1219. OMANA NG’WAKA ULWELWE, NG’WANZA MAGEMBE OMALA NG’WAKA.

Bhali hoyi bhalimi abho bhalibhalidebhile ilikanza lwa jidiku. Abhalimi bhenabho bhalolaga lwelwe na ng’wanza magembe. Abhoyi bhajibhonaga ilwelwe bhamana igiki ijidiku jashigaga bhandya gulima kunguno ijinijo jili noni ijo jigijaza ulu jandya ijidiku. Inoni jinijo, ulujingila yolechaga giki ilikanza lya gulima lyashigaga.

Abhalimi bhenabho ulu bhajibhona ing’wanza magembe bhamanaga igiki ung’waka goshilaga kunguno ijinijo jili noni ijo jigizaga hikanza lya ng’waka gulishila golecha giki japunaga chuu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “omana ng’waka ulwelwe, ng’wanza magembe omala ng’waka.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alidebhilie chiza ilikanza lya kutumama milimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga ajimanile chiza ijimanyikiza ja gwandya uigutumama imilimo yakwe yiniyo, kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi noyi aha kaya yakwe, kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umubhutumami bho milimo yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhalimi abho bhalimanaga ilikanza lya gulima bho gubhona lwelwe unabhandya gutumama milimo yabho na kuimala ulu bhabhona ng’wanza magembe, kunguno nuweyi agatumilaga masala gakwe ugulimana ilikanza lya kutumama milimo yakwe, ni lya kuimala, umubhutumami bho milimo yakwe. Hunagwene agayombaga giki, “omana ng’waka ulwelwe, ng’wanza magembe omala ng’waka.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gulidebha chiza ilikanza lya gwigulambija kutumama milimo yabho chiza nilya guimala, kugiki bhadule kupandisha sabho ningi, umubhutumami bho milimo yabho yiniyo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 1:14-18.

2Wafalme 19:29.

KISWAHILI: AMEJUA MWAKA LWELWE, NG’WANZA MAGEMBE AMEMALIZA MWAKA.

Walikuwepo wakulima ambao walikuwa wanaulewa vizuri muda wa masika. Watu hao waliangalia lwelwe na ng’wanza magembe. Lwelwe na ng’wanza magembe ni aina ya ndege ambao huonekana sehemu kuashilia kuanza kwa kipindi cha masika na wengine kipindi cha kiangazi. Wakulima hao, waliwaona lwelwe na kuelewa kuwa kipindi cha mvua yaani masika kimefika kwa sababu ndege hao huja inapoanza mvua kunyesha, yaani kipindi cha masika. Kuingia kwao huonesha kuanza kwa kipindi cha kulima.

Wakulima hao wakiwaona ng’wanza magembe na hutambua kuwa mwaka umeisha kwa sababu hao ni ndege wanaokuja kipindi cha kiangazi kuonesha kwamba mwaka umeisha. Ndiyo maana watu hao walisema kwamba, “amejua mwaka lwelwe ng’wanza magembe amemaliza mwaka.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule anayeulewa vizuri muda wa kuanza kuzitekeleza kazi zake na muda wa kuzimaliza, katika utendaji wa kazi zake. Mtu huyo, huzielewa vizuri dariri za kuanza kwa kazi zake hizo, kwa sababu ya umakini wake huo, maishani mwake. Mtu huyo, hupata mafanikio mengi sana katika familia yake, kwa sababu ya umakini wake huo wa kuelewa muda wa kutekeleza kwa bidii kubwa kazi zake, katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mtu huyo, hufanana na wale wakulima waliouelewa muda wa kuanza kazi zao kwa kuangalia lwelwe na ule wa kuzimaliza kwa kuangalia ng’wanza magembe, kwa sababu naye hutumia vizuri akili zake katika kuuelewa muda wa kuanza kuyatekeleza majukumu yake, katika kazi zake. Ndiyo maana watu husema kwamba, “amejua mwaka lwelwe ng’wanza magembe amemaliza mwaka.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuuelewa vizuri muda wa kuanza kazi zao na kutekeleza kwa bidii kazi zao na ule wa kuzimaliza, ili waweze kupata mafanikio makubwa, katika kazi zao, maishani mwao.

Mwanzo 1:14-18.

2Wafalme 19:29.

ENGLISH: CRANE NATURE BIRD HAS KNOWN THE YEAR, SEASONAL BIRD “NG’WANZA MAGEMBE” HAS FINISHED A YEAR.

There were farmers who nicely knew the rain season. They looked at the crane rain seasonal bird which is traditionally known as “lwelwe” and dry seasonal bird which is traditionally known as ng’wanza magembe. Lwelwe and ng’wanza magembe are types of birds that can be seen in some places at the beginning of the spring period and others in the summer period. The farmers who saw the lwelwe understood that the rainy season has arrived because these birds come when it starts to rain. Their entry marks the beginning of the farming period.

When the farmers see the ng’wanza magembe birds realize that the year is over because these are birds that come during the summer season to show that the rain season is over. That is why those people said that, “crane nature bird has known the year, seasonal bird “ng’wanza magembe” has finished a year.”

This saying is equaled to a person who understands well the time of starting to do his tasks and the time of finishing them, in the performance of his tasks. This person understands well the beginnings of his works, because of his attention, in his life. This person gets a lot of successes in his family, because of his attention to understand the time of carrying out his works with great effort in fulfilling his duties.

This person resembles to those farmers who understood the time of starting their works by looking at the lwelwe and the time to finish it by looking at the ng’wanza magembe, because he also uses his intelligence well in understanding the time to start carrying out his duties, in his works. That is why he says that, “crane nature bird has known the year, seasonal bird “ng’wanza magembe” has finished a year.”

This saying teaches people on how to be careful enough to understand well the time of starting their works and diligently carrying out their works to the point of finishing them, so that they can achieve great successes in their daily works in their lives.

Genesis 1:14-18.

2 Kings 19:29.

stork-21

 

 

 

 

 

 

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.