Akahayile kenako kalolile wiza bho nungu ubho bhuli bho hanze duhu. Olihoyi munhu uyo agayibhona nungu ya wiza uyipelela kunguno ya wiza bhoyo ubho hanze bhunubho. Umunhu ng’wunuyo agaitumila inungu yiniyo mulikanza liguhi duhu yubheleka kunguno yaliidapile chiza umugati yayo. Iyoyi yaliyawiza bho hanze duhu umugati yalitiyawiza. Hunagwene abhanhu bhagang’wila umunhu ng’wunuyo giki, “inungu insoga udizuipelela.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinihanga lyawiza aliyo inholo yakwe iliyabhubhi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agolechaga lihanga lya wiza aliyo inhungwa jakwe jili ja bhubhi kunguno ya miito gakwe agabhibhu ayo agagitaga umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agayisalambanyaga ikaya yakwe kunguno ya nhungwa jakwe ijabhubhi jinijo, umukikalile kakwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nungu iyo yaliyawiza bho guyilola hanze duhu aliyo umugati yaliidapile chiza, kunguno nuweyi agolechaga lihanza lyawiza aliyo inhungwa jakwe jili jabhubhi, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “inungu insoga udizuipelela.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujitila bhukengeji ijikolo jabho ubho bhudulile gubhambilija ugujidebha chiza ijikolo jabho jinijo, kugiki bhadule gujipandika ijawiza ijinagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Ayubu 29:16.
Mathayo 23:27-34.
KISWAHILI: CHUNGU NZURI USIIKIMBILIE.
Msemo huo, huangalia uzuri wa chungu kwa nje tu. Alikuwepo mtu aliyekiona chungu kizuri kwa muonekano wake akakikimbilia kwa sababu ya uzuri wake huo wa nje. Mtu huyo alikitumia chungu hicho kwa muda mfupi tu kikavunjika kwa sababu hakikuiva vizuri kwa ndani. Chenyewe kilikuwa kizuri kwa nje tu lakini kwa ndani kilikuwa kibaya. Ndiyo maana watu walimwambia mtu huyo kwamba, “chungu nzuri usiikimbilie.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana sura nzuri lakini roho yake ni mbaya, katika maisha yake. Mtu huyo, huonesha sura nzuri lakini tabia yake ni mbaya kwa sababu ya matendo yake maovu anayoyatenda, maishani mwake. Yeye huitawanya hovyo familia yake kwa sababu ya tabia yake hiyo ya kutenda maovu, katika maisha yake.
Mtu huyo, hufanana na kile chungu kilichoonekana kuwa kizuri kwa nje lakini kwa ndani ni kibaya, kwa sababu naye huonesha sura nzuri kwa nje lakini kwa ndani tabia yake ni mbaya, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “chungu nzuri usiikimbilie.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuvifanyia utafiti wa kuwawezesha kuvielewa vizuri vitu vyao, ili waweze kuvipata vile vilivyo vizuri katika kuziendeleza familia zao, maishani mwao.
Ayubu 29:16.
Mathayo 23:27-34.
ENGLISH: DO NOT RUN TO A GOOD POT.
This adage stares at an outside beauty of a pot. There was a man who saw a beautiful pot because of its appearance he ran to it. It was only outside beauty not an inside one. He did so because of its external beauty.
Such man used such pot for a short time and it broke because it was not cooked well inside. It was good on the outside but bad on the inside. That is why people said to him that, “do not run to a good pot.”
This saying is matched to the man who has good appearance but his soul is wicked, in his life. Such person, shows a good face but his character is evil because of his wicked deeds which he does in his life. He scatters his family carelessly because of his habit of doing evil in his life.
This person is similar to the pot that looks good on the outside but is bad in the inside, because he also shows a good appearance on the outside but on the inside his behavior is evil, in his life. That is why people tell him that, “do not run to a good pot.”
This saying imparts in people a clue of being careful enough to do research that can enable them to understand their things well, so that they can find what is good for advancing their families, in their lives.
Job 29:16.
Matthew 23:27-34.
