Ugub’uka nzule mumho gukolwa mpaga gub’itilija. Olihoyi munhu uyo agigwa mhayo nhebhe ukolwa ub’itilija mpaga uhaya gutulana kunguno goligonminya noyi umunholo yakwe. Uweyi agagayiwa ulubhangu kunguno imihayo igaminyanaga noyi kutinda iyagubhona. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki, “aha wigwa ub’uka nzule.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adinabhushiganu ubho guikengela chiza imihayo iyo agawigwaga umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigwagwa mhayo gosegose ugudilila bho nduhu nulu gugwitila bhukengeji ubho gung’wambilija ugugudebha ulugiki guli go nhana nulu go bhulongo kunguno ya guleka gwitegeleja chiza, umumiganiko gakwe. Uweyi agadumaga uguilela chiza ikaya yakwe kunguno ya guleka guitegeleja chiza imihayo iyo agaigwaga umuwikaji bhokwe bhunubho.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agigwa mhayo upekelana mpaga uhaya kutulana kunguno nuweyi agigwaga mihayo uidilila mpaga yamaja ulubhango, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “aha wiga ub’uka nzule.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guitila bhukengeji imihayo iyo bhagayigwaga gukigi bhadule guidebha iyo idulile gubhambilija ugujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Kutoka 32:10.
2 Wafalme 23:26.
KISWAHILI: ALIPOSIKIA ALIPATA HASIRA KALI.
Hasira hali ni hali ya mtu kukasilika mpaga kupitiliza. Alikuwepo mtu aliyesikia neno fulani akakasilika mpaga akapitiliza hali iliyompelekea kutaka kupigana kwa sababu ya kuumizwa na neno hilo moyoni mwake. Yeye alikosa raha kwa sababu maneno huumiza zaidi kuliko yale ya kuona. Ndiyo maana watu walisema kwamba, “aliposikia alipata hasira kali.”
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hana ukomavu wa kuyafanyia utafiti maneno ayasikiayo katika maisha yake. Mtu huyo, huumizwa na neno analolisikia bila hata kulifanyia utafiti wa kumsaidia kuelewa kama nila kweli au la uongo, kwa sababu ya kukosa umakini wa kuyafikiria vizuri maneno hayo, akilini mwake. Yeye hushindwa kuilea vizuri familia yake kwa sababu ya kukosa umakini huo ya kuyafikiria vizuri maneno ayasikiayo, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyekasilika mpaka akataka kupigana aliposikia neno fulani, kwa sababu naye hukosa raha anaposikia neno fulani bila hata kulifanyia utafiti wa kumsaidia kulielewa vizuri, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “aliposikia alipata hasira kali.”
Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuyafanyia utafiti wa kutosha kuyaelewa maneno wayasikiayo, ili waweze kuyaelewa yale wawezayo kuwasaidia katika kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.
Kutoka 32:10.
2 Wafalme 23:26.



ENGLISH: WHEN HE HEARD HE GOT STRONG ANGER.
An intense anger is a state of a person’s feeling of fury that goes beyond a point of resentment. There was a man who heard a certain word which caused him to feel a strong anger that led him to start fighting because his heart was by that word. He became unhappy in his life. That is why people said that, “when he heard he got strong anger.”
This saying is matched to a person who does not have maturity of researching words which he hears in his life. Such person is hurt by words which he hears without even researching them enough to help him understand whether they have truth or liars, because of not being attentive enough to think well about those words, in his mind. He fails to raise his family well because of not having such attention in his life.
This person is similar to the one who became angry to the point of starting to fight when he heard a certain word, because he also feels uncomfortable when he hears a certain word without even researching it enough to understand it well, in his life. That is why people say to him that, “When he heard he got strong anger.”
This saying imparts in people a clue of being careful to enough study words which they hear, so that they can help them in nurturing their families in their lives.
Exodus 32:10.
2 Kings 23:26.