Imbuki ya kahayile kenako, ilolile bhudoni bho nanha. Unanha kali kanti kadoo aka kadadulile gubheja mbeho ya gudula gunhangija munhu gupya limi. Unanha gunuyo gugatemagwa na kubhejiwa chiza kulonguno ya gwidimilija na kutumamila milimo yingi iyo ikolile na gunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “mbeho ya nanha idunhangija munhu gupya limi.”
Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agisagilagwa ginhu jigehu bho gujiganikila giki, jidulile gung’wambilija hatale, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agilendejaga nulu gutumama milimo yakwe ya gulima iyo idulile gung’wambilija hatale, kunguno ya gusendamila hamo ginhu jidoo guti igunila limo duhu lya mandege, aha kaya yakwe. Uweyi apandikaga makoye ga gugaiwa ijilwa aha kaya yakwe ulu ujimala ijo alijo jinijo, kunguno ya kuleka gwichobhela jikolo ja gudula gung’wambilija hatale, umuwikaji bhokwe bhunubho.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agiiganikilaga imbeho ya nanha giki idadulile gunkinga gupya limi, kunguno nuweyi agisagilagwa ginhu jigehu ulu ujipandika bho kuleka gutumama milimo ya gudula gung’wenhela sabho ja gung’wambilija hatale aha kaya yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “mbeho ya nanha idunhangija munhu gupya limi.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuleka gujisagiilwa jikolo jigehu bho guleka gutumama milimo yabho, kugiki bhadule gwikomeja kuitumama chiza imilimo yabho iya gubhambilija hatale ugujibheja chiza ikaya jabho.
Mwanzo 18:5.
I Wafalme 17:10-16.
KISWAHILI: KIVULI CHA FIMBO HAKIMZUII MTU KUCHOMWA NA JUA.
Chanzo cha msemo huo chaangalia udogo wa fimbo. Fimbo ni mti mdogo na mwembamba usioweza kutengeneza kivuli cha kuweza kumzuia mtu asichomwe na jua. Fimbo hiyo hutengenezwa kwa lengo la kujishikilia na kwa matumizi mengine yanayofanana na hilo. Ndiyo maana watu husema kwamba “kivuli cha fimbo hakimzuii mtu kuchomwa na jua.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutegemea kitu kidogo kwa kukifikiria kwamba kitaweza kumsaidia pakubwa, katika maisha yake. Mtu huyo, hujisahau kiasi cha kuchelewa hata kufanya kazi mbalimbali zikiwemo zile za kulima, baada ya kupata kitu kidogo akitumainia kuwa kitaweza kumsaidia pakubwa, badala ya kujibidisha kukiongeza, katika familia yake. Yeye hukumbwa na matatizo mbalimbali yakiwemo yale ya kukosa chakula katika familia yake hiyo, baada ya kukimalia kile alichokuwa akikitegemea, kwa sababu ya kuacha kujitafutia mahitaji yatakayoweza kumsaidia pakubwa, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule anayekifikiria kivuli cha fimbo kama kitaweza kumzuia kuchomwa na Jua, kwa sababu naye hutegemea kitu kidogo kwa kukifikiria kuwa kitaweza kumsaidia pakubwa, mpaka anaishiwa chakula katika familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kivuli cha fimbo hakimzuii mtu kuchomwa na jua.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kutegemea kusaidiwa pakubwa na kitu kidogo, ili waweze kujibidisha kufanya kazi za kuwaletea mafanikio makubwa katika familia zao.
Mwanzo 18:5.
I Wafalme 17:10-16.
ENGLISH: THE SHADOW OF A STICK DOES NOT PREVENT A PERSON FROM BEING BURNED BY THE SUN.
The origin of this saying looks at the smallness of the stick. A stick is a small and thin tree that cannot create a shade that can prevent a person from getting sunburned. This rod is made for the purpose of holding oneself and for other similar uses. That is why people say that “the shadow of a stick does not prevent a person from being burned by the Sun.”
This saying is equaled to a person who depends on something which is small thinking that it would be able to help him a lot in his life. Such person forgets himself so much that he even does various tasks including farming, after finding something small, hoping that it will be able to help him a lot, instead of increasing it, in his family. He suffers from various problems, such as lack of food in his family, after finishing what he was relying on, because he stopped looking for the needs that will help him a lot, in his life.
This person resembles the one who thinks of the shadow of a stick as being able to prevent him from being burned by the Sun, because he also depends on a small thing thinking that it would be able to help him a lot, until he runs out of food in his family. That is why people tell him that, “the shadow of a stick does not prevent a person from being burned by the Sun.”
This saying imparts in people an idea of stopping relying on a lot of help from little things, so that they can work hard enough to bring them great success in their families.
Genesis 18:5.
I Kings 17:10-16.
