1417. NIBHUKILE.

Aho kale olihoyi munhu uyo oli na bhatumami bhokwe. Abhatumami bhakwe bhenabho bhalibhadantokigishaga umubhutumami bhobho bhunubho kunguno bhatumamaga chayachaya. Hunagwene agayomba giki, “nibhukile.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agaitumamaga chiza imilimo yakwe bho nduhu gulagija bhangi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agigulambijaga gutumama milimo yakwe mpaka oyimala chiza bho nduhu gulagija bhanhu bhangi kunguno ya gutogwa guidilila chiza imilimo yakwe yiniyo umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga na sabho ningi noyi akaya yakwe kunguno ya guidilila bho guitumama chiza imilimo yakwe yiniyo mpaga oyimala chiza umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agibhukila guitumama chiza imilimo yakwe aho bhayitumama sagala abhatumami bhakwe, kunguno nuweyi agaitumamaga mpaga oyimala chiza imilimo yakwe bho nduhu gubhalagija bhanhu bhangi, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “nibhukile.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guyidilila imilimo yabho bho gwigulambija guyitumama mpaga bhayimala chiza, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Ezekieli 34:10-15.

Yohana 10:11-15.

KISWAHILI: NIENDE MWENYEWE.

Hapo zamani alikuwepo mtu aliyekuwa na wafanyakazi wake. Wafanyakazi hao wahakumfurahisha katika utendaji wao wa kazi kwa sababu walifanya kazi hovyo. Ndiyo maana alisema kwamba, “niende mwenyewe.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatekeleza vizuri majukumu yake bila ya kuwaagiza watu wengine, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake mpaga anazimaliza vizuri bila ya kuwaachia watu wengine kwa sababu ya kuzijali vizuri kazi zake hizo, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi sana katika familia yake hiyo kwa sababu ya kuzijali kazi zake hizo kwa kuzitekeleza vizuri mpaga anazimaliza, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo hufanana na yule aliyeenda mwenyewe kuitekeleza vizuri kazi iliyofanywa hovyo na wafanyakazi wake, kwa sababu naye huzitekeleza kazi zake mpaka anazimaliza vizuri bila kuwaagiza watu wengine, maishani mwake.  Ndiyo maana yeye husema kwamba, “niende mwenyewe.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuzijali kazi zao kwa kujibidisha kuzitekeleza vizuri mpaka mwisho ili waweze kupata mali za kutumia vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Ezekieli 34:10-15.

Yohana 10:11-15.

ENGLISH: LET ME GO MYSELF.

Once upon a time there was a man who had his employees. The employees did not please him in their work performance because they did not work well. That is why he said that, “let me go myself.”

This saying is equaled to the person who performs his duties well without ordering other people, in his life. This persons struggles enough to finish his works well without leaving them to other people because of taking decent care of his work in his life. He earns a lot of wealth in his family because of taking care of his work by performing it well, in his life.

This person is similar to the one who went himself to perform the work well done by his employees, because he also performs his works until he nicely completes them without ordering other people, in his life. That is why he says that, “let me go myself.”

This adage teaches people enough to take care about their works by striving to finish them well so that they can obtain decent wealth enough to use in their family lives.

Ezekiel 34:10-15.

John 10:11-15.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.