right direction, because of the power and intelligence which he has in his life.

This man is like the one who blocked the ways in which his enemies used to attack them, because he too has the power to lead and protect his people. He prevents enemies from reaching his people. That is why people call him that he is a “roads’ blocker.”

This saying instils in people an idea of having good minds enough to enable them lead their people well, so that they can live safely enough to protect their properties, in their lives.

Exodus 4: 1-8.

1 Corinthians 15: 56-58.

Exodus 14: 10-31.

Matthew 8: 23-27.

Philippians 2: 5-11.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.