Imbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo wilolaga hilole wibhone giki aliowiza noyi. Umunhu ng’wunuyo, wibhonaga giki abhelelile noyi aliyo oliadogile bho likanza lilihu.
Abhanhu bhamonaga giki abhipilile noyi kunguno ya guleka goga bho shidu ningi. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “kalole kabhalemba bhingi.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agakumilijiyagwa na bhanhu otogwa giki aliowiza, umukikalile kakwe, aliyo umunholo yakwe alina miganiko gabhubhi. Umunhu ng’wunuyo, agatumamamaga milimo yakwe bho guchola gukumilijiwa na bhanhu abho bhalimhona, kunguno ya gwigimba giki, alintumami o wiza aliyo alinamiganiko ga bhubhi, umu ng’holo yakwe. Uwei agadumaga uguyilela chiza ikaya yakwe, kunguno ya kutogwa gukumilijiwa giki alimtumami owiza aliyo agiganikaga mihayo ya bhubhi umu ng’holo yakwe.
Umunhu ng’wunuyo, akikolaga nuyo wilolaga hilole wilemba giki, aliowiza, aliyo oliadogile kulikanza lilihu, kunguno nuweyi atogilwe kuhaiwa giki alintumami owiza aliyo agikanikaga ya bhubhi, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “kalole kabhalemba bhinghi.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulwa ya gwiganika ya wiza iya gubhatogwa bhanhu na gutumama milimo yabho, bho nduhu gulinda gukumilijiwa na bhanhu, kugiki bhadule kujibheja chiza ikaza jabho, umuwikaji bhobho.
1Wakorintho 13:12-2.
2 Wakorintho 3:18.
Yakobo 1:23.
KISWAHILI: KIOO KIMEWADANGANYA WENGI.
Chanzo cha msemo huo, huangalia mtu yule ambaye alikuwa akijiangalia kwenye kioo na kujiona kuwa ni mzuri sana kumbe sivyo. Mtu huyo, alijiiona kuwa anapendeza bila kuuona uchafu wake wa kutokuoga kwa muda mrefu.
Watu walimuona kuwa na muonekano mbaya kwa sababu ya uchafu wake huo wa kutokuoga kwa muda mrefu. Ndiyo maana walisema kwamba, “kioo kimewadanganya wengi.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule anayesifikiwa na watu na kufurahi kwamba ni mzuri, katika maisha yake, wakati moyoni mwake huwaza maovu. Mtu huyo, hufanya kazi zake kwa kutafuta sifa kutoka kwa watu wanaomuona, kwa sababu ya majivuno ya kuitwa mfanya kazi mwema, bila kuacha kuwaza maovu moyoni mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake hiyo kwa sababu ya kupenda kusifiwa kuwa ni mzuri, wakati anawaza maovu moyoni mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyejiangalia kwenye kioo akajidanganya kuwa ni mzuri, wakati alikuwa na uchafu wa kutokuoga kwa muda mrefu, kwa sababu naye hufurahia kusifiwa na watu kuwa ni mzuri, wakati anawaza maovu moyoni mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kioo kimewadanganya wengi.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwaza mawazo mema ya kuwapenda wenzao, na kufanya kazi kwa bidii bila kutegemea kusifiwa na watu, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.
1Wakorintho 13:12-2.
2 Wakorintho 3:18.
Yakobo 1:23.

ENGLISH: THE MIRROR HAS DECEIVED MANY.
The basis of this saying looks at a person who used to look at himself in a mirror and thinks that he is very good-looking while he is not. Such person considered him/herself as being attractive without seeing his dirt because of not taking shower for a long time.
People saw him/her bad appearance because of his/her dirt which was caused by not bathing for a long time. That is why they said that, “the mirror has deceived many.”
This saying is compared to a person who rejoices by being praised by others who tell him, that he is good in his life, while in his heart he thinks evil. Such person does his works by seeking praise from people who see him, because of the pride of being called a good worker, without stopping to think evils in his heart. He fails to raise well his family members because of seeking prestige, while he thinks evils in his heart.
This person resembles the one who looked at himself in the mirror and lied to himself that he was fine-looking, when he had dirt in the body, because he also enjoys being praised by people as being fine-looking, while he thinks evil things in his heart. That is why people tell him that, “the mirror has deceived many.”
This saying teaches people about thinking good thoughts of loving their fellows, and working hard without relying on praise from people, so that they can raise well their family members in their lives.
1 Corinthians 13:12-2.
2 Corinthians 3:18.
James 1:23.