1478. HEMBAGA NYAGA UDIZUNIJANANIJA.

Akahayile kenako kahoyelile bhuhembi bho nyaga ntale. Unyaga gunuyo gugakenagulaga kunguno gugabhuchaga ginhu jidito ja mbika na mbika. Ugoyi gugabhuchaga bhanhu na gusambula manumba kunguno ya bhuhembi bhogo bhunubho. Hunagwene umunhu ng’wenuyo agayombaga giki, “hembaga nyaga udizunijananija.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agasataga witegeleja bho guja kubhugota wangu, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, agasataga oja gusitali wangu ogapandika bhugota kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agagulanhanaga chiza umili gokwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo wilalanhaga mpaka oleka guchalwa na nyaga, kunguno nuweyi agasata oja wangu kusitali ogalagulwa mpaka opila wangu umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “hembaga nyaga udizunijananija.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guyilanhana chiza imimili yabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 14:24.

Marko 4:37.

Matendo 27:7.

KISWAHILI: VUMA UPEPO USINIPEPERUSHE.

Msemo huo huongelelea upepo mkali. Upepo huo huharibu vitu mbalimbali kwa sababu ya uwezo wake wa kubeba vitu vizito vya aina mbalimbali. Wenyewe hubeba watu na kuharibu majumba kwa sababu ya ukali wake huo. Ndiyo maana mtu huuambia upepo huo kwamba, “vuma upepo usinipeperushe.”

Msemo huo hulingananishwa kwa mtu yule ambaye ana umakini wa kwenda hospitalini kila anapougua, katika maisha yake. Mtu huyo, huugua na kwenda hospitalini kupata matibabu haraka kwa sababu ya umakini wake huo, maishani mwake. Yeye huulinda vizuri mwili wake kwa sababu ya umakini wake huo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyejihadhali alipotaka kuchukuliwa na upepo mkali, kwa sababu naye huenda hospitali mapema kutibiwa mpaka anapona, maishani mwake. Ndiyo maana husema kwamba, “vuma upepo usinipeperushe.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzilinda vyema afya zao ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Mathayo 14:24.

Marko 4:37.

Matendo 27:7.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.