1326. IZUGA LYA MANYANYA NULU HALIMI DUHU JUPYA.

Imbuki ya kahayile kenako ilolile bhuzugi bho manyanya. A manyanya genayo gadi nizuga lidamu kunguno unzugi ogo adulile nulu gugachembagula duhu ugaleka mulimi gupya. Umunhu ng’wunuyo, agagutumamaga unimo gunuyo bho nduhu nulu gunoga. Hunagwene agayombaga giki “izuga lya manyanya nulu halimi duhu jupya.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile gutumama milimo yakwe chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga na milimo mingi iyo aidebhile uguitumama mpaga oyimala chiza kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi noyi aha kaya yakwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho gudebha guitumama mingi chiza chiniko, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo oliadebhile guzuga nyanya chiza, kunguno nuweyi adebhile gutumama milimo yakwe chiza chiniko, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “izuga lya manyanya nulu halimi duhu jupya.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gudebha kutumama milimo yabho chiza chiniko, kugiki bhadule gupandika matwajo  mingi, umuwikaji bhobho.

Ezra 5:8.

KISWAHILI: UPISHI WA NYANYA HATA JUANI TU ZINAIVA.

Chanzo cha msemo huo huangalia upishi wa nyanya. Nyanya hizo hazina mapishi magumu kwa sababu mpikaji wake aweza hata kuzikatakata tu akaziacha juani zikaiva. Mtu huyo huifanya kazi hiyo bila hata ya kumchosha. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “upishi wa nyanya hata juani tu zinaiva.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anaelewa kufanya kazi zake vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo hufanya kazi nyingi anazizoelewa kuzitekeleza mpaga anazimaliza vizuri, kwa sababu ya  umakini wake huo, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi sana kwenye familia yake kwa sababu ya umakini wake huo wa kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi zake hizo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeelewa kupika nyanya vizuri, kwa sababu naye anaelewa kuzitekeleza kazi zake vizuri, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “upishi wa nyanya hata juani tu zinaiva.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi zao zote, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Ezra 5:8.

 

ENGLISH: COOKING TOMATOES EVEN IN THE SUN WILL RIPEN.

The origin of this saying looks at cooking tomatoes. These tomatoes do not have difficult recipes because their cook can even just chop them and leave them in the sun to ripen. This person does this work without even being tired. That is why he says, “Cooking tomatoes even in the sun will ripen.”

This saying is matched to a man who understands how to do his work well, in his life. Such person does several tasks that he understands how to do, and he finishes them well, because of his responsiveness, in his life. He earns a lot of wealth in his family because of his thoughtfulness of understanding and carrying out his tasks well, in his life.

This person resembles the one who understood how to cook tomatoes well, because he also understands how to carry out his tasks well, in his life. That is why he says, “Cooking tomatoes even in the sun will ripen.”

This saying teaches people to be careful enough to understand and carry out all their tasks well, so that they can achieve great success in their lives.

Ezra 5:8.

 

 

woman-5935805__480

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.