Aho kale bhalihoyi bhanhu bhadatu abho bhali kihamo umulugendo lobho. Umo obho oliotuula jikolo umumhinda yakwe ukunu nabhiye bhadebhile igiki alinajo. Umunhu ng’wunuyo, agajiguma ijikolo jinijo bho nduhu ugumana uweyi kunguno ya bhulekanija bhokwe bhunubho. Uweyi aho ojilola umuoliojitulila agajigaiwa. Hunagwene abhiye bhagang’wila giki “ogumaga.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alingunanija ojikolo jakwe umukikalile kenako. Umunhu ng’wunuyo, agajilekanijaga sagala isabho jakwe mpaga nose jajimila, kunguno ya bhugumanija bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga ukoya na nzala aha kaya yakwe yiniyo kunguno ya gujilekanija sagala isabho jakwe mpaka nose jajimila, umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agajituula sagala ijikolo jakwe mpaga nose jujimila, kunguno nuweyi agajilekanijaga sagala isabho jakwe mpaga nose jajimila, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ogumaga.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujilabhila chiza isabho jabho, kugiki jidule gubhambilija chiza ugujibheja ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.
Ukubhazunya akahayile kenako kalanga bhabhatijiwa higulya ya guilanhana chiza inema ya wejiwa iyo igolechiwaga na ng’wenda gope uyo bhagawilagwa giki bhagushishe mpaga kuli Mulungu guligope chiniko.
Kutoka 12:17.
Hesabu 3:8.
Yohana 21:15-17.
KISWAHILI: AMEDONDOSHA.
Hapo zamani walikuwepo watu watatu waliokuwa pamoja katika safari yao. Mmoja wao aliweka kitu mfukoni mwake na wenzake wakafahamu kuwa na kitu kicho. Mtu huyo, alikidondosha kitu hicho bila ya yeye kufahamu kwa sababu ya kutokujali kwake vitu vyake. Yeye alipokiangalia mfukoni mwake alikikosa mpaka akaanza kukitafuta. Ndiyo maana wenzake hayo, walimwambia kwamba, “amedondosha.”
Masemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvitelekeza hovyo vitu vyake, katika maisha yake. Mtu huyo, huzitelekeza hovyo mali zake mpaka mwishowe zinapotea kwa sababu ya kutokujali kwake huko maishani mwake. Yeye husumbuliwa na tatizo la njaa, yaani tatizo la kukosa chakula, katika familia yake kwa sababu ya kutokuzijali vizuri mali zake hizo, katika maisha yake hayo.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyeweka hovyo kitu chake mpaka akakipoteza, kwa sababu naye huzitelekeza hovyo mali zake mpaka mwishowe zinapotea, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amedondosha.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzitunza vizuri mali zao, ili ziweze kuwasaidia katika kuziendeleza vyema familia zao, maishani mwao.
Msemo huo pia huwafundisha wabatizwa juu ya kuitunza neema ya utakaso inaoneshwa na nguo nyeupe ambayo huambiwa, na mbatizaji, kuwa, waifikishe kwa Mungu ikiwa nyeupe hivyo.
Kutoka 12:17.
Hesabu 3:8.
Yohana 21:15-17.
ENGLISH: HE DROPPED IT.
Once upon a time, three people were traveling together. One of them put something valuable in his pocket, and his companions noticed that he was carrying it. Because of carelessness, the man dropped the item without realizing it. Later, when he checked his pocket, he discovered that it was missing and began to look for it. That is why his companions said to him, “he dropped it.”
This saying is equaled to a person who carelessly neglects his possessions in life. Such a person fails to take good care of what he owns until it is eventually lost. As a result, he may face serious problems, such as hunger and lack of food in his family, because he did not protect and manage his possessions responsibly.
This person is like the one who carelessly put something in his pocket and lost it. In the same way, he neglects his resources until they disappear from his life. That is why people say about him, “he dropped it.”
This saying teaches people to be careful and responsible in taking care of their possessions, so that these possessions may help them develop and support their families well in life.
Spiritually, the saying also teaches the baptized to take good care of the grace of purification symbolized by the white garment they receive at baptism. They are reminded by the baptizer to preserve this purity and present themselves before God clothed in that white garment.
Exodus 12:17.
Numbers 3:8.
John 21:15–17.


