Untogolwa ali mkima uyo oshoshiwagwa ku ng’wawe gwingila kubhukwiye kugiki agalangwa chiza. Unkima ng’wunuyo agabhalemela abhakubhukwiye kunguno ya bhulambu bhokwe. Uweyi agashoshiwa kung’wawe kugiki agalangwe bhupya. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “umunhu uyu ngotolwa.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adadililaga chiza ililange lya bhatale bhakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adadegelekaga chiza ililange lya bhatale bhakwe ulu bhalinanga kunguno ya bhugumanija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya guduma gulidegeleka chiza ililange lya bhatale bhakwe bhenabho, umukikalile kakwe kenako.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nkima uyo agabhalemela abhabhukwiye kulwa lya bhulambu bhokwe mpaga ushoshiwa kung’wawe, kunguno nuweyi adalidililaga ililange lya bhatale bhakwe mpaga oduma uguyibheja chiza ikaya yakwe, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “umunhu uyu ngotolwa.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gulidimilaga chiza ililange lya bhatale bhabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Zaburi 119:31-37.
Kutoka 4:15.
Zaburi 25:45.
KISWAHILI: MTU HUYU AMERUDISHWA KULELEWA UPYA.
Mtu aliyerudishwa kulelewa upya ni mwanamke aliyepelekwa kwa wazazi wake kutoka kwenye familia ya mume wake kwenda kupewa malezi upya. Mwanamke huyo aliwashinda wanafamilia ya mume wake kwa sababu ya kiburi chake. Yeye alirudishwa nyumbani kwa wazazi wake ili akalelewe upya. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “mtu huyu amerudishwa kulelewa upya.”
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule asiyeyajali vizuri malezi ya wakubwa wake katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hayasikilizi vizuri malezi ya wakubwa wake hao kwa sababu ya kutokujali kwake, maishani mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake kwa sababu ya kushindwa kuyasikiliza vizuri malezi ya wakubwa wake hao, katika maisha yake.
Mtu huyo hufanana na yule mwanamke aliyerudishwa kutoka ukweni kwenda kwa wazazi wake kwa lengo la kulelewa upya, kwa sababu naye huwa hayajali vizuri malezi ya viongozi wake mpaka anashindwa kuilea vizuri familia yake hiyo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtu huyu amerudishwa kulelewa upya.”
Msemo huo hufundisha watu juu ya kuyasikiliza na kuyaishi vizuri malezi ya viongozi wao, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.
Zaburi 119:31-37.
Kutoka 4:15.
Zaburi 25:45.
ENGLISH: THIS PERSON HAS BEEN RE-RAISED.
A person who has been re-raised is a woman who was sent to her parents from her husband’s family to be nurtured again. This woman overcame her husband’s family because of her pride. She was sent back to her parents’ home to be re-raised. That is why people said about her that, “This person has been re-raised.”
This saying is equaled to a person who does not pay proper attention to upbringings of his elders in his life. This person does not listen well to the nurtures of his leaders because of his indifference, in his life. He fails to raise his family well because of his failure to listen well to that rearing of his seniors, in his life.
This person resembles the woman who was sent by her husband back to her parents for the purpose of being nurtured again, because he also does not pay proper attention to the upbringing of his leaders to the point of failing to raise his family well. That is why people say about him that, “This person has been re-raised.”
This saying teaches people about listening to and live well the upbringing of their leaders, so that they can raise their families well in their lives.
Psalm 119:31-37.
Exodus 4:15.
Psalm 25:45.


