891. NDUHU UNFULA UKUNU WELELO.

Olihoyi munhu umo, uyo wikalaga muchalo ja Ng’watuju. Umunhu ng’winuyo, oliakumukile giki alinfula noyi umuchalo jinijo. Lushigu lumo, agiduma na nzenganwa okwe mpaga bhiza bhanhu gubhayangula na gubhona giki uweyi alimhubhi. Abhanhu aho bhabhona chene bhagakumywa noyi kunguno yalilukangala lo gwandya uweyi ugwigela na bhuhubhi. Hunagwene abhanhu bhagayonga giki, “nduhu infula ukunu Welelo.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyolechaga giki ali owiza, aliyo umunholo yake agabhizaga na miganiko ga bhub’i, umukikalile kakwe. Umunhu ng’winuyo, agayombaga mihayo ya wiza, aliyo munholo yakwe agiganikaga mihayo ya bhub’i ukubhiye. Uweyi agatumamaga milimo yakwe bho gwiyolecha kubhanhu kugiki bhankumilije, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ng’wikaji o muchalo ja Ng’watuju, uyo aganhubhila unzenganwa okwe aliyo wigelaga giki aliyo wiza, kunguno nuweyi agiyolechaga ukubhanhu giki alinfula aliyo agiganikaga ya bhubhi, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “nduhu unfula ukunu Welelo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya guwiza bhanhu bha nhana  bho gubhiganikila na gubhiwitila ya wiza abhichabho, kugiki bhadule gwikala chiza na bhanhu bhabho, umuwikaji bhabho.

Mathayo 23:25-28.

Yakobo 1: 26-27,

Yakobo 3: 5-7.

KISWAHILI: HAKUNA MKAMILIFU HUKU DUNIANI.

Alikuwepo mtu mmoja aliyeishi katika kijiji cha Mwatuju. Mtu huyo, alisifika kuwa ni mkamilifu katika kijiji hicho kwa kadiri alivyoonekana kwa watu hao. Siku moja, alikosana na jirani yake mpaka wakaja watu kuwaamua, na kugundua kuwa yeye alikuwa na kosa. Watu walipoona hivyo walishangaa sana kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza kwake kupatikana na kosa. Ndiyo maana walisema kwamba, “hakuna mkamilifu huku duniani.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujionesha kwa nje kuwa ni mwaminifu, lakini kwa ndani huwa na mawazo maovu moyoni mwake, katika maisha yake. Mtu huyo, huongea maneno mazuri lakini moyoni mwake huwa anawaza maovu. Yeye hutenda matendo kwa lengo la kujionesha kwa watu ili wamsifu, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule mkaaji wa kijiji cha Mwatuji, aliyekosana na jirani yake, akapatikana na kosa wakati alionekana kuwa ni mwema, kwa sababu naye hufanya kazi zake kwa lengo la kujionesha kwa watu kuwa ni mwema wakati huwa ana anawawazia maovu wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “hakuna mkamilifu huku duniani.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa wakweli kwa kuwaza na kutenda matendo mema kwa wenzao, ili waweze kuishi vizuri na watu wao, maishani mwao.

Mathayo 23:25-28.

Yakobo 1: 26-27,

Yakobo 3: 5-7.

people----

falling-

 

modelo-mocambicana-

 

ENGLISH: NO ONE IS PERFECT IN THIS WORLD.

There was one man who lived at Mwatuju village. He was known to be perfect in the village as he so appeared to the people. One day, he quarreled with his neighbor until people came to reconcile him, and discovered that he was wrong. When the people saw this, they were amazed because it was the first time that he had been found guilty. That is why they said, “no one is perfect in this world.”

This saying is compared to a person who outwardly appears to be faithful, but inwardly has evil thoughts in his heart. This person speaks good words but in his heart there are evils. He does works for the purpose of showing off to people who can praise Him, in His life.

This man is like the resident of Mwatuji village who was found guilty after quarreling with his neighbor while he appeared to be good, because he also does his work with the aim of showing himself to be good when he thinks evil about his fellows, in life. That is why people say to him that, “no one is perfect in this world.”

This saying imparts in people an idea how to be honest by thinking and doing good deeds to their fellows, so that they can live harmoniously with their people, in their lives.

Matthew 23: 25-28.

James 1: 26-27.

James 3: 5-7.

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.