1446. JIGAFULAGWA JILINA MATU.

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile munhu uyo olina matu gawiza. Abhanhu bhang’wilaga imihayo oigwa chiza kunguno olina matu ayo gigwaga chiza pye imihayo yabho. Umunhu ng’wunuyo aliadinhalali umuwikaji bhokwe kunguno ya wigwi bhokwe bhunubho ubho wiza. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “jigafulagwa jilina matu.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina masala masoga agagwiigwa chiza na bhanhu na gugikalana chiza amalange ayo agalangagwa na bhatale bhakwe, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, agabhudegelekaga na guwikalana chiza ubhulungwa ubho agalangagwa na bhatale bhakwe bhenabho, kunguno ya masala gakwe agawiza genayo umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agayibhejaga chiza ikaya yakwe kunguno ya masala gakwe agawiza genayo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo olina matu gawiza ayo giyigwaga chiza imihayo iyo owilagwa na bhiye, kunguno nuweyi agawikalanaga chiza ubhulangwa ubho agalangagwa na bhatale bhakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “jigafulagwa jilina matu.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na masala gagulikalana chiza ililange lya bhatale bhabho kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mathayo 13:1-8.

Marko 4:1-9.

Luka 8:4-8’

KISWAHILI: HUFUNDISHWA ALIYE NA MASIKIO.

Chanzo cha methali hiyo huangalia mtu yule ambaye ana masikio yenye uwezo wa kusikia vizuri. Watu hulimweleza maneno yao ambayo huyasikia vizuri kwa sababu ana masikio yenye uwezo wa kuyasikia vizuri. Mtu huyo hakuwa mbishi katika maisha yake kwa sababu ya masikio yake kuwa na uwezo mzuri wa kusikia maneno ya wenzake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “hufundishwa aliye na masikio.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana akili nzuri za kuyaishi vizuri malezi anayofundishwa na walezi wake, katika maisha yake. Mtu huyo, huyasikiliza kwa makini na kuyaishi vizuri malezi anayofundishwa na walezi wake hao, kwa sababu ya akili nzuri alizonazo, maishani mwake. Yeye hufanikiwa vizuri katika kuilea vyema familia yake hiyo kwa sababu ya akili yake hiyo nzuri katika kuyaishi vizuri malezi aliyofundishwa na walezi wake.

Mtu hiyo, hufanana na yule aliyekuwa na masikio yenye uwezo wa kusikia vizuri maneno aliyoambiwa na wenzake, kwa sababu naye ana akili nzuri ya kuyaishi vizuri malezi anayopewa na walezi wake, maishani mwake. Ndiyo maana  watu humwambia kwamba, “hufundishwa aliye na masikio.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na akili nzuri ya kuyaishi vizuri malezi wanayopewa na walezi wao, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Mathayo 13:1-8.

Marko 4:1-9.

Luka 8:4-8.

 

ENGLISH: THE ONE WHO HAS EARS IS TAUGHT.

The source of this proverb refers to a person who has ears that can hear well. Such a person listens carefully when others speak to him, and people take time to explain things to him because he understands and values what he hears. He is not careless or foolish in his life, because his ability to listen well enables him to learn from his peers. That is why people say, “the one who has ears is taught.”

This proverb is related to a person who has a good mind and is able to live according to the upbringing taught to him by his guardians. Such a person listens attentively, understands the guidance given to him, and practices it faithfully in his life. Because of this good mind and willingness to learn, he succeeds in raising his own family well, applying the values and discipline he received from his caregivers.

This person is like the one who has ears that hear clearly the words spoken by others. In the same way, he has a mind that is open to instruction and wisdom. Because he listens, understands, and puts into practice what he is taught, people say of him, “the one who has ears is taught.”

This proverb imparts in people an importance of having an open and attentive mind, so that they may live well according to the upbringing given to them by their caregivers and, in turn, raise their families well in life.

Matthew 13:1–8.
Mark 4:1–9.
Luke 8:4–8.

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.