Akahayile kenako, kalolile bhulagwa bho ginhu na guru. Uguru ali munhu uyo adigwaga iyo aliwilwa na bhiye kunguno amatu gakwe gagab’izaga guti gachib’ile. Umunhu ng’wunuyo, ulu ulolela lwande luleb’e adadulile ugugaluchiwa na mhayo gosegose, kunguno adigwaga imihayo iyo aliwilwa na bhiye. Uweyi uko ulolela na kwene adagalukaga. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “lyalagwa guru.”
Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajaga kumilimo ogatumama chiza mpaga oyimala, bho ng’holo yape, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agaidililaga imilimo yakwe bho gwigulambija kuitumama chiza mpaka uishisha bhuli makanza. Uweyi agapandikaga sabho ningi kunguno ya guitumama imilimo yakwe yiniyo mpaga, guimala bho nduhu uguileka, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu guru uyo adagaluchiyagwa na mhayo gosegose uko olelaga, kunguno nuweyi agaidililaga chiza imilimo yakwe bho gwigulambija guitumama mpaga oimala, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “lyalagwa guru.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho mpaga guimala bho nduhu uguileka, kugiki bhadule gupandika sabho ja gubhambilija ugujib’eja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Mathayo 24:13.
Waroma 12:11.
Ufunuo 2:10.
KISWAHILI: LIMEAGWA NA KIZIWI.
Msemo huo, huangalia uagwaji wa kitu na kiziwi. Kiziwi ni mtu yule ambaye huwa hasikii yale anayoambiwa na wenzake kwa sababu ya masikio yake kuwa kama yameziba. Mtu huyo, akiangalia upande fulani huwa hawezi kugeuzwa na nelo lolote, kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kuyasikia maneno anayoambiwa na wenzake. Yeye alikoangalia ndipo huko hageuki. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “limeagwa na kiziwi.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huenda kwenye kazi na kuzitekeleza vizuri mpaga kuzimaliza, kwa moyo mweupe, katika maisha yake. Mtu huyo, huzijali kazi zake kwa kujibidisha kuzitekeleza vizuri kila wakati. Yeye hufanikiwa kupata mali nyingi kwa sababu ya kuzitekeleza kazi zake hizo mpaga kuzimaliza bila kuziacha, katika maisha yake.
Mtu huyo, hufanana na yule kiziwi asiyegeuzwa na neno lolote alikoelekea, kwa sababu naye huzijali vizuri kazi zake kwa kujibidisha kuzitekeleza mpaka kuzimaliza, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “limeagwa na kiziwi.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yao mpaka kuyamaliza bila kuyaacha, ili waweze kupata mali za kuwasaidia katika kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.
Mathayo 24:13. “Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka. ”
Waroma 12:11. “Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.12Iweni na furaha katika tumaini, katika dhiki iweni na saburi, dumuni katika maombi.”
Ufunuo 2:10. “Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
ENGLISH: IT HAS BEEN GIVEN FARE-WELL BY THE DEAF.
This saying looks at a being given fare well of someone by a deaf person. A deaf person is the one who does not hear what his or her fellows say because of his or her ears which seem to be blocked. Such person if he/she looks in a certain direction cannot be turned back by anyone, because of his/her inability to hear words which are spoken by others. He/she just focuses in such direction without turning back. That is why people say to him/her, “it has been given fare-well by the deaf.”
This saying is likened to a man who goes to work and performs it well to the end in good faith. Such person, in turn, takes care of his responsibilities by striving to accomplish them at all times. He manages to make a lot of money because he is capable of doing all what he can in his life.
This person resembles to a deaf person who was not distracted by a word in working, because he also cares for his work by striving enough to complete it in his life. That is why people say to him, “it has been given fare-well by the deaf.”
This saying teaches people on how to work hard enough to fulfill their responsibilities to the end without leaving them, so that they can have all needed resources for developing their families, in their lives.
Matthew 24:13 “But the one who endures to the end will be saved.”
Romans 12:11 “Not slothful in business; fervent in spirit; serving the Lord. 12Rejoice in hope, be patient in tribulation, be constant in prayer.”
Revelation 2:10. “Do not be afraid of the things you are about to suffer. I tell you, Satan will throw some of you into prison to test you, and you will have tribulation for ten days. Be faithful until death, and I will give you the crown of life.”