1394. AGASIMIZAGA NA MASHIGA GU NOMO.

Amashiga gali mazugilo ayo gagikalaga mawe nulu madifali adatu. Amashiga genayo gagaibhuchaga inungu nulu fulila. Abhanhu bhagabhachaga moto uyo gugikalaga aha gati yago amashiga genayo kunguno ya guzugila jiliwa. Unzugi agafulaga moto bho gutumila nomo gokwe nago gobhaka uyo gugabishaga ijiliwa. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga unzugi ng’wunuyo giki, “agasiminzaga na mashiga gu nomo.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabehaga shigala umukakilile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agajibehaga ishigala jinijo mpaga ofunya lyochi umunomo gokwe guti giki alina mashiga umunomo gunuyo, kunguno ya gukija gugudililaga chiza umili gokwe. Uweyi agajikenagulaga imbazu jakwe bho gubeha shigala jinijo, kunguno ya gugija gugudilila chiza umili gokwe gunuyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo ofulaga moto bho nomo gobhaka mpaga lyafuma lyochi, kunguno nuweyi agabehaga shigala mpaga ofunya lyochi umunomo gokwe gunuyo, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “agasiminzaga na mashiga gu nomo.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya guilanhana chiza imimili yabho bho guleka gubeha shigala, kugiki bhadule gwikala mhola, umukaya jabho.

Mwanzo 19:24-25.

Kutoka 9:23-24.

Waamuzi 15:14.

1Wafalme 1:1.

KISWAHILI: HUTEMBEA NA MAFIGA MDOMONI.

Mafiga ni aina ya jiko la kupikia lenye mawe au matofali matatu. Mafiga hayo hubeba chombo cha kupikia kama vile chungu au sufulia. Watu huwasha moto katikati ya mafiga hayo matatu kwa sababu ya kupika chakula. Mpishi gupuliza moto kwa kutumia mdomo wake ndipo moto huo unawaka ambao hukipika chakula hicho mpaka kukiivisha. Ndiyo maana watu humwambia mpishi huyo kwamba, “hutembea na mafiga mdomoni.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvuta sigala katika maisha yake. Mtu huyo, huvuta sigala hizo mpaka anatoa moshi mdomoni mwake hali ambayo huonekana kama anamafiga mdomoni mwake, kwa sababu ya kutokuujali vizuri mwili mwake. Yeye huyaharibu mapafu yake kwa kuvuta sigala hizo, kwa sababu ya kukosa umakini huo wa kuijali vizuri afya yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule awashaye moto kwenye mafiga kwa kupuliza akitumia mdomo wake mpaka unatoka moshi, kwa sababu naye huvuta sigala mpaka anatoa moshi mdomoni mwake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “hutembea na mafiga mdomoni.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzitunza vizuri afya za miili yao kwa kuacha kuvuta sigala, ili waweze kuwa salama, katika familia zao.

Mwanzo 19:24-25.

Kutoka 9:23-24.

Waamuzi 15:14.

1Wafalme 1:1.

 

ENGLISH: HE WALKS WITH KITCHEN IN THE MOUTH.

A kitchen is a type of cooking stove which has three stones or bricks. These stones or bricks carry a cooking vessel such as pot or saucepan. People light a fire in the middle of these three stones or bricks for cooking food. The cook blows the fire by using his mouth and the fire burns which cooks the food well. That is why people say to the cook that, “he walks with kitchen in the mouth.”

This proverb is equaled to a person who smokes cigarettes in his life. Such person, smokes those cigarettes until he exhales smoke in his mouth, which seems like he exhales it in his mouth, because of not taking respectable care of his body. He damages his lungs by smoking those cigarettes, because of not paying attention enough to take decent care of his health, in his life.

This person is like the one who lights the fire in the three cooking stones or bricks by blowing fire using his mouth until smoke comes out, because he also smokes cigarettes until smoke comes out in his mouth. That is why people say to him that, “He walks with kitchen in the mouth.”

This proverb instills in people an idea of taking virtuous care of their physical health by quitting smoking, so that they can be safe, in their families.

Genesis 19:24-25.

Exodus 9:23-24.

Judges 15:14.

1 Kings 1:1.

 

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.