1381. NAPUGILWA NG’WANANGWA.

Olihoyi munhu uyo wikalaga muchalo jilebhe na Ng’wanangwa okwe. Umunhu ng’wunuyo oli munhu o makoye mingi noyi mpaga nose ung’wanangwa okwe umana unzengi okwe kunguno oliadamalaga imihayo. Hungwene ung’wanangwa okwe aganema nang’hwe uyomba giki, “napugilwa ng’wanangwa.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli ntongeji obhanhu uyo agadumaga ugwiyumilija ulupandikaga makoye umukikalile kakwe. Untongeji ng’wunuyo, agabhapejaga abhanhu bhakwe abho bhagajaga gujuchola wambilijiwa bho gugamala amakoye genayo aha ng’wakwe, kunguno ya gugayiwa wiyumilija bhunubho, umubhutongeji bhokwe. Uweyi agadumaga ugubhatongela chiza abhanhu bhakwe kunguno ya gugayiwa wiyumilija bhunubho, umubhutongeji bhokwe.

Untongeji ng’wunuyo, agikolaga nu ng’wanangwa uyo aganema unzengi okwe uyo olinamakoye, kunguno nuweyi agabhapejaga aha ng’wakwe abhanhu bhakwe abho bhali na makoye ulu bhalichola wambilijiwa bho gugamala amakoye gabho genayo, umubhutongeji bhokwe. Hunagwene bhagayombaga giki, “napugilwa ng’wanangwa.”

Akahayile kenako kalanga bhatongeji bha bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gubhambilija abhanhu bhabho ugugamala wangu amakoye gabho, kugiki bhadule gwikala na bhuyeji umubhutongeji bhobho bhunubho.

Yakobo 5:8.

2 Timotheo 1:8.

1Wakorintho 13:4-7.

1 Petro 2:19.

 

KISWAHILI: NIMETENGWA NA KIONGOZI.

Alikuwepo mtu aliyekuwa akiishi kwenye kijiji fulani na kiongozi wake. Mtu huyo alikuwa mtu wa matatizo mpaka mwishowe kiongozi alimfahamu mwananchi wake huyo kwa sababu alikuwa hamalizi matatizo. Ndiyo maana kiongozi wake huyo alimkataa, naye akasema kwamba, “nimetengwa na kiongozi.”

Msemo huo hulinganishwa kwa kiongozi wa watu yule ambaye hushindwa kuwavumilia watu wake waliopata matatizo, katika maisha yake. Kiongozi huyo, huwafukuza nyumbani kwake watu wake wanaotafuta msaada wa kutatuliwa matatizo yao, kwa sababu ya kukosa uvumulivu huo, katika uongozi wake. Yeye hushindwa kuwaongoza watu wake vizuri kwa sababu ya kukosa uvumilivu huo katika uongozi wake.

Kiongozi huyo, hufanana na yule aliyemkataa mwananchi wake aliyekuwa na matatizo, kwa sababu naye huwafukuza nyumbani kwake watu wake wanaotafuta msaada wa kutatuliwa matatizo yao, katika uongozi wake. Ndiyo maana watu hao,  husema kwamba, “nimetengwa na kiongozi.”

Msemo huo, hufundisha viongozi wa watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuwasaidia katika kuyatatua matatizo ya watu wao, ili waweze kuishi kwa furaha katika uongozi wao.

Yakobo 5:8.

2 Timotheo 1:8.

1Wakorintho 13:4-7.

1 Petro 2:19.

ENGLISH: I HAVE BEEN SEPARATED BY THE LEADER.

There was a man who lived in a certain village with his leader. Such man had a number of problems until his leader recognized him because he did not finish problems. That is why his leader rejected him who said that, “I have been separated by the leader.”

This saying is matched to a leader of people who is unable to tolerate his people who have problems in their lives. Such leader drives away from his home his people who seek help for solving their problems, because of his lack of patience, in his leadership. He fails to lead his people well because of his lack of patience in his leadership.

This leader is similar to the one who rejected his fellow citizen who had problems, because he also drives away from his home his people who seek help for solving their problems, in his leadership. That is why those people say that, “I have been separated by the leader.”

This proverb teaches leaders about being patient by helping their people enough to solve their problems, so that they can live happily under their leadership.

James 5:8.

2 Timothy 1:8.

1 Corinthians 13:4-7.

1 Peter 2:19.

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.