877. KALAGU – KIZE. BHULI LUSHIGU AGUZENGAGA NDUHU YALEMA UGUSHILA NZENGA – NSWA.

Ikalagu yiniyo, ilolile kikalile ka nswa. Unswa jilisunbwa ijo jigikalaga jiguzengaga bhuli lushigu. Aliyo lulu, inzenga yago idashilaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “bhuli lushugu aguzengaga nduhu yalema ugushila inzenga – Nswa.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo mingi bhuli lushiku, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agandyaga gutumama milimo mitale ni midoo mingi halumo. Uweyi agapandikaga sabho ja gung’wambilija uguibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya wigulambija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nswa uyo gudamalaga nzenga, kunguno nuweyi agatumama bhuli lushiku umumilimo yakwe imitale ni midododo, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “bhuli lushugu aguzengaga nduhu yalema ugushila inzenga – Nswa.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo bho witegeleja bhutale, kugiki bhadule gupandika sabho ja gubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Waroma 12:11-12.

Mathayo 24:13.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KILA KUKICHA ANAJENGA NA UJENZI HAUJAISHA – MCHWA.

Kitendawili hicho, huangalia maisha ya mchwa. Mchwa ni kiumbe ambacho huwa kinajenga kila siku. Lakini, ujenzi wake huwa hauishi. Ndiyo maana watu walianza kuhadithiana kwamba, “kila kukicha anajenga na ujenzi haujaisha – mchwa.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi nyingi kila siku, katika maisha yake. Mtu huyo, huanza kutekeleza majukumu makubwa huku akiwa anaendelea na kazi ndogo ndogo nyingi kwa pamoja. Yeye hupata mali za kumsaidia katika kuiendeleza vizuri familia yake, kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kuedelea kuyatekeleza majukumu yake ya kila siku, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na mchwa aliyejishugulisha kufanya kazi kila siku, kwa sababu naye hujishugulisha kila siku katika kuyatekeleza majukumu yake ya kuiendeleza familia yake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kila kukicha anajenga na ujenzi haujaisha – mchwa.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujibidisha katika kuyatekeleza majukumu yao kwa umakini mkubwa ili waweze kupata mali za kuziletea maendeleo familia zao, maishani mwao.

Waroma 12:11-12.

Mathayo 24:13.

ant-1

 

ant-

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.