920. IYI WIB´ONA NG´WA NG´WIYO ILOLAGE NUKO MILI GOKO.

Ulusumo lunulo, lulolile mihayo iyo igigelega ukubhanhu. Olihoyi munhu uyo, oliadayidililaga imihayo yiniyo iyo iyakubhiye kunguno ya bhujidalonja bhokwe. Lushigu lumo, agagayiwa ijiliwa ija gulya aha ng’wakwe. Uja gujulanda ijiliwa jinijo aha bhuzenganwa. Abhahabhuzenganwa bhenabho, bhagang’wambilija bho gung’wilaga giki, “iyi wib’ona ng’wa ng’wiyo ilolage nuko mili goko.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhasekaga abhiye abho bhali na makoye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alina bhudoshi bho gubhadalaha abhanhu bhenabho kunguno ya gwibhona bhumani kukila abhiye. Uweyi agapandika makoye mpaka ogayiwa umunhu uo gung’wambilija kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’winuyo, agikolaga nuyo oliadabhalonjaga abhiye uyo  agagayiwa ijiliwa ija gulya aha kaya yakwe, kunguno nuweyi agabhasekaga abhanhu abho bhali na makoye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “iyi wib’ona ng’wa ng’wiyo ilolage nuko mili goko.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja bhudoshi bho gubhaseka abhanhu abho bhali na makoye, kugiki bhadule gwiyambilija chiza ugugamala wangu amakoye gabho, umuwikaji bhobho.

Luka 16:19-31.

Ayubu 22:19.

Zaburi 22:6-8.

Mithali 1:26.

 

KISWAHILI: ULIYOONA KWA MWENZAKO JITAZAME NA WEWE MWILINI MWAKO.

Methali hiyo, huangalia maneno yanayotokea kwa watu. Alikuwepo mtu mmoja asiyejali matatizo wanayoyatapata wenzake kwa sababu ya majivuno yake. Siku moja, alikosa chakula nyumbani kwake akaenda kuazima kwa jilani yake. Majirani zake hao, walimsaidia kwa kumwambia kwamba, “uliyoona kwa mwenzako jitazame na wewe mwilini mwako.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwacheka wenzake waliokumbwa na matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, ana majivuno ya kuwadharau watu hao, kwa sababu ya kujiona kuwa mjuani kupita wenzake. Yeye hupata matatizo ambayo humsumbua kwa muda mrefu kwa sababu ya majivuno yake hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule asiyejali shida za wenzake, kwa sababu naye huwacheka wenzake waliokumbwa na matatizo ya maisha.  Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ““uliyoona kwa mwenzako jitazame na wewe mwilini mwako.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwacheka watu waliko kwenye matatizo, ili waweze kusaidiana katika kuyatatua kwa haraka matatizo yao, maishani mwao.

Luka 16:19-31. ‘‘Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa, kila siku. Hapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima. Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kulamba vidonda vyake. ‘‘Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Abrahamu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa. Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake. Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Abrahamu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’ “Lakini Abrahamu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu. Zaidi ya hayo kati yetu na ninyi huko, kumewekwa shimo kubwa, ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko wasiweze, wala mtu ye yote asiweze kuvuka kutoka huko kuja kwetu.’ “Akasema, ‘Basi, nakuomba, umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, maana ninao ndugu watano. Awaonye, ili wasije nao wakafika mahali hapa pa mateso. “Abrahamu akamjibu, ‘Ndugu zako wana Mose na Manabii, wawasikilize hao.’ “ ‘Yule tajiri akasema, ‘Hapana, baba Abrahamu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.’ “Abrahamu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Mose na manabii, hawataweza kushawishiwa hata kama atafufuka mtu kutoka kwa wafu.’ ””

Ayubu 22:19. “Wenye haki wanaona maangamizi yao na

kufurahi nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema,…”

Zaburi 22:6-8. “Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza na watu wamenidharau Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao: Husema, “Anamtegemea BWANA, basi BWANA na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.’’”

Mithali 1:26. “mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,

nitawadhihaki wakati janga litakapowapata,…”

people---1

 

model-1

fish-market-1

ENGLISH: WHAT YOU SAW TO YOUR COMPANION LOOK AT YOURSELF IN YOUR BODY.

This proverb looks at events that happen to people. There was one man who did not care about problems of his colleagues because of his arrogance. One day, he ran short of food at his house and went to borrow it from his neighbor. His neighbor helped him by telling him that, “What you saw in your companion look at yourself in your body.”

This proverb is related to a man who laughs at his troubled fellows in his life. This man becomes proud at looking down on people who suffer from various tribulations, because he thinks of him being better than others. He gets into trouble that bothers him for a long time because of his arrogance, in his life.

This person resembles the one who did not care about problems of others, because he also laughs at his fellows who face problems in life. That is why people say to him that, “What you saw in your companion look at yourself in your body.”

This proverb imparts in people an idea on stopping to laugh at people who are in troubles, so that they can quickly help each other in solving various problems in their lives.

Luke 16: 19-31 ‘‘There was a rich man dressed in purple and fine linen, who lived in luxury, every day. At the door was a man named Lazarus, who had been crippled all his life. Lazarus longed to be satisfied with the crumbs that fell from the rich man’s table. Even the dogs would come and lick his sores. ‘‘ The time came when the poor man died, and the angels took him and stayed with Abraham. The rich man also died and was buried. And in hell he lift up his eyes, being in torments, and seeth Abraham afar off, and Lazarus in his bosom. So he called out to him, ‘Father Abraham, have mercy on me and send Lazarus to dip his finger in water and cool my tongue, for I am in great pain in this fire.’ “But Abraham replied, ‘Son, remember that in your lifetime you have received your reward. good things, but Lazarus got bad things. But now he is comforted here and you are in great pain. And, behold, there is a great gulf fixed: so that they which would pass from hence to thee cannot; neither can they pass to us, that would come from thence. And he said, I pray thee therefore, send Lazarus to my father’s house, for I have five brethren; Warn them, lest they also come into this place of torment. “Abraham replied, ‘Your brothers have Moses and the Prophets; listen to them.'” ‘The rich man said,’ No, father Abraham, but if someone from the dead goes to them, they will repent. ‘”Abraham said to him,’ If they do not listen to Moses and the prophets, to be persuaded, though one shall rise from the dead. ‘”

Job 22:19 “The righteous themselves will see and certainly perish

rejoicing with the innocent mocks them, saying,… ”

Psalm 22: 6-8 “I am a worm, and no man; a reproach of men, and despised of the people. All that see me mock me, they make fun of me, they shake their heads: They say,” He trusts in the LORD; let him deliver him. ” Let him deliver him, since he delights in him. ‘”

Proverbs 1:26 “… I will laugh at your calamity,

I will mock them when disaster strikes them,… ”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.