Isoloba kali bala kadoni ako munhu akagatumamaga kugiki adule gukamala na gusola kangi gwingila mu nimo guli ntale. Olihoyi munhu uyo ulimilaga ngese mungunda bho gumana utina kajipande kadoni okalimila mpaga okamala na otina kangi nose mpaga ogumala pye ungunda kunguno goligutale noyi. Hunagwene abhanhu agagitana akabala ako okamililaga kenako giki, “yiniyo soloba.”
Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga bhugagaja na wiyumilija bhokwe bho gutumama milimo mitale mpaga oyimala chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agamishaga diyu ogatumama milimo mitale bho gutumila bhugagaja bho gumana winja kadokado mpaga nose ogumala nimo ntale kunguno ya wiyumilija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga majikolo mingi noyi aha kaya yake kunguno ya gutumama milimo yakwe bho bhugagaja na wiyumilija bhunubho mpaga nose oyimala chiza, umubhutumami bhokwe bhunubho.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agalimila ngunda ntale bho gutina kabala kado kado mpaga nose ugumala chiza, kunguno nu weyi agatumamaga milimo mitale bho gutumila bhugagaja na wiyumilija bhokwe chiza mpaga nose oyimala chiza, umubhutumami bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “yiniyo soloba.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gutumama milimo yabho bho gutumila bhugagaja na wiyumilija bhutale mpaga bhayimale chiza, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umukaya jabho jinijo.
Waebrania 12:14.
KISWAHILI: HIKI NI KIPANDE.
Kipande ni sehemu ndogo ambayo mtu huifanyia kazi ili aweze kumaliza hicho na kuchukua kingine ndani ya shamba kubwa. Alikuwepo mtu aliyekuwa akipalilia palizi kwenye shamba kubwa kwa kukata kipande kidogo kidogo anakimaliza na kuanza kingine mpaka mwishowe akalimaliza kulipalilia shamba lote. Ndiyo maana watu walisema juu ya hicho kisehemu kuwa “hiki ni kipande.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi kubwa kwa kutumia ubunifu na uvumilivu wake mpaka mwishowe anaimaliza vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, huamka asubuhi na kuanza kuyatekeleza majukumu yake hayo makubwa kwa kukata kidogo kidogo mpaka anayamaliza vizuri kwa sababu ya kuutumila vizuri ubunifu na uvumilivu wake, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi sana katika familia yake hiyo kwa sababu ya kuutumia vizuri huo ubunifu na uvumilivu wake, katika kufanya kazi kubwa mpaka anazimaliza vizuri, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyepalilia shamba kubwa kwa kukata kipande kidogo kidogo mpaka akalimaliza shamba lote, kwa sababu naye hufanya kazi kubwa kwa kutumia ubunifu na uvumilivu wake, mpaka anazimaliza vizuri, katika utekelezaji wa majukumu yake hayo. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “hiki ni kipande.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kufanya kazi kubwa kwa kutumila ubunifu na uvumilivu wao vizuri mpaka wanazimaliza, ili waweze kupata mafanikio mengi katika familia zao.
Waebrania 12:14.
ENGLISH: THIS IS A PIECE.
A piece is a small part that a person works on so that he can finish it and take another part in a large field. There was a man who was weeding a large field by cutting a small piece and finishing it and starting another one until he finally finished weeding the whole field. That is why people said about that part that “this is a piece.”
This saying is equaled to a person who does a great job by using his creativity and patience until he finally finishes it well, in his life. Such person wakes up in the morning and begins to carry out his big tasks by cutting little by little until he finishes them well because of using his creativity and patience in his life. He gets a lot of wealth in his family because of using well his creativity and patience, in doing great works until he finishes them well, in his life.
This person is similar to the one who weeded a large field by cutting a small piece until he finished the whole field, because he also does a great job by using his creativity and patience, until he finishes them well in implementing his duties. That is why he tells people that, “this is a piece.”
This saying teaches people about doing great works by instilling their creativity and patience well until they finish them, so that they can get a lot of success in their families.
Hebrews 12:14.
