Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya Nzob’e. Nzob´e ili ndimu iyo idab´ohiyagwa gunguno idashemagwa. Indimu yiniyo, idalemejaga ung´wana ugonhya amab’ele gabho. Kuyiniyo lulu, idiho nguno ya guibhohya, kunguno idina bhuhub’i bhose bhose. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “nzob’e idab’ohiyagwa.”
Ulusumo lunulo, lugalenganiyigwa kuli munhu uyo agikalaga chiza na bhanhu umukajile kakwe. Umunhu ng’wunyo, agabhambilijaga abhiye abho bhali na makoye bho kujibhinha ijikolo ijo jigafumilaga mumatwajo ga milimo yakwe. Uweyi apandikaga bhageni bhingi aha kaya yakwe, kunguno ya likujo ilo alinalyo ukubhiye bhenabho, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunyo, agikolaga ni nzob’e iyo idab’ohiyagwa kunguno, nu weyi agatumamaga milimo yakwe chiza, bho nduhu uguhadikijiwa, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “nzob’e idab’ohiyagwa.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwikomeja gutumama milimo yabho chiza, bho nduhu guhadikijiwa, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umu milimo yabho.
Ulusumo lunulo, hangi lolanga bhanhu higulya ya guleka gubhib’onela abhanhu abho bhadina bhuhubhi bhose bhose, umuwikaji bhobho.
Isaya 42:3.
Marko 5:3-4.
KISWAHILI: PUNDA HAFUNGWI KAMBA MIGUUNI:-
Methali hiyo, huongelea juu ya Punda. Punda ni myama asiyefungwa kamba miguuni mwake kwa sababu huwa hakamuliwi. Mnyama huyo, huwa hamnyimi mtoto wake kunyoma maziwa yake. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kumfunga kamba miguuni mwake mnyama huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “punda hafungwi kamba miguuni.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huishi vizuri na watu katika mwenendo wake wa maisha. Mtu huyo, huwasaidia wenzake walioko kwenye matatizo kwa kuwapatia mahitaji yao kutoka kwenye mapato ya kazi zake. Yeye hupata wageni wengi kwenye famiia yake, kwa sababu ya heshima aliyo nayo kwa wenzake hao, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule Punda asiye fungwa kamba miguuni, kwa sababu naye hufanya kazi zake vizuri, na bila kulazimishwa, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “punda hafungwi kamba miguuni.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yao, bila kushurutishwa, ili waweze kupata mafanikio mengi katika kazi zao.
Methali hiyo huyo pia kuwafundisha watu juu ya kutotoa adhabu kwa mtu au kitu kisichokuwa na kosa lolote.
Isaya 42:3. “…mwanzi uliopondeka hatauvunja na utambi ufukao moshi hatauzima. Kwa uaminifu ataleta haki,…”
Marko 5:3-4. “Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo, kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa kwa minyororo mikononi na miguuni, akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu ye yote aliyekuwa na nguvu za kumzuia.”
ENGLISH: A DONKEY IS NOT TIED BY ROPE TO THE LEGS.
This proverb speaks of the Donkey. A donkey is an animal that is not tied by rope to its legs because she is not milked. This animal does not deprive her baby of her milk. Therefore, there is no need to tie her around her legs. That is why people say that, “A Donkey is not tied by rope to the legs.”
This proverb is equaled to the person who lives well with people in his or her way of life. This person, in turn, assists colleagues who are in need by providing them with their basic needs from the income of his or her works. He/she finds many visitors in the family, because of the respect he/she has to others.
This person resembles the Donkey that was not tied by ropes in her legs, because he/she also does work well, and without compulsion, in life. That is why people say to him/her that, “A Donkey is not tied by rope to the legs.”
This proverb imparts in people a clue on how to work hard enough to fulfill their responsibilities, without coercion in their societies, so that they can be more successful in their works.
The same proverb also teaches people about not punishing a person or thing without any guilt.
Isaiah 42: 3. “A bruised reed he will not break, and a smoldering wick he will not quench. He will faithfully bring justice,… ”
Mark 5: 3-4 “This man lived in the tombs, and no one could bind him, no, not with a chain; for he had often been bound with fetters and chains, and the chains had been torn apart by him, and the fetters broken in pieces. No one had the power to stop him. ”