Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola iwe lya gushela na sho jalyo ijo jigatumamaga kihamo nalyo. Iliwe linillo ni sho jalyo jinijo, jigashilanijaga kunguno ya bhutumamilwa bhojo bho milimo ubho bhugabhizaga bho kihamo, na gukomangwa kihamo na bhashi bha bhufu. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “iwe na sho jalyo jigashilanijaga – bhanhu bhitolile.”
Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhitolile ngosha na nkima, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagakulanijaga kihamo umukikalile kabho mpaga binamhaja nulu bhigiguluhya. Abhoyi bhagikalaga kihamo gwingila hawitoji bhobho mpaga kwikanza lya gwinga kuwelelo.
Abhanhu bhenabho, bhagiikolaga niliwe kihamo ni sho jalyo umo jigatumamilagwa kihamo mpaga jashilanija, kunguno nabhoyi bhagiyumilijaga bho gwikala bhutumama kihamo na witogwi mpaga bhigiguluhya na gwinanhaja, umukikalile kabho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki “iwe na sho jalyo jigashilanijaga – bhanhu bhitolile.”
Ikalagu yiniyo, yalanga bhitoji higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gwikala kihamo bhitogilwe bho pye shigu jabho, kugiki bhadule gwikomeja gutumama milimo yabho bho gwiyambilija chiza uguyilang’hana ikaya yabho, umuwikaji bhobho.
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.
JIWE NA KISAGIO CHAKE HUISHA PAMOJA -WATU WALIOOANA.
Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia jiwe la kusagia na visagio vyake ambavyo ni mawe madogo madogo ambayo yote huisha pamoja nalo. Jiwe hilo na masagio yake hayo huisha kwa pamoja na lenyewe kwa sababu ya kutumiwa kwa pamoja na msagaji wa unga, na kupigwa pigwa pamoja katika kuwekewa makali ya kusaga nafaka kwa urahisi. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “jiwe na kisagio chake huisha pamoja – watu waliooana.”
Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu waliooana ambao ni mume na mke, katika maisha yao. Watu hao, hukua kwa pamoja katika maisha yao mpaka wanazeheshana. Wao huishi na kufanya kazi zao kwa pamoja kuanzia pale wanapooana mpaka kufikia wakati wa kuaga dunia.
Wana ndoa hao, hufanana na lile jiwe ambalo hufanya kazi na kisagio chake mpaka kufikia hatua ya kuisha pamoja, kwa sababu nao wana upendo wa kuvumiliana kwa kuishi pamoja wakisaidiana mpaka kuzeheshana katika maisha yao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “jiwe na kisagio chake huisha pamoja – watu waliooana.”
Kitendawili hicho, chafundisha watu wa ndoa juu ya kuwa na uvumilivu na upendo wa kuishi pamoja siku zote za maisha yao, ili waweze kujibisha katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao kwa kusaidiana katika kuilinda familia yao, maishani mwao.
Waefeso 5:21-25.
Marko 10:1-9.
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.
THE GRINDER STONE AND ITS GRINDING STONE GET FINISHED TOGETHER – MARRIED PEOPLE.
The cradle of this riddle looks at the grinder stone and its grinding one which is a small stone that get finished up with it. Such grinder stone and its stone get finished together because they are broken off by their co-operation. They grind flour together after being sharpened by being beaten by person who uses them. They all carry on being broken slowly to point of getting finished together. That is why people say to one another that, “the grinder stone and its grinding one get finished together – married people.”
This riddle is compared to the married people who are husband and wife, in their lives. These people, grow together in their lives until they become old. They live and work together from the time they get married until the time of passing away one of them.
These couple resembles the grinder stone that worked with its grinding stone to the point of exhaustion, because they also love to tolerate each other by living together and helping each other to the point of exhaustion in their lives. That is why people tell them that, “the grinder stone and its grinding one get finished together – married people.”
This riddle instills in married people and idea on how to have patience and love one another enough to live together for the rest of their lives, so that they can focus on fulfilling their responsibilities of helping each other in protecting their family.
Ephesians 5: 21-25.
Mark 10: 1-9.