Imbuki ya lusumo lunulo ingilile kubhulemi bho ng’holo ya ng’wa munhu umo. Umunhu ng’wunuyo, agahaya guja lugendo halebhe, wiyangula giki aleke kunguno ing’holo yakwe yaliyalema.
Oho oleka uguja uko oliajile agigwa giki, iloli iyo ohayaga gwibakila yapingukaga mpaka yulabhula na gubhulaga bhanhu. Agamana igiki, gashiganaga ulu niosimiza niopandika ajali. Umunhu ng’wunuyo, agenhelwa masugu ga nduguye giki ozumalikaga. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agayomba giki, “ng’holo igamanaga.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agaidegelekaga chiza ing’holo yakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’winuyo, agaligwaga ililaga lya mung’holo yakwe ilo ligayegaga chiza uluwita mihayo yawiza. Uweyi hangi agailekaga uguita imihayo iyo iliyabhubhi, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agaleka uguja ulugendo lokwe aho yanemeja ing’holo yakwe, kunguno nuweyi agaigwaga ing’holo yakwe na gwita umo yiling’wilila, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “ng’holo igamanaga.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guligwa ililaga lya ng’holo jabho na guita imihayo iyawiza, kugiki bhadule gwikala bho mholele chiza na bhichabho, umuwikaji bhobho.
Yohane 15:36-38.
Mathayo 26:45-46.
Marko 9:30-32.
KISWAHILI: MOYO HUTAMBUA.
Chanzo cha methali hiyo, chaangalia ukataaji wa moyo wa mtu mmoja. Mtu huyo, alitaka kusari kwenda sehemu, akaahirisha kwa sababu ya moyo wake kukataa kwenda huko.
Alipoahirisha kwenda safari yake, muda mfupi baadaye alisikia kwamba, lile gali alilotarajia kusafiria limepata ajali ya kuumiza na kuua baadhi ya wasafiri. Akaelewa kwamba, kumbe angekuwemo na yeye kwenye ajali hiyo endapo asingeacha kwenda. Mtu huyo aliletewa habari za msiba wa ndugu yake aliyefariki. Ndiyo maana mtu huyo alisema kwamba, “moyo hutambua.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huisikiliza vizuri dhamiri ya moyo wake, katika maisha yake. Mtu huyo, huifuata sauti hiyo ya dhamiri ya moyo wake kwa kuyatekeleza yale yaliyo mema na kuyakataa yale yaliyo maovu. Yeye huishi kwa kuongozwa na dhamiri yake hiyo iliyo njema.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyeadhirisha safari yake baada ya moyo wake kukataa, kwa sababu naye huisikiliza dhamiri ya moyo wake na kufuata inavyomweleza, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “moyo hutambua.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzisikiliza na kuzifuata vizuri sauti za dhamiri ya mioyo yao kwa kuutekeleza kwa makini ushauri huo wa kutenda matendo mema, na kuyaacha yale yaliyo maovu, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, katika maisha yao.
Yohane 15:36-38.
Mathayo 26:45-46.
Marko 9:30-32.
ENGLISH: THE HEART KNOWS.
The cradle of the overhead proverb looks at the denial of the heart of a man. Such man wanted to go somewhere but he postponed because his heart refused to go there.
As he was about to leave, a short time later he heard that the car that he was expecting to travel with had crashed to the point of killing some of the passengers. He understood that he would be involved in such accident if he could travel. He was also informed of the tragedy of his deceased brother. That is why he said that “the heart knows.”
This proverb is likened to a man who listens well to the conscience of his heart, in his life. Such person follows the voice of his conscience by practicing what is good and rejecting what is evil. He lives by following his clear conscience.
Such person is alike the one who stopped his journey after his heart refused, because he also listens to his conscience enough to follows what it tells him, in his life. That is why he says, “the heart knows.”
This proverb teaches people on how to listen to their conscience by carefully applying the counsel of doing what is good, as well as turning away from evil, so that they may live peaceably with one another, in their lives.
John 15: 36-38.
Matthew 26: 45-46.
Mark 9: 30-32.